yusufu mtegwa
Member
- Oct 27, 2019
- 6
- 2
Kati ya friji ya mtumba na ya dukani IPI ni nzuri na brand IPI kwa jina. Thibitisha kama unatumia brand hiyo.
Fridge yeyote ambayo hana chapa ya Energy star inatafuna umeme kichizi!I give you technical advice
Nunua fridge dukani, hata kama ni la bei ndogo nunua dukani...
Ila mafundi wengi wa bongo ni hovyo sana, fridge ikisumbua kidogo anavuruga mfumo wote utashangaa fridge inapiga kazi 24/7 hata usipofungua wiki nzima.I give you technical advice
Nunua fridge dukani, hata kama ni la bei ndogo nunua dukani..
Fafanua mkuu, "hata usipofungua wiki nzima " maana nataka kupeleka friji kwa fundiIla mafundi wengi wa bongo ni hovyo sana, fridge ikisumbua kidogo anavuruga mfumo wote utashangaa fridge inapiga kazi 24/7 hata usipofungua wiki nzima.
Majuisiiii ya azam matamuuu hayooo...Mie nina Uzoefu na American Fridge.
-Brand Super General though nimeona zipo Brand nyingine nyingi Tafauti.
-Side by side doors with Water dispenser and -cocktail maker.
-Size 700L
-Sifa zake Kwanza zinagandisha bila kuweka barafu kabisaa hata tone kwenye freezer.
-Ulaji wa umeme ni wa kawaida sana(Zina energy server Compressors) maana ukifika some freezing points inzajima, then itajiwasha automatically.
-Ina Space kubwa mno for a family.
Brand New ni bit expensive hadi 1.5 to 2m.
Ila mtumba waeza pata hadi 900k clean.
Ni Best Fridge aisee.
View attachment 1573882View attachment 1573884View attachment 1573885
Vipi kuhusu brand ya BOSSFriji najua ufanisi wake moja tu, Samsung na ni zuri sana lakini tatizo bei imechangamka. Nina uzoefu na freezers hope utaapply kwenye fridge, pia kabla usichukue freezer/fridge ya mtumba yenye miaka mingi. Wachache sana walikuwa wameanza kuapply energy saving, zipo freezer zinachukua umeme karibu mara mbili, pili freezer za mtumba kutoka Ulaya zina category ya nchi yao, yetu inatakiwa kuwa na label ya T(Tropical) kwa ufanisi bora.
BEKO: Zimekuwa designed kula umeme mdogo sana na kutunza baridi muda mrefu sana baada ya kuzima hasa usipofungua fungua. Downside halifanyi kazi vizuri kipindi cha joto kali pia kwa freezers zinakuja bila compressor fan, kipindi cha joto unaweza kufunga kuongeza ufanisi, kipindi cha hali ya hewa nzuriutalipenda sana na bei yake ya kawaida.
West Point: Zuri sana kwa ufanyaji kazi na energy saving, bei zake zimechangamka kidogo. Nadhani kwa freezers ndio zuri zaidi kwa haya yanayokuja kwa wingi nchini.
Delta: Sikushauri, umeme unaenda na ufanisi sio mzuri sana.
Hisense: Classic na bei imechangamka, unaweza kukuta appliance ni kubwa lakini ikachukua umeme kidogo na ufanisi mzuri. Mara nyingi fridge/freezer ujazo ukiwa mkubwa huchukua muda kugandisha.
Bosch: Hayapatikani sana nchini, ni bora kuliko yote kwenye list hii. Ukilipata hata la mtumba beba, alianza kutumia energy saving zamani. Bei imechangamka.
Mo electric: Sijui kafanyaje lakini ameweza, bei ya mtanzania.
Bruhm: Kwa freezer ukiweka vitu vingi vipya visivyo na ubaridi, compressor inafeli. Unasort kwa kuweka extra compressor fan pia usiliweke sehemu palipojibana sana, compressor inahitaji sana hewa.
Von: Yuko vizuri sana
Kama unataka kununua mtumba, usiende mathalan Magomeni pale ukachukua mtumba wa ulaya wa miaka na miaka, umeme mwingi au zilishabadilishwa compressor au pipes zimetoboka(fundi atakuja na suggestion usukie pipe ndani, usikubali, bora ukubali hasara)
Kwa freezer, mtumba huwa tunanunua ambayo mtu alinunua dukani then akaamua kuuza na mara nyingi sababu huwa biashara imekufa. Unaweza kumpa hela ya umeme aiwashe uifate asubuhi yake. Uikute ina alama ya barafu kuanzia juu mpaka chini, kama iliwekwa kitu kidogo, kiwe kimeganda vizuri.
FRIDGE ina mfumo ambao ikipata hali inayopaswa inajizima ili kuendelea kutotumia umeme, kama "AC" sasashida inakuja kwa mafundi wetu huwa wengi wamesoma miaka hiyo wanavuruga huo mfumo kwa kutoifahamu na kufanya iwake moja kwa mojaFafanua mkuu, "hata usipofungua wiki nzima " maana nataka kupeleka friji kwa fundi
Hii ni mtumba au mpya? Ulinunua wapi hii?Mie nina Uzoefu na American Fridge.
-Brand Super General though nimeona zipo Brand nyingine nyingi Tafauti.
-Side by side doors with Water dispenser and -cocktail maker.
-Size 700L
-Sifa zake Kwanza zinagandisha bila kuweka barafu kabisaa hata tone kwenye freezer.
-Ulaji wa umeme ni wa kawaida sana(Zina energy server Compressors) maana ukifika some freezing points inzajima, then itajiwasha automatically.
-Ina Space kubwa mno for a family.
Brand New ni bit expensive hadi 1.5 to 2m.
Ila mtumba waeza pata hadi 900k clean.
Ni Best Fridge aisee.
View attachment 1573882View attachment 1573884View attachment 1573885
😂 😂 😂 😂 😂AborderRising, Boss, Sundarna uchafu mwingine wa kichina
Nilinunua LG mwaka 2008 mpaka leo sijui maana ya fundi, ila ndo kwanza majuzi imeunguza taa ya ndani(bulb)I give you technical advice
Nunua fridge dukani, hata kama ni la bei ndogo nunua dukani.
Advantage ni kwamba, mafridge ya kisasa ni Power saving unaweza kuta fridge inatumia units 150 kwa mwaka mzima.
Usijichanganye ununue mtumba, yanakula umeme hatari sababu ya wattage
Kuhusu brands wala usibabaike sababu yote ni ya kichina/ Sub standard tafuta unalo lipenda kwa rangi, umbo urefu or size/ capacity Eg. Beko, Mo electro, Aborder Rising, Boss, Sundar na uchafu mwingine wa kichina
Kama unataka Fridge genuine, nenda kwa wakala husika Eg. LG, Samsung, Hisense, Hitach, Sharp, Bose na most known brands nyingine.