Ni bora Elimu ya kulipia kuliko ya Bure bila Ubora.

Jef Kirhiku

Member
Dec 10, 2016
39
76
Hivi karibuni nimefanya utafiti juu ya namna sera ya elimu bure inavyotekelezwa katika hali ambayo shule zinapelekewa hela kidogo ukilinganisha na mahitaji na kugundua upo uwezekano hali ya elimu nchini ikazidi kuwa mbaya .Maeneo kadhaa yameathirika ikiwa ni pamoja na :-

1.Maandalizi ya wanafunzi kufanya mitihani ya Kitaifa.
Huko nyuma kamati za wazazi za shule kwa kushirikiana na uongozi wa shule walikuwa wanahakikisha watoto wanaotarajia kufanya mitihani wanaandaliwa vizuri na mapema kwa kutumia hata muda wa ziada ili kumaliza silabus na kufanya mazoezi ya kutosha .
Wazazi walichangia kidogo kwa hiari yao na wasio na uwezo waliruhusiwa kusoma hata bila kuchangia .
Tangu itangazwe elimu bure hakuna mtu anajishughulisha kuhakikisha wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa sylabus inaisha mapema na wanafanya mazoezi ya kutosha .
Shule za binafsi wanahakikisha sylabus zinaisha mapema na wanafunzi wanafanya mazoezi ya kutosha hata nje ya muda wa kawaida wa Vipindi .
2.Kufanyika kwa mitihani mikubwa ya maandalizi kabla ya mtihani wa Taifa .
Zamani ilifanyika mitihani mikubwa ya kutosha kabla ya mtihani wa taifa tena katika mazingira yanayofanana kwa kiwango fulani na yale ya mtihani wa taifa .Mtihani ulitungwa na kusahihishwa kisha matokeo kupangwa kama ule wa taifa .
Kwa kile kinachodaiwa kupunguza garama leo hii mtihani wa mock unaletwa shuleni shule husika wauchape ,ufanyike hapo shuleni na usahihishwe hapo hapo na waalimu walewale .
Hii Ina compromise ubora wa mtihani wenyewe .
Shule za private wao hawakwepi garama bado wanafanya mitihani hii kwa utaratibu ule ule na wazazi wanagaramia mitihani hii .

3.Uhaba wa waalimu hasa wa sayansi na hisabati .
Uhaba wa waalimu si jambo geni isipokuwa hapo nyuma kamati za shule ziliweza kukutana na kutafuta namna ambavyo watoto wao wangeweza kuendelea kufundishwa mpaka serikali itakapoajiri kwa kuazima mwalimu au kuajiri kwa muda waalimu wanaosubiria ajira za serikali .
Hivi sasa kama kuna somo hakuna mwalimu hakuna cha kufanya wanafunzi wanakaa kusubiri mwalimu atakapoajiriwa ndio waanze kusoma .

4.Upatikanaji wa Chakula shuleni kwa shule za kutwa .
Huko nyuma kamati za shule ziliweka utaratibu wa hiari wa kuwapatia watoto chakula ili wasome kwa bila njaa na kwa kutumia muda mrefu .
Tangu elimu itangazwe kuwa bure na marufuku ya kuchangisha sasa ni lazma ratiba za shule zibanwe ili vipindi viishe mapema watoto wakale nyumbani .

Kwa hakika wanasiasa mnavuruga elimu ya nchi yetu .Mnaposema mkisema bure mnamaanisha bure kwelikweli huku hamna uwezo wa kupeleka fedha za kutosha kwa mahitaji ya shule mnamaanisha nini ?
Hivi ni kweli sera inaelekeza marufuku kwa wazazi kuchangia au sera inatamka elimu pasipo ada ?
 
Hata humu JF wamo watu kama hao, kila mada wanataka kuchangia hata kama ni ya kitaaluma wanachangia kwa mawzo ya kinzengo.

Subili waje utawaona!!!
 
Nakubaliana na wewe kabisa.Bure ina gharama kubwa sana na mara nyingi ubora wake ni hafifu.Kama Hospital tunalipia,Maji tunalipia,Umeme tunalipia,Huduma za vyoo tunalipia na karibu kila kitu tunalipia kupitia Kodi mbalimbali,sioni kwa nini Elimu itolewe bure.
Hizi kauli za kisiasa zitauwa Elimu yetu.
 
Ni kweli kabisa mkuu ... Nadhani ilitakiwa wajipange kwa miaka kadhaa ili waweze kutekeleza hii Sera sio gafla hivi ila kwa sababu ya kitaka ridhaa kwa wananchi ikabidi iyo hivyo ..siujua wakati wa kampeni hiyo ilikuwa ajenda muhimu sana..na huu mdororo wa uchumi uliopo sijui huko tuendako itakuwaje katika utekelezaji wa hii sera
 
Back
Top Bottom