Ni bahati mbaya? Ni Kukosa umakini? Ni kutokujua hesabu? Ni ukilaza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni bahati mbaya? Ni Kukosa umakini? Ni kutokujua hesabu? Ni ukilaza?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by The Prophet, May 10, 2011.

 1. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 2. dazenp

  dazenp Senior Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ni ukilaza....................full familia nzima nikjumlisha na maneno ya Rizone ya kutaka kuwapeleka mahakamani viongozi wa vyama vya siasa ............wamejaaa ujuha:A S cry:
   
 3. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  VYOTE KWA PAMOJA+UFISADI
  Mkulo anatuongopea?
  Mkulo: Serikali haijafilisika

  na Mwandishi wetu, Dodoma
  Source: Hapa

  WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amesema serikali haijafilisika na haijawahi kukopa fedha kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wake.

  Mkulo alisema hayo mjini Dodoma jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akijibu tuhuma za Naibu Katibu Mkuu wa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto, aliyesema kuwa serikali imefilisika kiasi cha kukopa kwenye mabenki ya ndani kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wake na wabunge.

  "Napenda kutumia fursa hii kukanusha vikali madai hayo kuwa ni uongo mtupu na upotishaji unaofanywa kwa maksudi kwa lengo la kujitafutia umaarufu wa kisiasa… napenda kuwaeleza wananchi kuwa taarifa hizo si sahihi. Serikali inalipa watumishi wake mishahara kwa kutumia mapato yake ya ndani pia ina uwezo wa kugharamia shughuli zake nyingine ikiwemo kuendesha Bunge," alisema Mkulo.

  Alisema mishahara ya watumishi wa serikali katika kipindi cha kuanzia Desemba hadi Aprili mwaka huu, makusanyo na mapato ya ndani ni malipo ya mishahara ya watumishi wa serikali.

  Akifafanua hilo Mkulo alieleza kwamba Desemba mwaka jana serikali ilikusanya sh bilioni 594 ambapo kiasi cha sh bilioni 243.80 kilitumika kulipa mishahara na ziada ya sh bilioni 350.20 ilipatikana wakati Januari mwaka huu makusanyo yalikuwa sh bilioni 433.50 na mishahara iliyolipwa ni sh bilioni 240 huku ziada ya sh bilioni 193 ikiendelea kuwepo.

  Mkulo aliendelea kufafanua kuwa Februari mwaka huu walikusanya sh bilioni 430 na ikalipa mishahara sh bilioni 266 na ikabaki na ziada ya sh bilioni 163.70 huku Machi serikali ikikusanya sh bilioni 567 na ikalipa mishahara sh bilioni 249 na kubaki na ziada ya sh bil. 317 wakati Aprili walikusanya sh bilioni 432 na ikalipa mishahara sh bilioni 246.70 na kubaki na ziada ya sh bilioni 185.40.

  "Uchambuzi huu unaonyesha dhahiri kuwa serikali inayo mapato ya kutosha ambayo yanakidhi kulipa mishahara ya watumishi wa serikali kwa ukamilifu na tunayo ziada ya kutosha kugharamia shughuli nyingine za serikali… kwa kawaida serikali inatumia fedha taslimu kulipa gharama zake.

  "…Kwa hiyo mapato ya Desemba yanalipa mishahara na matumizi ya Januari. Mapato ya Januari yanalipa matumizi ya Februari na kadhalika, kwa utaratibu huu hakuna hata mwezi mmoja ambao wafanyakazi wa serikali wamekosa mshahara.

  "Wanaotoa uongo huo wanatafuta umaarufu wa kisiasa, wamekosa uzalendo kwa taifa lao," alisisitiza Mkulo na kuongeza kwamba posho mbalimbali za wabunge zimelipwa kwa wakati licha ya ongezeko la wawakilishi hao na kutaja stahili zao kuwa ni kwa ajili ya shughuli za kamati za Bunge, posho majimboni, mishahara na mafuta ya kila mwezi.

  Aliongeza kuwa mwezi uliopita mishahara ya wabunge ilitolewa Aprili 22 mwaka huu na fedha kwa ajili ya posho mbalimbali nazo zimeshatolewa kwenye ofisi za Bunge. Hivyo alisisitiza na kuelewesha umma kuwa serikali haijashindwa kulipa mishahara ya wabunge na posho zao tofauti na taarifa zilizotolewa na Zitto akidai wabunge hawajalipwa.

  Akizungumzia mikopo ya serikali na malengo yake, Mkulo alisema pamoja na kutumia mapato ya ndani kugharamia shughuli zake, hukopa kutoka vyanzo mbalimbali ili kugharamia shughuli za maendeleo. Mikopo hiyo inahusisha ile yenye masharti nafuu na kibiashara.

  "Kwa mfano katika mwaka wa fedha wa 2010/2011 serikali ilipanga kukopa kiasi cha dola za Marekani milioni 525 ambapo kati hizo dola za Marekani 250 zitagharamia miuondombinu wakati kiasi cha dola za Marekani milioni 175 zitatumika kununua mitambo ya kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 kwa ajili ya Dar es Salaam na megawati 60 kwa ajili ya Mwanza," alisema.

