Ni ajabu rais Jakaya Kikwete alikuwa hajui madai halisi ya Madaktari, Jana ndiyo kaambiwa Rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ajabu rais Jakaya Kikwete alikuwa hajui madai halisi ya Madaktari, Jana ndiyo kaambiwa Rasmi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Mar 10, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa Taarifa ya Madaktari iliyo tolewa leo, imedhihirisha kuwa rais hakuwa anajua madai halisi ya madaktari mpaka alipoambiwa jana baada ya kukutana na madaktari hao,

  Nimejaribu kuirudia zaidi ya mara mia kuisoma taarifa hii bado nimeridhika kuwa mkuu wa nchi na amiri jeshi mku, hakujua madai ya mgomo unaokaribia miezi mitatu sasa, napata hofu kujua kama tatizo lipo wapi, je ni wasaidizi wake, au yeye nduye tatizo?

  Jambo lapili na muhimu ni je madaktari shida ilikuwa nikukanyaga magogoni au? ukiangalia majibu ya raisi hapo chini hayana tofauti na ahadi za kampeni za mwaka 2005 na mwaka 2015!

  Haki za watumishi hawa zimibwakwa na wao, hawana sababu tena ya kuleta mgomo nawashauri wafute dhana ya kukombolewa toka utumwani kwa kwenda kunywa juice magogoni na kukenuliwa meno.

  Lakini bado napata hofu, najiuliza hivi hiki chama cha madaktari hakina anwani? hivi nikiprinti hiyo ripoti nakutaka kufika nayo ofisini kwao nitafikaje?

  RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI.

  UTANGULIZI
  Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

  ... 1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).

  2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

  3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

  4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

  5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

  TAMKO LETU:

  JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

  KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

  PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

  MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

  SOLIDARITY FOREVER.
  RAIS(MAT)
   
 2. A

  Amani charles g New Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono 100%
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kuna jipya lipi hapo? Silioni hata ukasema Rais alikuwa hajui kwani hakuna sehemu hao madaktari wamesema hivyo. Hizo ni speculations zako tu.

  Leo watoeni Dr. Mponda na Lucy, kesho mutasema munataka kuwapigia kura mawaziri watakaokuja hapo kwenu...... haya Miungu muliojiteua.
   
 4. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni usanii tu kwani pinda ni waziri mkuu wa japan au tanzania? Ni kawaida yake
  tumemzoea kudharau watanzania na kukimbilia mizozo ya nje
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ye ni rais wa mambo ya nje haya ya huku ndani hayamuhu
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Hakika kabisa ni usanii uliopitiliza
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,311
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  JK haijawahi kutokea duniani...vyombo vyote hivi na wasaidizi wote hao wamejazana ina maana alikuwa hapelekewi report au ndio zake kuwaruka wasaidizi aonekane yeye ni fresh wale ndio vilaza??sidhani hapa kuna namna katika utendaji kazi wake!!usanii mwingi kuliko ukweli
   
 8. M

  Makwarukwaru Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwani huyo JK amewaahidi nini na tofauti na Pinda? tatizo la Mponda na Nkya ni nini waweke wazi ili na sisi wagonjwa tujue.
   
 9. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hii style ya serikali kushughulikia matatizo/malalamiko baada ya walalamikaji kwenda kumwona mkuu ikulu sijui itatufikisha wapi? Maana inaonekana mambo hayaendi mpaka watu wakamwone jk mwenyewe utadhani serikali haina watendaji zaid ya rais.
   
 10. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Hapo ndipo ninaposhangaa, Pinda alionana nao na wakazungumza naye na sasa Kikwete .Kuna lipi jipya wlilozungumza na Pinda hakumwambia bosi wake. Safari bado ni ndefu aisee
   
 11. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Madaktari wengi walikuwa wanagoma bila madhumuni ika kuna wachache ambao ni viongozi wao akina Dr Ulimboka na Mkopi walikiuwa na agenda zao za siri. Wengine awikuwa wanafuata mkumbo tu kama ile minyama ya Serengeti inayoitwa nyumbu. Nyumbu mmoja akianza kukimbia kwenda mtoni unakuta na wengine wanafuata, basi utakuta wote wanaishia kufa mtoni.
   
 12. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hiyo inaitwa tia maji tia maji au funika kombe mwanaharamu apite, wameliwa hao Ma-dr. ndio imetoka. Waende wakajipange tena, bingwa wa uongo amesha wadanganya
   
 13. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Usikute wasaidizi wake walikuwa wanammislead!
  Ila upande mwingine usikute ilikuwa kuwapiga sound madr kuwa hajui!
   
