mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Kwanza Kuna neno Bahati mbaya, ila hakuna kitendo cha Bahati mbaya ulimwenguni kote. Kila jambo na Kila tukio linasababu au Chanzo.
Tujikite kwenye Chanzo ni nini na sio ilikuwa Bahati mbaya. Kwa kukumbatia kauli hizi za kizembe, excuses siku moja tutajikuta tanzania ni taifa la walemavu, wagonjwa na makaburi mengi ya raia waliokufa kizembe...
Ni Mipango ya Mungu. Hii kauli nayo ni kauli inayohamasisha uzembe na kuhafifisha Nia ya kutatua tatizo. Binafsi siamini Mungu alipanga watoto wetu wafariki wakiwa bado wabichi na tunawahitaji zaidi, siamini Mungu alipanga kuzamisha MV Bukoba, au Kurudisha treni riverse na kuua mamia dodoma.
Ninachoamini Mungu ANAJUA sio ALIPANGA kwa sababu Mungu anajua yote (omnipotent).
Inafaida sana Kuishia Mungu anajua, maana tutajiuliza kwa nini itokee, utagundua sababu nyingi ya Ajali na Matatizo ni matokeo ya maamuzi mabovu ya mtu mmoja au wachache. Ni afya sana kutatua tatizo kuliko kumsingizia Mungu alipanga. Kauli hii inahafifisha moyo wa watu kuchukua Taadhari.
Mungu anajua ila hakupanga, wakati mwingine anaacha tupate matokeo ya tunachokichagua ili akili zichangamke na kuangulia suluhisho kwa akili alizotupa. Tusitegemee Mungu kukanyaga break pale ambapo dereva anapaswa kukanyaga na akili ya kufanya hivyo kampa.
Tukiendelea kutumia maneno haya mawili katika kutiana faraja, tutaendelea kuzika Kila siku mtanzania wa Kila Rika, kabila na rangi.
Hakuna kitu cha Bahati Mbaya ulimwenguni kama kipo tusaidiane.....
wenzetu wa magharibi wangekuwa hivyo hadi leo wangekuwa wanakufa Kila siku kama sisi kwa matukio ya kuepukika...