Ni ajabu rais Jakaya Kikwete alikuwa hajui madai halisi ya Madaktari, Jana ndiyo kaambiwa Rasmi

Hapo ndipo ninaposhangaa, Pinda alionana nao na wakazungumza naye na sasa Kikwete .Kuna lipi jipya wlilozungumza na Pinda hakumwambia bosi wake. Safari bado ni ndefu aisee
Mi simwelewagi huyu Pinda kwa kuwa anaongozwa zaidi na hisia. Lilipokuwa suala la Jairo alisema, "lau ningekuwa na Mamlaka ningeshaamua lakini namsubiri Rais atue South Africa nimpatie taarifa......" Lilipokuwa suala la kina Blandina akaamua, sielewi ni mimi mzito kuelewa au ni Pinda hajui mamlaka yake. Kwa Rais awamu hii ni Subjective na si taasisi kama tulivyozoea wakati wa Nyerere.
 
JK haijawahi kutokea duniani...vyombo vyote hivi na wasaidizi wote hao wamejazana ina maana alikuwa hapelekewi report au ndio zake kuwaruka wasaidizi aonekane yeye ni fresh wale ndio vilaza??sidhani hapa kuna namna katika utendaji kazi wake!!usanii mwingi kuliko ukweli

Huyo ndo manaSiasa! Akitaka kuramba matapishi yake anaanzia hapo!
 
Kwa mujibu wa Taarifa ya Madaktari iliyo tolewa leo, imedhihirisha kuwa rais hakuwa anajua madai halisi ya madaktari mpaka alipoambiwa jana baada ya kukutana na madaktari hao,

Nimejaribu kuirudia zaidi ya mara mia kuisoma taarifa hii bado nimeridhika kuwa mkuu wa nchi na amiri jeshi mku, hakujua madai ya mgomo unaokaribia miezi mitatu sasa, napata hofu kujua kama tatizo lipo wapi, je ni wasaidizi wake, au yeye nduye tatizo?

Jambo lapili na muhimu ni je madaktari shida ilikuwa nikukanyaga magogoni au? ukiangalia majibu ya raisi hapo chini hayana tofauti na ahadi za kampeni za mwaka 2005 na mwaka 2015!

Haki za watumishi hawa zimibwakwa na wao, hawana sababu tena ya kuleta mgomo nawashauri wafute dhana ya kukombolewa toka utumwani kwa kwenda kunywa juice magogoni na kukenuliwa meno.

Lakini bado napata hofu, najiuliza hivi hiki chama cha madaktari hakina anwani? hivi nikiprinti hiyo ripoti nakutaka kufika nayo ofisini kwao nitafikaje?









RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

... 1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)

Sijaiona ile sehemu inayobeba kichwa cha habari yako! Je kuna kipengele umekiruka?
 
Madaktari wengi walikuwa wanagoma bila madhumuni ika kuna wachache ambao ni viongozi wao akina Dr Ulimboka na Mkopi walikiuwa na agenda zao za siri. Wengine awikuwa wanafuata mkumbo tu kama ile minyama ya Serengeti inayoitwa nyumbu. Nyumbu mmoja akianza kukimbia kwenda mtoni unakuta na wengine wanafuata, basi utakuta wote wanaishia kufa mtoni.

Haswaa!
 
Ni kweli hakuna palipo andikwa! Lakini labda nikujuze tu jambo moja na muhimu kwako, unapo zama kimang'amuzi kutafakuri tafasiri tata, mang'amuzi huja yaliyo huru bila mawaa.

Pili makubaliano uliyoyaorodhesha hapo juu kati ya Pinda, Madaktari na JK, kwangu mimi si rasmi kwani hayapo katika tamko la madaktari wala tamko la serikali

Mponda yupo hayupo? Nkya yupo hayupo? baada ya kutoka Ikulu wametangaza kuwacha mgomo hawajatangaza?

Zingine zote pumba za kutafuta kuficha aibu. Umewashuka shu.
 
