Ni ajali kwa kwenda mbele, kama vile tuna wazimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ajali kwa kwenda mbele, kama vile tuna wazimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukwangule, Mar 3, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naam tairi la basi la AM COACH lilipasuka likasababisha watu 26 kufa pale kitangiri Nzega Tabora.
  Kisha kukatokea tatizo katika tairi ala kwenye ndege.
  leo asubuhi naambiwa kuna ajali nyingine ya basi majeruhi kibao huko huko Tabora eneo la Ziba wilayani Igunga.
  Tunashukuru tu kupasuka kwa tairi la ndege ya ATCL kulikoambatana mvua kulipita salama japo sikubaliani na maelezo ya ajali yaliyotolewa na hao wanaomiliki ndege hiyo aina ya boeing 737-200 moja ya ndege ambazo ziliachwa kutengenezwa na kampuni ya Boeing mwaka 1988.
  Duhh sijui unachanganya vipi mambo haya lakini ndio hivyo tena ng'ombe ya maskini. unavipanga wawili mmoja anakwenda chini bwaa na hatoki pale anavutwa na kuwekwa katika kaburi lake.
  Halafu una magari yanayoenda bila kukaguliwa miguu na madereva wanaopania kufika saa mbili kabla ya wakati na hali inabadilika mhh. swali linabaki palepale ni gavana, ni matairi manake suala la matairi lilishazungumzwa sana na sijui hilo la ndege mhh
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  kaka rekebisha ili kupate wingo mzuri wa ku -discuss. chanzo cha ajali ni mwendo kasi - dereva alishindwa kulimudu gari lake na kuacha njia ikasababisha kupasuka kwa tairi la mbele gari ikapinduka mara tatu. nilishasema mara nyingi hizi ajali zingine za kujitafutia wenyewe.

  - dereva baada ya ajali kakimbia anatafutwa - hawa madereva ndiyo chanzo cha ajali hizi.

  Nilisha drive toka DSM - Tabora - DSM - Km karibia 1500 - jamani niliyoyaona njiani ni hatari - jamaa wanakimbiza magari kufuru. overtake popote tu hawajali duh - Akikupigia hony kwenye mlima haoni mbele harafu wewe unamnyima site utajikuta kwenye mtaro.

  Sasa haya ndiyo matokeo yake - sijui tumlaumu nani

  a) Askari barabarani
  b) Dereva
  c) abilia
  d) Jamii kwa Ujumla
  e) au Tuseme ajali haina kinga kama tulivyozoa kusema kila siku.

  mimi nasema hawa madereva ndiyo chanzo .
   
 3. L

  Lukwangule Senior Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sishauri watu kuandika kwa hasira kama wakati mwingine ninavyoandika. Uko sahihi.Lakini hapa wote wako sambweni ila hivi kama sheria ni kali na gavana kichwani hamna si balaa hilo.Mimi hupenda speed dunia ya leo ni speed lakini wazimu ah ah haiwezikani na haitakiwi. Speed sawasawa. Gavana kichwani.
  Lakini nilitaka watu wajadili pia haya matairi yetu kama yapo sawasawa. Nilichanganya na ndege kwa sababu harakaharaka tunaambiwa kwere kwere kwere na haya ya ndege ni ufundi zaidi.
  haya nataka tuangalie haya matairi yanavyopasuka
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...