Ni biashara gani inafaa kufanywa na mtoto mdogo?

sonofobia

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
325
2,292
Likizo inayokuja nataka kufanya kitu tofauti kwa watoto wangu.

Pamoja na kujisomea nyumbani ila nitaweka nguvu kuwafundisha biashara kwa vitendo.

Nataka niwafungulie biashara ya kufanya kila mtu na yake na wapo wawili.

Nitawakopesha mtaji na nitawadai wakimaliza likizo faida yao itanunulia mahitaji yao wanayotaka ya ziada.

Nisaidieni ni biashara ipi wanaweza fanya kwa mazingira ya nyumbani?

Note: mimi sio mfanyabiashara, nimepata hii idea ili kuziba gap nililokuwa nalo kwenye malezi yangu.
 
Haitasaidia nadhani idea yako, idea nzuri ni ile ya wahindi pale kariakoo, kama una biashara nenda nae kwenye hizo biashara zako na mpangie majukumu, kama ni duka ahudumie kabisa wateja moja kwa moja! Kama unachukua mizigo chanzo fulani mwagize afatilie manunuzi na akuletee record ya nini kanunua kwa kiasi gani na garama.gani.
 
Taja kwanza umri wao

Mm wakwangu mapacha me na ke wapo darasa la 5 walipokuwa darasa la 4 niliwauliza kila mmoja anataka kufanya nn

Wakike akaniambaia anataka kufuga kuku nikamnunulia kuku 20 Koo 15 jogoo 5 leo anakuku 90+ wakienyeji

Wakiume alitaka kifuga mbuzi na sungura nikamnunulia majike 5 na dume 1 leo hii ana mbuzi 10 jumla sungura sikumnunulia

Wote wanatokea nyumban
 
Huwa naona watoto huku wakati wa likizo huwa wanakuja kufanya kazi kama work experience ila ni kuanzia miaka 13 na kuendelea

Kama ni wadogo zaidi ya hapo sukushauri uwatume nje wakauze vitu hata kama ni magazeti

Ila kama una miradi yako na wapo chini ya umri huo inafaa uwashirikishe ukiwa nao na kuwafunza kwa vitendo
 
Haitasaidia nadhani idea yako, idea nzuri ni ile ya wahindi pale kariakoo, kama una biashara nenda nae kwenye hizo biashara zako na mpangie majukumu, kama ni duka ahudumie kabisa wateja moja kwa moja! Kama unachukua mizigo chanzo fulani mwagize afatilie manunuzi na akuletee record ya nini kanunua kwa kiasi gani na garama.gani.
naunga mkono hili wazo kwa 100%
 
Lengo ni kuwafunza maisha tofauti na ajira ya kusubiri mshahara au posho.

Nataka waanze kupata experience ya biashara wakiwa wadogo. Wakitengeneza hasara ni sehemu ya kujifunza siangalii sana watazalisha nini.
Mawazo yako yako vizr

Nilisema hivyo nikijua wewe ni mfanya biashara kumbe mwajiriwa sasa biashara sio kuwa utauza Leo Leo ndio maana nikashauri uwapeleke huko ili wajifunze kuwajibika
 
Kam
Likizo inayokuja nataka kufanya kitu tofauti kwa watoto wangu.

Pamoja na kujisomea nyumbani ila nitaweka nguvu kuwafundisha biashara kwa vitendo.

Nataka niwafungulie biashara ya kufanya kila mtu na yake na wapo wawili.

Nitawakopesha mtaji na nitawadai wakimaliza likizo faida yao itanunulia mahitaji yao wanayotaka ya ziada.

Nisaidieni ni biashara ipi wanaweza fanya kwa mazingira ya nyumbani??

Note: mimi sio mfanyabiashara, nimepata hii idea ili kuziba gap nililokuwa nalo kwenye malezi yangu.wa
Wanunulie baiskeli wakodishe watoto wenzao, nunua game wachezeshe watoto wenzao home , ila angalia wakizoea pesa shule wansweza kuona shida...
 
Taja kwanza umri wao

Mm wakwangu mapacha me na ke wapo darasa la 5 walipokuwa darasa la 4 niliwauliza kila mmoja anataka kufanya nn

Wakike akaniambaia anataka kufuga kuku nikamnunulia kuku 20 Koo 15 jogoo 5 leo anakuku 90+ wakienyeji

Wakiume alitaka kifuga mbuzi na sungura nikamnunulia majike 5 na dume 1 leo hii ana mbuzi 10 jumla sungura sikumnunulia

Wote wanatokea nyumban

Watoto wako wana akili mimi wa kike nilimuuliza akasema eti awe anapika wali akauze shuleni sasa nawaza sijui sababu muda mwingi yupo jikoni au anapenda tu kula
 
Haitasaidia nadhani idea yako, idea nzuri ni ile ya wahindi pale kariakoo, kama una biashara nenda nae kwenye hizo biashara zako na mpangie majukumu, kama ni duka ahudumie kabisa wateja moja kwa moja! Kama unachukua mizigo chanzo fulani mwagize afatilie manunuzi na akuletee record ya nini kanunua kwa kiasi gani na garama.gani.
Safi good idea
 
Bado wapo primary school, mmoja miaka 8 mwingine 10. Sawa nimeichukua hii idea.
Dunia ya ajabu kwelikweli,we kama mzazi una jukumu la kujua vipaji au talanta za watoto wako gundua vipaji vyao kwanza walizozaliwa nazo ndio uombe ushauri huku
 
Likizo inayokuja nataka kufanya kitu tofauti kwa watoto wangu.

Pamoja na kujisomea nyumbani ila nitaweka nguvu kuwafundisha biashara kwa vitendo.

Nataka niwafungulie biashara ya kufanya kila mtu na yake na wapo wawili.

Nitawakopesha mtaji na nitawadai wakimaliza likizo faida yao itanunulia mahitaji yao wanayotaka ya ziada.

Nisaidieni ni biashara ipi wanaweza fanya kwa mazingira ya nyumbani??

Note: mimi sio mfanyabiashara, nimepata hii idea ili kuziba gap nililokuwa nalo kwenye malezi yangu.
Kama upo dar jarbu kucheki na hii account ya twitter itakupa taarfa zaidi, kuna binti anakusanya watoto wadogo pamoja na walimu mbalimbali meaning wafanyabishara na corporates personnel nakuwapa watoto elmu zakibiashara nakuwasaidia kuanzisha mradi wao wa kwanza wakibiashara

Screenshot_20211121-134755.jpeg
 
Bado wapo primary school, mmoja miaka 8 mwingine 10. Sawa nimeichukua hii idea.
Wafundishe misingi ya kusevu pesa (Saving) kwa matumizi ya baadae hasa emergence.

itawasaidia sana kisaikolojia sio kila hela kukimbilia kununua viwalo na kula hovyo

kuhusu biashara, hao watoto bado ni wadogo sana. Acha wamalize la saba hata wajue kurudisha chenchi
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom