LAZIMA NISEME
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 232
- 260
NI AIBU WABUNGE WA UPINZANI KUTUMIKA KUTETEA MAFISADI.
• Sasa mafisadi watumia wabunge wa upinzani kujisafisha.
• Waahidiwa donge nono kufanikisha kuichafua kazi nzuri inayofanywa na serikali
• Mabilioni yaliyoibwa na kufichwa na mafisadi hao, yatumika kulipa upinzani
• Waandishi nao wamehongwa mamilioni ili kuichafua serikali
Kwa mujibu wa taarifa zinazopatikana NIDA ni kwamba Gharama za mradi wote wa kuzalisha vitambulisho vya uraia (Kitambulisho cha Taifa) ni zile zile ziliokuwa katika mkataba hata pamoja na kufanyiwa maboresho muhimu katika kitambulisho cha uraia.
“Utengenezaji, usambazaji na ukandarasi wa miundo mbinu ya vitambulisho vya taifa unagharimu kiasi cha Dola za kimarekani $3.45 kwa kila kitambulisho mpaka kinapokabidhiwa kwa Mtanzania. Bei hii ya kitambulisho ndiyo bei iliyopo katika mkataba wa awali hata pamoja na maboresho ya msingi yaliyofanyika” Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA Rose Mdami amekiambia chanzo chetu.
Ikumbukwe kwamba kiwango kiasi hicho cha dola ya Marekani ni sawa na shilingi ya TANZANIA 7,693.5 tu na si shilingi 17,000 kama inavyodaiwa na wabunge wanaotumika na mafisadi.
Kwa mujibu wa maelezo sahihi ya Bi Mdami, maboresho yaliyofanyika ni kuweka saini ya mmiliki wa kitambulisho, kuweka tarehe ya kuzaliwa na kuweka saini ya mtoaji wa kitambulisho na vyote baada ya kuongezea, hakukuathiri bei ya kitambulisho.
Kuwepo kwa saini ya mmiliki, saini ya mtoaji wa kitambulisho na tarehe ya kuzaliwa kumepandisha hadhi ya kitambulisho cha uraia cha Tanzania na kukifanya sasa kuaminika katika taasisi za kifedha, benki, kupigia kura, kuingilia nchi jirani kama Kenya na nyinginezo pamoja na kupata Pasiporti mpya ya kielekroniki na faida nyingine nyingi ambazo HAZIKUWEPO katika kitambulisho kilichokuwa kikitengenezwa awali kabla ya Mheshimiwa Rais Magufuli hajawatumbua watendaji wakuu wa wakati huo.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kwamba wabunge wa upinzani ambao hawana tena pesa kutokana na serikali kuziba mianya yote ya kujipatia fedha kijanjajanja bila kufanyakazi; sasa wamebuni mbinu ya kujikimu na bila aibu wanapokea maelekezo kutoka kwa vibaraka wa tuhumiwa wa ufisadi kwa ahadi ya kulipwa donge nono kwa kila elekezo ili kuwasafisha mafisadi hao kwa kuwafanya wananchi waamini kwamba maboresho yaliyofanyika yaliongeza gharama za kitambulisho cha taifa jambo ambalo sio la kweli.
Taarifa za kiuchunguzi pia zilibaini kuwa mafisadi hao wamejipanga kujisafisha kwa gharama yoyote kama maandalizi yao ya kuharibu uchaguzi mkuu mwaka 2020 kisha mafisadi hao kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa 2025.
Baadhi mafisadi na vibaraka wao ambao mawasiliano yao na wabunge wa upinzani pamoja na waandishi yamenaswa wakioongea; Ni wale vigogo walioondolewa NIDA kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na matumizi makubwa ya pesa ambayo hayakuendana na kazi iliyofanyika. Vigogo hao ambao majina yao yapo, wamewaahidi wabunge na waandishi hao kuwapa mgao wa pesa walizochuma katika dili zao za kifisadi kama malipo kwa kuichafua kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano.
Mbunge mmoja wa upinzani mwishoni mwa wili iliyopita aliibuka na kudai kwamba gharama ya mradi wa vitambulisho vya uraia zimeongezeka baada ya kufanyika kwa maboresho jambo ambalo sio la kweli huku akitoa takwimu na madai ya kizushi kwa lengo la kuigombanisha Serikali na wananchi wake.
Uchunguzi pia umebaini, wabunge wa upinzani watajitokeza kwa nyakati tofauti tofauti kuongea uwongo kwa nia ya kupotosha umma. Hali kadhalika waandishi na vyombo vya habari vilivyopangwa kuuaminisha Umma na jamii ya kimataifa taarifa hizo za kuzusha, uchunguzi umebaini vimeamrishwa kuanza kutoa habari hizo mwezi huu mfurulizo hadi mwezi Julai 2020 ili kukamilisha awamu ya kwanza ya kuvuruga juhudi za serikali na kuwasafisha mafisadi.
Vigogo wengine walionaswa wakitoa ahadi za malipo kwa wabunge hao ni wale walioondolewa Uhamiaji kwa makosa ya kutaka kuiingiza serikali katika hasara ya zaidi ya dola za marekani milioni 226, Ambapo sasa kwa ujumla wake mradi wa mfumo wa uhamiaji mtandao (e-immigration) umefanyika kwa dola za Marekani milioni 57 tu!
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala alipozungumza wakati wa uzinduzi wa ePassport amesema kwamba mradi e- immigration utafanyika kwa awamu nne;-
(i). e-Passport ilianza Septemba 2017 hadi Januari 2018 Imeshazinduliwa tarehe Mosi mwezi Februari, 2018 na Mhe. Rais Magufuli.
(ii). e-VISA Februari hadi Juni 2018.
(iii). e-Border utaanza Juni hadi Septemba 2018 na
(iv). e-Immigration kwenye Balozi zote nje ya Tanzania utaanza Septemba hadi Disemba 2018.
Miradi yote mnne itatekelezwa kwa thamani ya dola za kimarekani Milioni 57 tu pamoja na kodi kwa awamu zote na hakuna malipo mengine yatakayoongezeka.
Kufanikiwa kwa mradi huu e-Immigration kwa gharama ya dola za Marekani milioni 57 tu, limewaumbua vigogo walioondolewa Uhamiaji na sasa wanahaha kwa aibu wakidai kwamba gharama iliyotajwa ni kwa ajili ya mradi mradi mmoja tu wa e-Passport tu jambo ambolo sio la kweli.
Ni haki ya watanzania kufahamu juu ya matumizi ya pesa ya kodi zao kwani wanapopata ukweli kuhusu matumizi ya kodi wanayolipa inawapa hamasa kuendelea kufanya kazi kwa ari, kizalendo, kiadilifu na kulipa kodi zaidi kwa mafufaa ya jamii nzima.
Ni wajibu wa kila mtanzania kuwa macho na wale wote wanaotumiwa na mafisadi kwa ajili ya kuichafua serikali ya awamu ya tano kwa nia ya kuzuia juhudi za kupambana na ufusadi zinazofanywa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli na watendaji wake.