Madaktari waambieni mliowatuma Ikulu wawaambie ukweli walikumbana na nini huko hata wakasitisha mgomo haramu, maana taarifa yao haisemi chochote zaidi ya kuonesha ya kutangaza uadui kwa Mponda na Nkya.
 
Madaktari waambieni mliowatuma Ikulu wawaambie ukweli walikumbana na nini huko hata wakasitisha mgomo haramu, maana taarifa yao haisemi chochote zaidi ya kuonesha ya kutangaza uadui kwa Mponda na Nkya.

Ni kweli kabisa!
 
Mwanangu unauonea Kikwete. Hivi ulitegemea kilaza kama yeye ajue kinachoendelea wakati wapambe zake wanamlisha uongo naye anaupwakia kutokana na akili ndogo. Hana hata muda wa kufuatilia habari zaidi ya kuishi kama kivulana kilichobarehe jana. Mtu mzima hovyo. Kikwete amekosa busara, akili hata kujua kuwa ni kiongozi wa nchi anayepeswa angalau kujua kila kinachoendelea badala ya kungoja aletewe habari. Ni mvivu wa kusoma na kufikiri.
 
Madaktari wengi walikuwa wanagoma bila madhumuni ika kuna wachache ambao ni viongozi wao akina Dr Ulimboka na Mkopi walikiuwa na agenda zao za siri. Wengine awikuwa wanafuata mkumbo tu kama ile minyama ya Serengeti inayoitwa nyumbu. Nyumbu mmoja akianza kukimbia kwenda mtoni unakuta na wengine wanafuata, basi utakuta wote wanaishia kufa mtoni.

hahahaaa hahaaa you are so silly,nyumbu tena?umenichekesha acha mana nimepata ile taswira wanavokimbia
enogh for today
 
Kuna jipya lipi hapo? Silioni hata ukasema Rais alikuwa hajui kwani hakuna sehemu hao madaktari wamesema hivyo. Hizo ni speculations zako tu.


Mtoa hoja hajakosea kusema kama Topic inavyosema. Kwani ina maana Rais anajifanya kuwa alikuwa hajui na sasa ndio anaomba kuyashughulikia; Ina maana Waziri Mkuu alikuwa hajamfikishia au Waziri Mkuu alikuwa anataka kutekeleza yeye hadi leo Raisi aseme kuwa atayashughulikia.

Ni muda gani umepita toka kikao cha kwanza kati ya Madakitari na Waziri Mkuu? Kama kweli Serikali ilikuwa na nia ya kushughulikia si ingelikuwa tayari.

Au ndio kusema kuwa kauli ya Waziri Mkuu haina nguvu mbele ya Rais na kuwa Waziri Mkuu anayosema yote ni PUMBA TU?

TUNASHUKURU KUWA RAISI AMEINGILIA KATI MGOGORO HUU, NA KUKUBALI KUONGEA NA WAWAKILISHI WA MADAKITARI ILI KUPATA RULUHU. KWANI ALIKUWA ANATUTISHA KWA UMKIMYA WAKE NA KUMTUMIA WAIRI MKUU KUTOA MATAMKO YA SERIKALI AMBAYO HAYANA NGUVU KIUTENDAJI.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 


RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

... TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.
KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA...........
SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)


Sijaiona ile sehemu inayobeba kichwa cha habari yako! Je kuna kipengele umekiruka?


Je, kwa kauli hiyo ya Tamko, unaweza kusema kuwa Raisi alikuwa anajua kinachoendelea??

Au vinginevyo tuseme kuwa tamko lina utata.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mie naona madaktari ndio walikuwa hawajui wanataka nini, kutoka katika madai yao ya msingi kuishia kutaka waziri na naibu wajiuzulu. Shame on them all, ilibakia kidogo wananchi wajichukulie sheria mikononi.

Sidhani kama kuna ambaye alitegemea majibu tofauti kutoka kwa rais, vinginevyo mtake kutubuluza na sisi hapa hakuna hata dammy cheque rais aliwapatia zaidi ya politike tu!
 
Back
Top Bottom