Ni bora IGP Mwema naye akiri kushindwa kama alivyokiri Edward Hosea wa TAKUKURU

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Wiki iliyopoita Hosea alionekana alikiri hadharani kwamba ameshindwa kushugulikia vita dhidi ya rushwa ya vigogo kwa sababu amebanwa mikono na serikali kupitia DPP kwamba anakwamisha kesi zao kufika mahakamani. Kwa mara ya kwanza kabisa nampongeza Hosea kwa kusema kile kilicho cha kweli.

Namuomba naye IGP Mwema afanye hivyo hivyo -- kwamba jeshi lake linashindwa kuwalinda raia ipasavyo kwa sababu limebanwa mikono kwa kuingiliwa sana na wanasiasa. Na huo ndiyo ukweli -- siasa za wakubwa wa CCM ndiyo linaoendesha jeshi hilo na kulifanya kukosa weledi kabisa.

C-mon Mwema -- nawe jitutumue uwe jasiri kidogo kwa kukiri kile cha ukweli.
 
Ni mchumia tumbo tu. Yeye, Kova na wengine walionenepa katika jeshi lake wanatishwa na TISS kwamba lazima wafuate matakwa yao (TISS) ama sivyo wataibua ufisadi wao.

Utawala wa Nchi hii umeshakuwa balaa kubwa!!
 
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
 

C-mon Mwema -- nawe jitutumue uwe jasiri kidogo kwa kukiri kile cha ukweli.

kesho yake atakutwa kwenye msitu wa M.pande la sivyo atafananishwa na jambazi pindi akitoa tamko unalotaka wewe.Sisi Waafrika ni watu wa ajabu sana.....hata whites walio wengi wanashangaa sana life style yetu uwe unaishi ulaya au Marekani.Tunatumia sehem ndogo san ya akili yetu na tunapenda kuchukua simple answer for complicated problem.Wengi watapinga
 
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.

Mkuu kama mnawafahamu nani anawazuia kuwakamata ?kwani mna polis mna jeshi mna Tiss mna mgambo mna greenguard, kama mmeshindwa kuwakamata povu la nini asubhi yote hii mkuu.
 
Watanzania bado hawajaamua kubadilisha nchi yao, mpaka hata mtandaoni. Lakini ukombozi utakuja tu. Hawa akina Mwema hawa wanaotumiwa na waliowachagua badala ya kutumikia wananchi watakuwa na miisho mibaya tu
 
Haitakuja tokea akawa na ujasiri huo wa kujiuzulu.Hawa wote ni MANYANG'AU pepo hii waipatayo kwa gharama za walalahoi hawako tayari kuziachia.hapa bila PEOPLES POWER Inchi inaelekea kuzimu.But there's a day when they'll find no where to hide justice will take it's course.We'll take them to the Gallows.
 
Back
Top Bottom