Ni akina nani waliohukumiwa kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Mbowe kama alivyosema Rais Samia?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,628
218,059
Namba hazijawahi kudanganya, kwa mujibu hati ya mashitaka ,Mbowe ameshitakiwa pamoja na wenzake watatu, kwa mashitaka kadhaa huku Mbowe akikabiliwa na mashtaka mawili, hawa wote wako rumande na kesi yao inaendelea.

Nukuu
Rais Samia: Mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa kwasababu navyojua Mbowe alifunguliwa Kesi mwezi wa Tisa mwaka jana (2020), kwa hiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi. Nadhani wenziwe kesi zao zimesikilizwa na wengine wameshapewa sentence zao wanatumikia. Yeye (Mbowe) upelelezi ulikuwa haujeisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea so amekwenda amefanya tumeingia kwenye uchaguzi, amemaliza uchaguzi nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao, wamemuhitaji waendelee na kazi yao.

Sasa hao wengine ambao Mtukufu Rais Samia anadai walikwishahukumiwa ni akina nani na wako wangapi na wako gereza gani?
 
Hapa kuna siri kubwa , nani anaongoza nchi ambaye anapewa taarifa za kuwepo tishio la ugaidi, uhaini na kuondoa uhai wa viongozi.

Tulitegemea Mh. Rais Samia Suluhu Hassan awe na taarifa hizi nzito sana na nyeti za tuhuma za watanzania wanaotuhumiwa na vyombo vya usalama na intelijensia vya serikali ya Tanzania ya awamu ya 5 akiwa Makamu wa Rais na awamu ya 6 akiwa Rais, kuwa kuna genge hatari la kutaka kuvuruga amani, kubadilisha uongozi wa nchi ulio madarakani kwa nguvu yaani Uhaini.

9 AGOSTI 2021 DIRA YA DUNIA BBC SWAHILI



Source: BBC Swahili News
 
Tayari kabla ya mahojiano ya leo kuna viongozi walianza kujiuliza:

7 August 2021

PROF: LIPUMBA AMZUNGUMZIA MBOWE, KUHUSU SUALA LA UGAIDI.




Prof. Ibrahim Haruna Lipumba asema Haingii akilini gaidi na mhaini akapelekewa salamu za rambirambi tarehe 8 Julai 2021 na Rais ambaye ni amiri jeshi Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, halafu tarehe 23 Julai 2021 Freeman Mbowe akakamatwe kwa ugaidi wa mwaka 2020.

Maana rais kila siku hupewa taarifa za usalama za nchi nzima, iweje tarehe 8 Julai 2021 Freeman Mbowe apelekewe salamu za pole za rambirambi za msiba wa kaka yake. Ina maana rais alikuwa hana taarifa za ugaidi wa Freeman Mbowe mpaka tarehe 21 Julai 2021 siku ya kongamano la CHADEMA juu ya katiba ya nchi, anahoji Prof. Haruna Lipumba.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba anakwenda mbali na kuhoji kuwa haiwezekani vyombo vya ulinzi na usalama kutomfahamisha Rais juu ya mipango ya kuwakamata watuhumiwa wa mipango ya ugaidi wa kulipua sehemu mbalimbali, njama za kuua viongozi na kufanya uhaini za mtuhumiwa Freeman Mbowe kiasi rais anatuma pole kwa mtu mwenye kutuhumiwa kesi nzito ambaye yupo mbioni kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka ya kutisha sana ya ugaidi na uhaini.

Source: StarTV Habari
 
Respect is ALWAYS a TWO WAY TRAFFIC. Provocation!? Who is provocating who? Wewe babaako angekuwa yuko ndani kwa ushahidi FEKI ungeandika upuuzi kama huu!? Au mkuki ni kwa nguruwe!? 😳😳😳
Please, respect our Head of State...Huna adabu wewe!

Kumtusi Rais ni kutukana watanzania wote; inamaana sisi tuliopiga kura kumweka kama Makamu wa Rais ambaye ni Rais in waiting hatukua akili....

Kwanini mnapenda provocation?
 
Namba hazijawahi kudanganya , kwa mujibu hati ya mashitaka , Mh Mbowe ameshitakiwa pamoja na wenzake watatu , kwa mashitaka kadhaa , huku Mbowe akikabiliwa na mashtaka mawili , hawa wote wako rumande na kesi yao inaendelea .

Sasa hao wengine ambao Mtukufu Rais Samia anadai walikwisha hukumiwa ni akina nani na wako wangapi na wako gereza gani ?
Mkuu,

Mbona unajichanganya?

Si unapigania serikali TATU sio? Ni kitu gani na kitu ukijumlisha kinaleta TATU?

Wanaodai serikali MBILI iendelee wanatoa sababu ya kihesabu kwamba 1 jumlisha moja ni MBILI

Je Ngapi jumlisha ngapi upate TATU?

Tanganyika HURU=1

Zanzibar HURU=1

Tan-Zan......(Kimalizio ni kifupi cha jina la mtu binafsi na dini yake)

IA.......Iqbal+Ahmadiya

Tan-Zan-IA (Mmiliki halali wa jina la Tanzania ni MOHAMMED IQBAL DAR muumini wa dini ya AHMADIYA MUSLIM JAMAAT)

Nchi hii imepatikana kimaajabu, watu wake ni waajabu na matukio ya yanayoendelea kutokea ni ya adabu, mauzauza na giza tupu

Mwanzilishi wa jina hili ni mstaarabu wa kiwango cha juu sana vinginevyo angedaia haki yake mpaka kwenye mahakama za kimataifa ikiwemo kusudio la kumilikishwa nchi na kuabudiwa kama mwenye mali

Wananchi msigombane bure nchi hii siyo yenu ina mwenyewe kwahiyo unapojitwika jeuri kwamba lazima ni dai hili ama lile litekelezwe ni ajabu maana hata viongozi inawabidi kutii masharti na kiapo wanachokutana nacho ambacho wewe na mimi ambao hatujawahi kuingia kwenye tanuru la jumba la kiutawala wa nchi kushuhudia hivyo madai yoyote ukianzisha yatakuwa hewa na ukishupaza shingo utavunjika.
 
Najisikia vibaya Kama Mtanzania,majibu mepesi kwa hoja nzito!!!
Katibu_Mwenyezi_wa_CCM_Taifa_SHAKA__akimkumbatia_Gaidi..jpg
%22Haki_Huinua_Taifa,_Bali_dhambi_ni_aibu_kwa_watu_wote%22-_Mithali_14:34.jpg
Rais_Mstaafu_Kikwete_akiwa_na………..?_%0A%0AMalizia_kwenye_comments..jpg
Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram:_“Mwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana_na_Waziri...jpg
 
Please, respect our Head of State...Huna adabu wewe!

Kumtusi Rais ni kutukana watanzania wote; inamaana sisi tuliopiga kura kumweka kama Makamu wa Rais ambaye ni Rais in waiting hatukua akili....

Kwanini mnapenda provocation?

Kutokuwa na akili ni sifa ya mtu huyo...

Haiwezi kuwa kutokuwa na adabu kumpa sifa yake mtu wa namna hiyo...

Kama tulimchagua Rais mtu asiye na akili timamu, basi wote tuliomchagua Rais huyo, ni kweli tutakuwa hatuna akili, ukiwemo wewe maana ni wazi ulimpa kura mwaka jana 2020...!!

Kwanini tuukatae ukweli huu...???
 
Back
Top Bottom