Ni ajabu, askofu anaepaswa kua na mke mmoja hana mke, sisi ambao sio maaskofu tunalazimishwa kua na mke mmoja.

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,319
Waraka wa Paulo kwa Tito na kwa Timotheo unatamka wazi kua viongozi wa kanisa wanapaswa kua na mke mmoja. Hilo halina ubishi kabisa.

Dhana ya mke mmoja ni dhana ni kwa ajili ya maaskofu, mapadri na wachungaji.

Sisi ambao sio maaskofu hatulazimishwi kua na mke mmoja, hiyo ni hiyari yetu. Mke mmoja ni kwa ajili ya viongozi wa kanisa pekee.

Sasa unashangaa huku kwetu kwenye ukatoliki, anaepaswa kua na mke mmoja kama maandiko yanavyosema yeye hana mke, sisi ambao sio maaskofu tunalazimishwa kua na mke mmoja, maana yake sisi tunalazimishwa kua maaskofu, hii sio sahihi kabisa.

Mada inaendelea.
 
Ki uhalisia wanaume tuliooa ndio target kwa wanawake ambao wanahitaji kuolewa, hivyo basi naamini tulio ktk ndoa tunaongiza kuwa na wanawake wengi lakini mke mmoja..ukweli mchungu
 
Paulo huyo huyo anawataka mnaoweza kudhibiti tamaa zenu kutokua na wake kabisa.

Yesu ambaye ndiye aliyeleta injili je, alikua na wake wangapi?
 
Jamaa yangu.....hako kamchepuko achana nacho.
Usitafute uhalali
 
Back
Top Bottom