The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Sasa ni wazi kabisa Urais wa Donald Trump unaisha kwa aibu na fedheha kubwa.
Kitendo cha kuhamasisha wafuasi wake jana kuvamia jengo la Bunge la Congress (Capitol Hill) ili kuzuia bunge lisifanye kazi yake kumwidhinisha Rais Mteule Joe Biden (D) na makamu wake Kamala Harris ilikuwa ni ishara ya mwisho kuwa huyu mzee ni "mentally unfit" na hafai kukalia kiti cha Urais hata kwa siku 14 zilizobaki.
Sasa kwa sababu ya "uropokaji" wake bila ya kupima madhara ya kauli zake hizo, amefungiwa kutumia mitandao yote mikubwa ya kupashana habari duniani ikiwemo Facebook, Instagram na Twitter.
Inasemekana kwa sasa, yumo kifungoni cha kutopiga wala kupokea simu yoyote kwa yeyote.
Aidha, tayari utaratibu wa kumng'oa White House kabla hata ya tarehe 20/1/2021 siku ya kuapishwa Rais Joe Biden maarufu kama "impeachment" unaandaliwa kwa mujibu wa sheria za Marekani. Na hii ni dharura na itafanyika kwa udharura pia.
Tayari pia mawaziri wengi na maafisa wa taasisi nyeti za serikali kama FBI, CIA nk baadhi wameachia ngazi na wengine wanajiandaa kwa kuwa wamechukizwa na tabia ya Rais Trump isiyojali sheria na katiba ya nchi na hata kuhatarisha usalama wa RAIA na NCHI kwa ujumla.
Naye Makamu wa Rais, Bw. Mike Pence, amechukizwa sana na tabia ya Rais na katika hali ya kushangaza, akasema wazi kuwa, hakubaliani naye.
Na Republicans wenzake wamemtaka kuitisha baraza la mawaziri haraka iwezekanavyo ili kuweka njia ya kumwondoa Donald Trump madarakani kwa kutumia Article 25 ya katiba ya Marekani inayoweka utaratibu wa VP kuchukua madaraka ya Rais iwapo ameshindwa ku - discharge majukumu yake ya Urais kwa sababu zozote zile kabla ya mambo kuharibika zaidi.
Kwa kifupi Wamerekani wamechukizwa sana na kilichotokea jana tendo lililochagizwa na kauli za Rais. Hawatamani hata awe Rais kwa kwa siku mbili zijazo.
For sure kabisa, ni wazi sasa, kuwa Donald Trump hamalizi wiki moja ijayo akiwa Rais wa Marekani.