 15. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kama Rais hajui kila kitu kinachoendelea, anajua nini sasa? Dowans pia alisema haijui
   
 16. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hawa madaktari hawakuwa serious, utoto ukiwatawalAa sijui waktakua lini
   
 17. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #17
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Kila kinachotokea na kitakachotokea keshokutwa rais anajua, kinachotofautiana ni maamuzi tu
   
 18. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  UNAJUA MAT NI WEHU SAMAHANI NASEMA HIVI KWA KUMAANISHA
  A)WAKATI WANAENDA KWA RAIS AWAKUAMBIWA NA PINDA NMADAI YAO YANASHUGULIKIWA
  B)WALIPOKUWA WAKIENDA IKULU AWAKUJUA AWANA IMANI NA WAZIRI WALA NAIBU WAZIRI WA AFYA
  C)AWAKUJUA DR NKYA MPAKA WANAFIKIA STAGE ILE AKUITAJIKA KUWEPO KAMA MEMBER WA MAT
  D)AWAJUI DK NKYA AMA MPONDA WAKIUMWA AWAITAJI HUDUMA ZAO WANAKIMBILIA AGHAKAN KUELEKEA APPOLO-INDIA
  E)NAHISI KUNA MAMBOMNATAKIWA MUWE KITU KIMOJA NAKUMBUKA MH PINDA ALIWAONA KABLA YA KWENDA IKULU NA MAJIBU ALIOWAAMBIA AKUNA TOFAUTI NA RAIS ALICHOWAAMBIA JAMANI ..SASA SWALI LANGU WANAMWAMINI RAIS KIASI GANI WAKAOGOPA KUNYWA JUICE WAAMINI ATAWAFANYIA MALALAMIKO YAO
  F)KAMA SI MMOJA WAO KUWA SHEMEJI YANGU NINGEWAITA WEHU KWA ANINI???

  1a)WAKATI WANAANZA MGOMO AWAKUJUA RAIS WA NCHI ALIKUWA TANZANIA NA ANAWASNIFU KUWAANGALIA KWENYE RUNINGA KUANGALIA MAJIBU ALIYOMPA PINDA AYANELEKEAJE

  2A)AWAKUJIULIZA WAKATI WANAGOMA NA MAITI ZINATAMBAA PALE MUHIMBILI N A KWINGINEKO NA KUFIKIA MMOJA WA WANA JF KUPOTEZA SHANGAZI WAKE AWAKUJUA RAIS KIKWETE ALIKUWA AKIJUA KINACHOENDELEA JAMANI

  3A)IWEJE LEO HII WAGEUZWE KAMA MISUKULE YA KIKWETE WAKATI WATU WAKIFA HOSPITALINI TANZANIA NZIMA RAIS ALIKUWA AKIIANGALIA NA KUKAA KIMYA

  4A)KAMA WANAHISI RAISI ANA IMANI KWA NINI WASIRUDI KWANZA KWA WATANZANIA KUOMBA RADHI KWA KUFANYA MGOMO NA WATANZANIA KADHAA AKUPOTEZA MAISHA KWA UJINGA WA KUGOMA

  5A_KAMA WALIJUA KUNA SOLN NA SOLN NI KUMWONA RAISI KIKWETE KWA NINI AWAKUFANYA HIVYO MUDA ULE NA KURUHUSU WATU WANAKUFA OVYO MASHEMEJI ZANGU..BINAFSI NILIKUWA NYUMA YENU LAKINI KUTOKANA NA HILI NAJIULIZA KUMBE SOLN ILIKUWEPO KWA NINI AMUKUOMBA KUONANA NA RAIS NA KAMA MMENYIMWA KWA NINI AMKUTUAMBIA TUANGALIE TUANDAMANE AMA LA RAIS AWAONE KUPUNGUZA VIFO VILIVYOTOKEA

  MWISHO USHAURI
  NAOMBENI KABLA YA KUFANYA CHOCHOTE MUULIZANE WAPI MNAHISI SULUHISHO KULIKO KUENDEKEZA UPUMBAVU WA KUGOMA NA KUENDEKEZA VIFO VISIVYO NA MSINGI NA MWISHO KUISHIA KURUDI KULE KULE SERIKALINI MLIKOAMBIWA MADAI YENU YANASHUGULIKIWA/.....NIKICHEKESHO KUANDIKA ATI KIKWETE AKUJUA MADAI YA MA DK..HUU NI UPOPOMPO AKUNA KINACHOFANYIKA RAIS ANAWANGALIA NA ANASIKILIZIA KIMEENDELEA NINI MWISHO NASHAURI MA DK WENGINE MLIOENDKEZA HUU MGOMO

  MWISHO KUMRADHI SHEMEJI YANGU MAWAZO YANGU YASIINGILIANE NA NDOA ZENU MUSIHI NA DADAZETU VYEMA TU

  """""""""""KUPOTEA WAAKATI WA KWENDA KURUDI MNARUDI WENYEWE WATCHOUT""""""
   
 19. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180

  lowaasa akamuumbua leo wehu wanaamini raisi Ajui madai ya ma dk??loh
  'EL ALIWAAMBIA AKUNA ALICHOFANYA RICHMOND SJSMDHIRIKISHA KIKWETE
   
 20. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Nahisi kuna kitu mmrpuliziwa niko mbion kuonana na kanumba tutengneze movie yenu kwa kweli hii mve naamini itauzika maelezo
   
Loading...