  Mkulo alisema ameamua kutoa ufafanuzi huo ili kuonyesha kwa kifupi kuwa serikali ina uwezo wa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake, mishahara na gharama zote za kuendesha Bunge kutokana na mapato yake ya ndani. Sio kweli na ni upotoshaji wa makusudi wenye malengo ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

  Alipoulizwa hatua gani atachukuliwa Zitto kutokana na kutoa taarifa za uongo kwa Watanzania, alijibu kuwa yeye alichofanya ni kueleza kile ambacho ndicho sahihi kwa serikali na kwamba wanaoweza kumchukulia hatua Zitto kwa kusema uongo ni Bunge lenyewe. Kutokana na ufafanuzi huo, Mkulo alisema kuwa kikubwa kinachotakiwa hata kama ni mtu wa chama chochote cha kisiasa ama kiongozi kuchuja mambo na kuangalia athari zake kwa kina na si kukurupuka kwa kutafuta umaarufu ambao hauna tija kwa taifa zaidi ya kusababisha matatizo.  My Take:

  1. Mkulo anataka kutuaminisha kwamba kazi ya mapato ya serikali ni kulipa mishahara basi. Sasa sijui hata hivyo vikao vya bajeti wanakaa kwa ajili ya nini.

  2. Kwa takwimu za mkulo ina maana mpaka sasa serikali ina ziada ya shillingi bilioni elfu moja mia mbili na nane au Shillingi Trilioni 1 na bilioni mbili

  3. Inakuwaje sasa serikali yenye ziada ya mihela yote hiyo halafu inaenda kukopa tena?

  4. Hivi huu si uwendawazimu? Februari mwaka huu walikusanya sh bilioni 430 na ikalipa mishahara sh bilioni 266 na ikabaki na ziada ya sh bilioni 163.70 . Mishahara tu ni 62%, hiyo serikali iakuwaje na hela?

  5. Kwa mapato hayo na matumizi hayo kwa mishahara tu, si ni indicator ya wazi kabisa kwamba tuna liserikali likuubwa tena lisilo na manufaa yeyote.

  6. Hiyo trend ya matumizi hainekani kabisa kwamba jamaa wanajali kubana matumizi wao ni kutumia tu!

  7. Kama hizi data nni za kweli, basi Mkulo, JK and the government are failing us miserably.

  8. Bunge linaingiajae hapa kumchukulia hatua Zitto kama amesema uwongo?
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kha! Hii ya Vodacom nilikuwa sijaiona bado.
  Hili tatizo kwa hii familia ni HEREDITARY.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Dr. Kikwete anatabasamu kweli kweli mshiko huo
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Dah naona Lukuvi yupo Dr. Kikwete wanauza sura kwa cheque feki
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Kama kawa huu utaratibu huu inabidi upigwe marufuku.
   
 8. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hayo tumeyaona hadharani kwa msaada wa camera kwenye mikataba ambayo wanasahini nafikiri huko hali mbaya zaidi wanasahini vitu bila kusoma.hapa ndipo inapoanzia mikataba feki!!!!
   
 9. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Na kama maandisi makubwa namna hiyo, machache na yapo kwenye karatasi moja wanashindwa kuyaona, watawezeje kuona maandishi ambayo yanaandikwa kwenye karatasi ya A4 ambayo kwa wengine inabidi kutumia msaada wa miwani ili kusoma ambayo jumla yake ni mamia ya makurasa.
   
 10. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jamani hata mikataba kati ya Serikali yetu na watu wengine huwa ni ya namna hiyo.
   
 11. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Jamani tuache kuwacheka,hili swala linahitaji maombi.
   
 12. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani Nimecheka sana na nikaurumia Viongozi wangu, yani wanacheka kwa nguvu zote kwa vitu wasivyo visoma, sasa wasaidizi wako wapi waweze rekebisha izo check kabla ya kupigwa picha?
   
 13. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  kuna siku ntaandika cheki alaf kwa maneno niandike 'president is dead' alaf nimuite mkulu nimkabidhi mbele ya media. Bila kusoma mkulu anaweza akaja kupiga nayo picha. Kweli kuna vioja duniani.
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  tatizo la kuandikiwa jamani,nasikia hata kwenye hotuba akishaanza kusoma mbele ya media huwa anagundua makosa na kushtuka alaf anapotezea kiaina. Mfano: mlipuko wa mabomu g.la mbota wa tar17 febr. ...alaf shit..mbona ilikuwa tar16 sa1jion? Kisha anapotezea, kaja kwenye malipo ya mishahara...tukiwalipa wafanyakazi ambao wako lak3.5 itabidi tupate nusu ya bajeti sawa na trilion6.5 alaf anagundua shit ,watu lak3.5 mara mshahara kima cha wastan lak3.5 haifiki hata trilion2,anaona dah isiwe noma next month sitohi hotuba.
   
 15. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jamani hivi kweli hizi sio picha za kutengenezwa hizi? Siamini kuwa hicho kitu ni kweli zaidi ya kutaka kuchafuana hapa.Hata mtoto wa shule ya msingi lazima atajua tu kuwa hizo cheki zimekosewa.
   
 16. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  shame on all the people responsible and this shows lack of seriousness in all the levels in the country from leaders, workers, and investor. sijui kwa nini tutegemee kuendelea kama watu hawako serious kiasi hichi, its very wrong kufikiri ni aibu kwa president lakini hata muandikaji ni mpuuzi na bosi wake, knowingly alitakiwa kuipresent walitakiwa wawe wamecheki vizuri, tusikubali aibu kama hizi tena.:A S cry:
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Kuna vilaza wengi nchi hii, kuanzia juu hadi chini! na hii ni familia moja!
   
 18. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  duuuuh ama kweeeeli kazi iiiipo..................mkulu haji hata invalid cheque iko vp,kalaghabhao
   
 19. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  sio photoshop hii jamani!!!???, hii inawezekana kweli? au wanmfanyia kusidi wajue kama anazisomaga kabla ya kupiga pic nazo!!!!
   
Loading...