Ni aibu sana kwa chama kikongwe kama CCM kutumia polisi kujisitiri

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,585
217,973
Mwaka 1992 Nchi ya Tanzania iliukubali rasmi MFUMO WA VYAMA VINGI VYA SIASA , ikatungwa sheria mpya ya vyama vya siasa na kuruhusu Kusajiliwa kwa vyama mbalimbali vilivyokidhi matakwa ya sheria hiyo mpya , ili kuviruhusu rasmi kuingia kwenye ushindani wa sera na kuziuza kwa Wananchi kwa lengo la kupigania kuongoza nchi kwa njia ya kidemokrasia .

Nachukua nafasi hii kuwashukuru viongozi wa wakati ule kwa kuruhusu mfumo huu wa kisasa wa kuendesha nchi .

Kwenye kila jambo zuri kuna upande wa ubaya wake , kitendo cha viongozi kuruhusu mfumo huu wa kisasa ikageuka kuwa NDIO KABURI LA CCM nchini , wananchi wakafundishwa jinsi ccm ilivyoleta dhiki na mkusanyiko wa shida zote katika nchi hii , na kwa kauli moja wakakubaliana kuiondoa ccm madarakani , yaliyotokea ni historia .

Baada ya kitendo hicho ccm imestuka na kutambua kwamba HAINA TENA UWEZO WA KUSIMAMA JUKWAANI NA KUWAAMINISHA WANANCHI KATIKA JAMBO LOLOTE , hivyo ikaamua kutumia JESHI LA POLISI KUUA DEMOKRASIA NCHINI KWA GHARAMA KUBWA SANA YA JASHO NA DAMU ZA WAPINZANI .

Yanayotokea nchini kila mmoja ni shahidi .
Wanasiasa wa upinzani wanaogopwa na ccm kuliko hata umasikini , njaa na maradhi .

Itoshe tu kusema kwenye jukwaa la siasa la Tanzania , BILA POLISI CCM NI WEPESI KULIKO PAMBA .

KWA SASA POLISI NDIO MWAMVULI WAO WA KUJISITIRI NA MAFURIKO YA WAPINZANI .
 
Tatizo Watz tulizoea sana kuendekeza siasa. Mtu Jumatano, saa sita mchana anataka awe kwenye mkutano wa hadhara. Hata kwa Trump wanakoimba democracy hawafanyi hivyo!
 
Hivi mwenyekiti wa ccm wa sasa hivi anasikilizaga hutuba za mwl,nyerer kweli?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Tatizo Watz tulizoea sana kuendekeza siasa. Mtu Jumatano, saa sita mchana anataka awe kwenye mkutano wa hadhara. Hata kwa Trump wanakoimba democracy hawafanyi hivyo!
Kwani polepole anafanya siasa saa ngapi ? Halafu kingine ni hiki , Tangu mwenyekiti wa ccm aisigine katiba ya nchi kwa kukataza mikutano ya siasa ni maendeleo yapi yaliyofanyika ?
 
Kwani polepole anafanya siasa saa ngapi ? Halafu kingine ni hiki , Tangu mwenyekiti wa ccm aisigine katiba ya nchi kwa kukataza mikutano ya siasa ni maendeleo yapi yaliyofanyika ?
Siasa ni maisha kila siku hakuna siasa ni sawa na kuwa taifa lililo ktk machafuko kwa hiyo Sisi ni taifa huru kinachotafutwa na mtawala ni laana ya kuliumiza hili taifa lenye umoja

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Siasa ni maisha kila siku hakuna siasa ni sawa na kuwa taifa lililo ktk machafuko kwa hiyo Sisi ni taifa huru kinachotafutwa na mtawala ni laana ya kuliumiza hili taifa lenye umoja

Post sent using JamiiForums mobile app
True ! Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba , CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI .
 
Back
Top Bottom