Ni aibu serikali kushindwa kuadhimisha siku ya UKIMWI

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,427
85,872
Yaani tumeshindwa hata kutoa article tu? Ni kweli UKIMWI umekua sio tatizo nchini? Week iliyopita tulikutana pale Kinondoni ili kujua at least namna ya kuadhimisha siku hii maana serikali haijatoa hata senti tano, tukaamua Washika Dau wenyewe ndio tujichangishe ili tuadhimishe. Kwangu mimi naona kama serikali inacheza na hili janga.

Maadhimisho haya yalisaidia sana kueneza taarifa sahihi na kuhamasisha watu juu ya madhara ya UKIMWI, leo hii nchi nzima kimyaaaaa. Kama unajiamini huna UKIMWI basi kumbuka una ndugu jamaa au marafiki wanasumbuliwa na huu ugonjwa. Siku yakikufika basi utajua nini maan yake.

Kuna mdada mwaka jana au juzi alianzisha thread hapa juu ya UKIMWI ulivyokuwa unamtesa, ile thread ilinitoa machozi lakini leo hii serikali imekaa kimya. Haya bhana

Invisible naomba nitafutie ile thread ya yule Dada, nadhani ilikua inasema UKIMWI bila Hela ni Mateso!!!! Uniwekee hapa ili kuikumbusha serikali
 
habari wanajanvi??

hivi leo si tarehe 1 des siku ya ukimwi?? hv kwa mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyikia wapi?? kauli mbiu yake jee?? au MTUKUFU wa nchi kafuta maadhimisho hayo kwa kile kinachosemekana ni kubana matumizi??? na huku tunapoelekea ARV zitaanza kuuzwa ili kubana bajeti.

ndugu wanajamvi naomba majibu asanteni
 
Yaani tumeshindwa hata kutoa article tu? Ni kweli UKIMWI umekua sio tatizo nchini? Week iliyopita tulikutana pale Kinondoni ili kujua at least namna ya kuadhimisha siku hii maana serikali haijatoa hata senti tano, tukaamua Washika Dau wenyewe ndio tujichangishe ili tuadhimishe. Kwangu mimi naona kama serikali inacheza na hili janga.

Maadhimisho haya yalisaidia sana kueneza taarifa sahihi na kuhamasisha watu juu ya madhara ya UKIMWI, leo hii nchi nzima kimyaaaaa. Kama unajiamini huna UKIMWI basi kumbuka una ndugu jamaa au marafiki wanasumbuliwa na huu ugonjwa. Siku yakikufika basi utajua nini maan yake.

Kuna mdada mwaka jana au juzi alianzisha thread hapa juu ya UKIMWI ulivyokuwa unamtesa, ile thread ilinitoa machozi lakini leo hii serikali imekaa kimya. Haya bhana

Invisible naomba nitafutie ile thread ya yule Dada, nadhani ilikua inasema UKIMWI bila Hela ni Mateso!!!! Uniwekee hapa ili kuikumbusha serikali

Wizara ya Afya ilitakiwa ije na kauli mbiu ya siku ya ukimwi na at least kuandaa makongamano na kutupa report ya nchi kwa sasa na nini kifanyike kupunguza maambukizi.

Nafikiri idadi ya maambukizi mapya inakua kila mwaka na lazima tujue na kukumbushana kuwa Ukimwi upo na unauwa.
 
IMG_20161104_213608.JPG

Ukimwi upo na hauzoeleki, tujitunze pia tuwafariji ndugu/jamaa/marafiki walioathirika.
 
Yaani tumeshindwa hata kutoa article tu? Ni kweli UKIMWI umekua sio tatizo nchini? Week iliyopita tulikutana pale Kinondoni ili kujua at least namna ya kuadhimisha siku hii maana serikali haijatoa hata senti tano, tukaamua Washika Dau wenyewe ndio tujichangishe ili tuadhimishe. Kwangu mimi naona kama serikali inacheza na hili janga.

Maadhimisho haya yalisaidia sana kueneza taarifa sahihi na kuhamasisha watu juu ya madhara ya UKIMWI, leo hii nchi nzima kimyaaaaa. Kama unajiamini huna UKIMWI basi kumbuka una ndugu jamaa au marafiki wanasumbuliwa na huu ugonjwa. Siku yakikufika basi utajua nini maan yake.

Kuna mdada mwaka jana au juzi alianzisha thread hapa juu ya UKIMWI ulivyokuwa unamtesa, ile thread ilinitoa machozi lakini leo hii serikali imekaa kimya. Haya bhana

Invisible naomba nitafutie ile thread ya yule Dada, nadhani ilikua inasema UKIMWI bila Hela ni Mateso!!!! Uniwekee hapa ili kuikumbusha serikali
Halafuuu iweje ndiooinapunguza ukimwi unajuawalewashenzi waukimwi sikukamayaleo wanasemaga wametumia ah nap nahukuzimeenda mifukonimwaoo srkl awabahatishii
 
Wizara ya Afya ilitakiwa ije na kauli mbiu ya siku ya ukimwi na at least kuandaa makongamano na kutupa report ya nchi kwa sasa na nini kifanyike kupunguza maambukizi.

Nafikiri idadi ya maambukizi mapya inakua kila mwaka na lazima tujue na kukumbushana kuwa Ukimwi upo na unauwa.

Wakat yalipokuwa yakifanyika tulikuwa tunasema ni Matumizi Mahayana ya fedha
 
WaTanzania wau wa ajabu sana, watu wakfanya makongamano na maadhimisho mnapiga kelele, amekuja Rais wa kukataza maadhimisho na makongamano kelele! mwatakani nyie watu?

Hebu tupe list ya nchi ambazo huo ugonjwa umeathiri na wanafanya hayo maadhimisho kila mwaka!
 
Mashirika ya misaada ya nje haiwezi kuona kuwa suala hili halisapotiwi na serikali kwa huu ukimya?
 
Acheni uvivu mnalilia maadhimisho ya Ukimwi ili mpate off ya kazini
Tuache ubabaishaji mpaka leo kuna mtu hajui Ukimwi ni nini? Kuna mtu hajui kujikinga?
Fanyeni kazi

Hapa kazi tu
 
Ukimwi ni janga kubwa lakini ni ukweli kwamba litaisha kwa kufanya makongamano? Na kuja na kaulimbiu mpya kila mwaka? Naamini hii siyo dawa ya hili dubwana.

Ikiwa tutatarajia makongamano na kaulimbiu zimalize hii shida tutakua hatuna tofauti na mkuu wa mkoa yule ambaye yuko bize kuonekana kwenye tv akinadi usafi huku hatua za kufanya eneo liwe safi hazichukuliwi.

Tunahitaji kuwe na bajeti ya kuleta ARV kwa ambao wameshaathirika, kuwe na bajeti ya kukuza uelewa wa wananchi juu ya ugonjwa husika, vituo vya afya viwepo na manesi na madaktari waliofuzu wawepo.
Hivi vyote havitaletwa na hayo makongamano au kaulimbiu, hapo utakua unacheza makida makida.
 
Acheni uvivu mnalilia maadhimisho ya Ukimwi ili mpate off ya kazini
Tuache ubabaishaji mpaka leo kuna mtu hajui Ukimwi ni nini? Kuna mtu hajui kujikinga?
Fanyeni kazi

Hapa kazi tu
Kuna kipindi nilikiangalia kwenye tv mtangazaji alikua anazunguka mtaani anauliza watu juu ya Ukimwi na kama wanajua unavyoambukizwa majibu yao yalikua yanaonesha wazi hawana uelewa mpana juu ya swala husika, na hapo ni Dar eneo ambalo lina access na info zote ukizitaka.

Rais Zuma katika kesi yake ya kubaka akasema alifanya ngono na mlalamikaji kwa makubaliano na alipomaliza alienda kuoga ili kupunguza uwezekano wa kupata Ukimwi, huyu ni raisi wa taifa kubwa kwa Afrika yetu akaonesha hata yeye hana uelewa juu ya Ukimwi.
 
Kuna mtu asiyejua madhara ya ukimwi?

Kuna mtu asiyejua namna ya kujikinga na ukimwi?

Miaka yote ambayo serikali ilikuwa inaadhimisha takwimu zinaonyesha ugonjwa huu umepungua au kuongezeka?

Kila mtu TZ anajua kama ukimwi ni ugonjwa hatari ,kwahili nampongeza rais
 
Back
Top Bottom