Ni aibu ya mwaka: 60 tena

Freiston

JF-Expert Member
Oct 25, 2020
302
339
Ni miaka 60 sasa tangu Taifa letu pendwa kujipatia uhuru wake toka kwa watu wasiostaarabika wa zamani hizo. Leo hii tunapoadhimisha miongo 6 ya uhuru, umoja, amani na mshikamano kuna watu wazima na akili zao timamu wanakaa mitandaoni ni kutukanana mambo ya kijinga kijinga kabisa kama vile watoto. Badala ya kukaa chini meza moja na kuwashauri vyema viongozi wa serikali namna bora ya kufikia miaka 60 mingine tukiwa na umoja zaidi na mshikamano kama Taifa huru na lenye kujitegemea.

Siku hizi hoja zimekuwa zikipigwa na rungu, matusi na kejeli na siku inakuwa imeisha. Katika ulimwengu huu wa watu waliostaarabika na kuwa na matarajio makubwa ya kushika nyadhfa kadha wa kadha serikali, ni mbaya sasa kuwa mropokaji wa maneno yasiyofaa, usijua yanachafua taswira ya Taifa letu pendwa.

Niwasihii sana, tofauti zetu sisi kama vijana, ni vyema tukazizika kaburini na tukaishi kwa namna ya kuvumiliana na kupendana kwa kuwa watanzania wote ni ndugu.

RIP Mh. Mwl. JKN
RIP Mh. BWM
RIP Mh. DR. JPM
RIP Mh. Maalim SRH

HERI KWA MARAIS WASTAAFU

JMK
HAM

KAZI IENDELEE

RAIS WA JMT Mh. SSH
RAIS WA Zanz. Mh. Dr. HM

VIONGOZI WA UPINZANI

Ndg. HM
Ndg. ZZK
Ndg. JM Mama Tanzania
Ndg. Prof. L
Ndg. RR

Wote kwa pamoja nawatakia heri ya 60 ya Uhuru wa Tanganyika sasa Tanzania bara 🇹🇿. Amani tuliyonayo ni kwa neema za Mungu tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom