Ni benki gani inatoa mkopo kwa wafanyabiashara wadogo pasipo udhamini wa nyumba?

Apr 3, 2016
5
2
Habarini wana forum,

Mimi ni mfanyabiashara. Nipo kwenye kundi la wafanyabiashara wadogo kwani nina duka linauza vifaa vya umeme, hasa umeme wa solar. Ninauza battery ya solar, solar panels, lantern, taa, nyaya, Radio na TV zinazotumia umeme wa solar, pasi za solar, na vifaa vingine vya umeme.

Duka lina vibali vyote yaani TIN, Leseni ya biashara na mkataba wa flame. Duka lina mtaji wa kama million 10. Ninahitaji kukuza biashara yangu kwa kuongeza baadhi ya vitu dukani kwangu. Naombeni kuuliza ni Bank gani hapa Tanzania inatoa mkopo kwa mfanyabiashara mdogo kama mimi ambaye hamiliki nyumba?

Ninahitaji sana mkopo ila kila bank ninayoenda naambiwa niwe na mali isiyohamishika kama nyumba au shamba. Tafadhari naombeni mnisaidie kujua ni bank gani inaweza kunipa mkopo kwa masharti mengine pasipo hilo la nyumba? Sina/similiki nyumba nimepanga.

Ninaishi Mbeya mjini nipo soko la SIDO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asiye na nyumba haaminiki!
Tafuta kiwanja nje ya mji hata cha laki tatu, kule njia ya kwenda Tukuyu. Jenga nyumba ya matofali ya udongo, jengea na tope. Then nunua mifuko miwili mitatu uipige lipu nyumba ipendeze kisha nenda 'kawauzie benki'...
Otherwise inabidi uchukue mkopo mdogo sana yani kama mkopo wa chini ya milioni mbili ndio unaweza kukopesheka hivi hivi.
 
benki ambayo unaweza kukopa 1milioni bila ofa ya kiwanja ni finka pekee.ila ikizidi milioni 1 unatakiwa uwe na ofa
 
Asiye na nyumba haaminiki!
Tafuta kiwanja nje ya mji hata cha laki tatu, kule njia ya kwenda Tukuyu. Jenga nyumba ya matofali ya udongo, jengea na tope. Then nunua mifuko miwili mitatu uipige lipu nyumba ipendeze kisha nenda 'kawauzie benki'...
Otherwise inabidi uchukue mkopo mdogo sana yani kama mkopo wa chini ya milioni mbili ndio unaweza kukopesheka hivi hivi.
Hahaa daah hapo bank itakuwa wamepigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa benki zetu bila dhamana haiwezekani mkuu kuna kipindi nmb walikuwa wanatoa kwa dhamana ya vitu vya ndan lakin siku hiz wameacha
 
Asiye na nyumba haaminiki!
Tafuta kiwanja nje ya mji hata cha laki tatu, kule njia ya kwenda Tukuyu. Jenga nyumba ya matofali ya udongo, jengea na tope. Then nunua mifuko miwili mitatu uipige lipu nyumba ipendeze kisha nenda 'kawauzie benki'...
Otherwise inabidi uchukue mkopo mdogo sana yani kama mkopo wa chini ya milioni mbili ndio unaweza kukopesheka hivi hivi.
Ushauri safi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom