Jinsi ya kupika kabichi pekee na yenye mchanganyiko na mboga za aina nyingine

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
1603028912808.png

Hatua kwa hatua jinsi ya kupika mboga aina ya kabichi
Mahitaji

Kabichi 1/2 kilo

Nyanya ya kopo 1/2

Kitunguu 1

Curry powder 1/2 kijiko cha chai

Chumvi

Olive oil

Matayarisho

Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu.

Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto.

Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
1603027552563.png

*********

Jinsi ya kupika kabichi kwa mayai​

jinsi ya kupika kabichi kwa mayai

Habari mdau wa jinsi ya kupika. karibuni tena katika jiko letu. Leo tuandae mboga ya kabichi. Mboga hii yaweza kupikwa kwa nyama, njegere, yenyewe tu kwa viungoviungo, na aina tofauti tofauti, lakini sisi leo tuipike na mayai, ni nzuri sogea karibu tuandae wote.

Mahitaji​

  • Kabichi 1
  • Mayai 4
  • Mafuta robo
  • Vitunguu 4
  • Nyanya 5
  • Karoti kubwa 1
  • Pilipili manga kiasi
  • Chumvi kiasi kwa ladha

Jinsi ya kupika kabichi hatua kwa hatua​

  1. Andaa kabichi uikatekate kisha uikoshe.
  2. Bandike jikoni iive kidogo kisha iweke pembeni.
  3. Menya nyanya, kata vitunguu na karoti uviweke tayari kwa mapishi.
  4. Bandika sufuria jikoni utie mafuta, yakipata moto tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi kisha tia nyanya ukaange.
  5. Tia karoti kaanga kidogo, tia kabichi, pilipili manga na chumvi, vunja mayai uyapige uyatie. koroga hadi likauke, hapo linakua tayari.
Namna hiyo kabichi yetu liko tayari, linakwenda sambamba na ugali, wali na hata pilau simbaya. Hivi karibuni mungu akipenda tutaandaa kabichi la njegere. karibuni sana.

***********
Kabichi ya nyama

Mahitaji
  • Nyama ya ngombe 1/2 kilo
  • Vitunguu maji viwili
  • Nyanya nne
  • Pilipili hoho nusu
  • Kabichi 1
  • Viazi vinne
  • Karroti 1
  • Njegere nusu kikombe
  • Mafuta vijiko vitatu vya supu
  • Kitunguu saumu
  • Pilipili manga kiasi
Jinsi ya kutayarisha
  1. Kata nyama,osha,weka chumvi,kitunguu saumu na pilipili manga acha chemsha na uikoroge ili viungo vikolee,ongeza maji kuifunika nyama,acha iive
  2. Kata kabichi kama vile unavyokata la kachumbari lioshe na maji ya vuguvugu,Tayarisha kitunguu,nyanya,karoti,viazi vigawe mara mbili.
  3. Injika chungu jikoni,weka mafuta yapate moto,kaanga kitunguu mpaka kibadilike rangi kiwe hudhurungi,weka nyanya,viazi,supu ya nyama na nyama uloichemsha,acha nyanya iive mpaka ipondeke.Na mchuzi uwe mzito.
  4. Weka carrot na njegere pamoja na kabichi.Acha viendelee kuiva sosi ya kwenye kabichi ikikaribia kukauka weka pilipili hoho acha vichemke dakika kadhaa kisha epua.
  5. Ongezea chumvi ikiwa haijatosheleza
Msosi huu ni mzuri ukiula na wali wa nazi au chapati.
1603028078014.png


Mchango wa mdau
Hivi ni nani aligundua kwamba kabichi ni Mboga asee,

Mbona tunatesana hivi si ni bora aliyegundua mrenda japo unatereza lakini ni mwake na ugali kitu kinaenda.

Hivi ugali na kabichi kuna ambae anauelewa kweli ?

Tuache tuseme tu ukweli ni bora nile ugali bila mboga kuliko kula ugali na kabichi.
 
Hivi ni nani aligundua kwamba kabichi ni Mboga asee,

Mbona tunatesana hivi si ni bora aliyegundua mrenda japo unatereza lakini ni mwake na ugari kitu kinaenda.

Hivi ugari na kabichi kuna ambae anauelewa kweli ?

Tuache tuseme tu ukweli ni bora nile ugari bila mboga kuliko kula ugari na kabichi.
Mkuu unamaanisha Kabichi kama ndomu au unamaanisha nini?maana wewe akili zako unazijua mwenyewe.
 
Daaah nimekumbuka kuna jamaa yangu alishawahi kuniambia hawezi kula ugali na dagaa (misumali ya bati) hata siku moja. Mungu fundi bhana, bahati mbaya nyumba yao imeungua na maisha yao yamedrop economically sababu ya ujenzi wa nyumba yao. Maisha anayoishi jamaa nayaelewa mimi anachokula naelewa mimi.

Wewe naweza kusema unamkufuru Mungu kama huyo jamaa yangu, kabichi ni kachumbari tu au sio? Ngoja yakukute mkuu hapo ndio utajua kwanini chips hazina ukoko.

This Time Tomorrow
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom