Ni biashara gani inafaa kufanywa na mtoto mdogo?

Nikiwa darasa la 5,6 na 7...mwishoni mwa miaka ya 90...
Niliuza miwa. Nikitoka shuleni natoka nduki nakimbia kwelikweli, nanunua miwa kwa bibi jirani, narudi barabarani kuuzia wale wale wanafunzi niliowaacha nyuma wakitembea kama mabibi harusi.
Ni kijijini, hakuna zile habari za kuchonga na kuweka kwenye karatasi kama mjini. Ni hapo barabarani nakukatia pingili zako unasepa.

Baadae nikaja kuuza popcorn na karanga. Nikajimudu mambo mengi.

Kwa hao wanao....

Wape mtaji wauze ubuyu, karanga, pipi, popcorn na biscuits. Target market ni watoto wenzao mtaani.
 
Mimi Nilikuwa form two nilitengeza bustani ya mboga mboga hasa broccoli, cauliflower, lettuce na Chinese, Chinese walinunua majirani na hizo zingine nilikwenda kuuza kwa wahindi kwa kutumia baiskeli.
 
Mjengee 21'Century Passion

Usiwaambie wala kuwafahamisha nini unataka wawe.

Wananunulie Computers alafu wape mafunzo ya Skills mfano Graphics Design, Coding nk level ya Basic unaweza ukawapa mwalimu...Baada ya hapo wawekee machapisho na mafunzo kwenye Storage zao za Computer waendelee kujifunza wenyewe the way muda utavyozidi kwenda UBONGO utajenga Passion ya kupenda Computer watakuwa na interest ya kujifunza zaidi na zaidi ukiona kitu hiko waongezee TASKs zaidi na zaidi wakifikia kuwa level ya TECH MANIA wa-direct kwenye Skills nyengine kama Business, Marketing.

Goal ya kwanza iwe Passion, wakiendelea hivyo nahakika katika 20's yao watakuwa wamefika level za kuongea Deal za Billion mezani na Investors.
 
Still hapo umemchagulia...
 
Wangu mm wakifikia umri unafaa nitatafuta fund simu (nawafahamu wengi tu) nawakabidhi wakachezee gun na solder za kutosha , kutoka hapo wajifunze coding, atayependa carpentry ama welding
Planning is easy!!! Tuombe uzima
 
Watoto wako wana akili mimi wa kike nilimuuliza akasema eti awe anapika wali akauze shuleni sasa nawaza sijui sababu muda mwingi yupo jikoni au anapenda tu kula

Nafikiri yupo interested na mambo ya migahawa.
Itakuwa anapenda sana kupika ama huko shuleni kuna mtu anawauzia chakula na yupo karibu nae au anavutiwa na anavofanya.

Mkuu kila mtu anapenda kula
 
Bado wadogo kwa karne hii peleka shamba hao wakajifunze hata majina ya mazao na kushangaashangaaa
Ila mimi nikiwa na miaka hiyo tulikuwa tunashindana kugonga kokoto Halafu tunauza kwa ndoo ndogo
Mawe tulikuwa tunapata tu karibu na ilikuwa kama mchezo tunashindana
 
Watoto wako wana akili mimi wa kike nilimuuliza akasema eti awe anapika wali akauze shuleni sasa nawaza sijui sababu muda mwingi yupo jikoni au anapenda tu kula
Huyu atakuwa shishi food. Labda atashika tenda za kulisha jeshi mbelen. Mfanye ajue watu wangap wanakula kias gani cha nini kwa muda flan
 
Likizo inayokuja nataka kufanya kitu tofauti kwa watoto wangu.

Pamoja na kujisomea nyumbani ila nitaweka nguvu kuwafundisha biashara kwa vitendo.

Nataka niwafungulie biashara ya kufanya kila mtu na yake na wapo wawili.

Nitawakopesha mtaji na nitawadai wakimaliza likizo faida yao itanunulia mahitaji yao wanayotaka ya ziada.

Nisaidieni ni biashara ipi wanaweza fanya kwa mazingira ya nyumbani?

Note: mimi sio mfanyabiashara, nimepata hii idea ili kuziba gap nililokuwa nalo kwenye malezi yangu.
'Note: mimi sio mfanyabiashara, nimepata hii idea ili kuziba gap nililokuwa nalo kwenye malezi yangu.'

Hii ina maana gani?
 
'Note: mimi sio mfanyabiashara, nimepata hii idea ili kuziba gap nililokuwa nalo kwenye malezi yangu.'

Hii ina maana gani?
Hataki wanae wapitie yale aliyoyapitia,anawalea katika misingi ambayo ameamua kuwafanyia njia ya kile alikikosa kukipata kwenye malezi yake
 
Watoto wako wana akili mimi wa kike nilimuuliza akasema eti awe anapika wali akauze shuleni sasa nawaza sijui sababu muda mwingi yupo jikoni au anapenda tu kula
hata mtoto wako ana akili sana,sema wewe hujajua namna gani ya kukiongezea thamani kitu anachokipenda(kupika),
hakuna biashara ya uhakika kama chakula
natamani niwe coach wa huyo mtoto
ili niweze kutimiza ndoto zake za upishi bora.
 
Taja kwanza umri wao

Mm wakwangu mapacha me na ke wapo darasa la 5 walipokuwa darasa la 4 niliwauliza kila mmoja anataka kufanya nn

Wakike akaniambaia anataka kufuga kuku nikamnunulia kuku 20 Koo 15 jogoo 5 leo anakuku 90+ wakienyeji

Wakiume alitaka kifuga mbuzi na sungura nikamnunulia majike 5 na dume 1 leo hii ana mbuzi 10 jumla sungura sikumnunulia

Wote wanatokea nyumban
Respect mkuu, mfano anataka kununua viatu vya shule, begi na vitu kama hivyo unamtafutia mteja anauza mwenyewe mbuzi mmoja, unaenda nae dukani anachagua vitu vyake kulingana na fedha aliyonayo na change anakeep kwenye pig-bank yake…. Akikua huyo hatataka ajira maisha yake yote… tayari anafoundation. Darasa safi sana.
 
hata mtoto wako ana akili sana,sema wewe hujajua namna gani ya kukiongezea thamani kitu anachokipenda(kupika),
hakuna biashara ya uhakika kama chakula
natamani niwe coach wa huyo mtoto
ili niweze kutimiza ndoto zake za upishi bora.
Mpishi anapiga hela kuanzia level za mama ntilie mpaka wa 5stars hotel….jamaa hajasoma gape tu vizuri….. wamiliki wa bar/ pub nyingi wanathamini jiko kuliko counter ya vinywaji.
 
Watoto wako wana akili mimi wa kike nilimuuliza akasema eti awe anapika wali akauze shuleni sasa nawaza sijui sababu muda mwingi yupo jikoni au anapenda tu kula
Mkuu nimecheka kwanza , lakini si kwamba huyo wa kwako kakosea au anapenda kula sana ila huenda ana kipaji hicho na moyo wake unatamani sana kazi hiyo, hivyo siku ikifika mfungulie tu ki mgahawa
 
Back
Top Bottom