Ni aibu Tanzania mpaka sasa hatuna Mahakama ya kuhoji matokeo ya Urais

Hatuna tofauti na Burundi yaan kwa utawala huu unaokuja ukikosoa hata kama serikali imekosea unafungwa kweupe
Hii ni mbaya sana wengi watakuwa na vinyongo hivyo watakuwa wanaombea mabaya yaan mungu alikosea sana kunifanya nizaliwe taifa la mazuzu namlaumu sana mpk siku ya mwisho
 
Kama Mahakama ya mafisadi ipo kama geresha tuu...

Kua na Mahakama ya kuhoji ya Urasi ni ndoto...



Cc: mahondaw
 
Kwa karne hii ya 21 yenye vizazi vya wasomi waliobobea katika nyanja mbalimbali hapa Tanzania hatuna mahakama ya kuhoji matokeo ya Urais ni aibu sana

Vinchi vidogo vidogo vyenye population ndogo kama Malawi wamekuwa na uelewa wa kuwa na mahakama ya kuhoji matokeo ya Urais halafu Tanzania tunakuwa na wasomi wanaojali matumbo yao na kuabudu watawala

Nchi nyingi duniani wanaofanya uchaguzi wa vyama vingi waliishaona mbali kama kutoridhika kwenye uchaguzi iwepo mahakama ya kuhoji matokeo ili kuondoa utata still sisi tupo kwenye ujima ni aibu kwa wanaojiita wasomi kwenye hii nchi

Kenya walijifunza kwa uchaguzi ule uliozua ghasia chini ya Samwel Kiwitu na kuja na katiba ambayo imeweka kila kitu separated, na isingekuwa katiba mpya hii referendum ingelete mzozo mnoo

Mnaojiita maprofesa,madakrari na wanazuoni wa Tanzania ni aibu kwenu na vizazi vyenu

Kama haiwezekani basi Tanzania ijulikane ni nchi ya kishoshilisti na tufute mfumo wa vyama vingi kama zilivyo nchi za kishoshilisti tusifanye maigizo

La sivyo muundo huu wa uchaguzi kama sio sasa utakuja kugharimu maisha ya watanzania kwa malaki

Mpaka sasa jeshi la polisi wanapata wakati mgumu kwa sababu wangewambia upinzani nendeni mahakamani mkadai haki,mahakama haipo imebaki jeshi la polisi kutoa vitisho kila dakika hii ni aibu Tanzania na wasomi wake

Ni aibu sana lakini kwa hao maprofesa wa matumbo wataona muhimu kunyazisha watu kwenye mitandao lakini kuweka utaratibu mzuri wa kupata Rais wanaona hakuna haja. Kwahiyo wizi kama wajuzi huu wa waziwazi wanatangaza mshindi ndo basi. Hili ni tatizo kubwa sana
 
Most of African minds
IMG_20201112_103629.jpeg
 
Pia ni makosa makubwa Sana kuongozwa na katiba chakavu. Katiba mpya ni kwa faida ya wote watawala na watawaliwa japo watawala awaelewi hilo, uja kuelewa baadae Sana baada ya mfumo kuwatupa na hawana namna tena ya kushawishi upya mchakato. Thus tumeona Lowasa, Sumaye, membe, Mkapa eti wakitamani katiba mpya baada ya mfumo kuwatupa Hali waliweka pamba walipokuwa na nafasi hio
 
Ni aibu sana lakini kwa hao maprofesa wa matumbo wataona muhimu kunyazisha watu kwenye mitandao lakini kuweka utaratibu mzuri wa kupata Rais wanaona hakuna haja. Kwahiyo wizi kama wajuzi huu wa waziwazi wanatangaza mshindi ndo basi. Hili ni tatizo kubwa sana

Huwa na akili baada ya mfumo kuwatupa yaani wakiondolewa mezani.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom