Ni ajabu ila ni kweli: Hakuna mtanzania yeyote aliyewahi kushuhudia utawala mwingine zaidi ya wa CCM

TeamLowassa

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
1,495
936
Zimebaki siku 5 kabla ya watanzania kushuhudia utawala wa chama kingine!

Jumamosi ya tarehe 24 kuanzia asubuhi hadi asubuhi ya tarehe 25 hali ya wananchi itakuwa katika utulivu mzito sana. Wananchi watakuwa kwenye utulivu mzito kwa kuwa tangu uhuru, tangu kuzaliwa kwao hakuna mtanzania yeyote yule aliyewahi kuonja ladha ya kuongozwa na chama kingine tofauti na CCM. Duru za siasa zinaonyesha kuwa hapa barani Afrika kumebaki vyama viwili tu vikongwe, ZANU-PF ya Zimbabwe ya Robert Mugabe na CCM Tanzania ya Jakaya Mrisho Kikwete. CCM ya sasa ni CCM maslahi!

Wakati CCM maslahi wakipigana kufa na kupona kwa ajili ya kunusuru uhai wa mirija yao ya kiuchumi pamoja na washirika wao (yale mikataba ya siri ya wachina), watanzania nao waliobatizwa jina la malofa na wapumbavu wanapambana bila kukata tamaa kunusuru maisha ya vizazi na vizazi vya watanzania. Watanzania hawa wamezoea kupigwa mabomu na kuuwawa kila wakijaribu kupasa sauti zao juu ya utawala wa CCM!

Hata hivyo kwa mara ya kwanza kabisa watanzania wapumbavu na malofa wamedhamiria kusimama na kuhesabiwa kama mashujaa wapya waliowezesha ujio wa Tanzania mpya kwa watanzania wapya! Ni jambo la heshima na la utukufu pale unapoamua kutumia nafasi yoyote inayopatikana kwa ajili ya kupigania maisha ya watanzania wenzako!

Kwa kifupi niwatie moyo wapiganaji wenzangu, siku ya siku tupige kura na kulinda kura! Bila kulinda kura, bao la mkono linatuhusu asubuhi na mapema sana!

Mungu yupo pamoja nasi!
 
We wa wapi mkuu? Ungerekebisha uzi wako ili ueleweke vizuri, ccm imezaliwa mwaka 1977 sasa una maana hakuna mtazania aliyekuwepo kabla ya mwaka huo? Au hata kama serikali ni ileile toka uhuru ina maana hakuna mtanzania anayeishi kwa sasa ambaye alikuwepo kabla ya uhuru? Hebu rudi hapa utoe ufafanuzi .
 
Back
Top Bottom