Ni aibu kwa mheshimiwa Rais kusema haya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni aibu kwa mheshimiwa Rais kusema haya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Feb 11, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni aibu kubwa kwa Mheshimiwa Rais Kikwete kusema kuwa hawajui wamiliki wa Dowans

  Maelezo yaliyotolewa na Mh Kikwete kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake binafsi na ama wajumbe wa kamati nyeti za chama chake kuwa yeye hawajui na wala hajawahi kukutana na wamiliki wa Dowans ni kujivunjia heshima yeye na wasaidizi wake.

  Kama kweli Mh Kikwete angetaka kuwafahamu wamiliki halisi isingechukua hata wiki mbili {ana miundombinu na rasilimali za kuweza kufanya hivyo}, manung'uniko juu ya Dowans/Richmond yana zaidi ya miaka minne sasa na imemchukua zaidi ya wiki nne kulizungumzia suala hili baada ya mahakama ya ICC kuiamuru serikali kulipa. Katika hali ya kawaida tungetarajia basi Rais awe muungwana atusaidie wananchi wake kupata ukweli baada ya watu kumtuhumu yeye binafsi na kama kweli yey hapendi kuona Dowans ikilipwa kama alivyosema (kitu ambacho kinatia shaka kama kweli huu ndio msimamo wake).

  Dowans/Richmond ni bomu linaloweza kusambaratisha mshikamana na utengamano wa nchi hii... kama tulivyoona wanafunzi wakidai kuongezewa posho yao na wakihusisha madai yao na serikali kuwalipa Dowans.. TUCTA wana madai ambayo hayajalipwa na serikali kwa kisingizio kuwa haina hela, wanaweza sasa kukaza uzi kwani wanajua serikali ina pesa: walimu, madaktari, n.k. nao wamekuwa wakilalamika kuwa mishahara yao ni duni... itakuwa nao wakisisitiza kuwa waongezewe mishahara kwa kuwa mwajiri wao ambaye mara zote amekuwa akilalamika kuwa hana pesa kumbe anazo za kuchezea?

  Inawezakana tu kwa Mh Rais kusema hawajui wamiliki wa Dowans kama hasemi ukweli ama hayuko makini, kwa mtu yeyeto aliye makini na mwenye mamlaka aliyonayo Kikwete na kwa kuwa alikuwa amaeamua kuvunja ukimya na kuamua kulisemea hili alitakiwa atoe maelezo yanayojitoshereza, siyo porojo alizotoa pale Dodoma siku ya maadhimisho ya miaka 34 ya CCM.

  Ni aibu kwa watu wenye uelewa kuridhika na kusifia maelezo yale ya Rais, ni aibu kwa wote waliokuwa wakimsikiliza na kumshangilia kwa maelezo yale ya rejareja...

  Kama ni kweli Rais hatuambii ukweli basi ni aibu nyingine kubwa!
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  JK hawajui Dowans wala Richmond

  JK hajui kwa nini Tanzania ni maskini

  JK alienda Ngorongoro mwaka jana wakati wamasai na mifugo yao wanakufa kwa njaa na ukame, akamsingizia Mungu eti yeye ndo hajatema mvua, kana kwamba Mungu ndie aliekata miti au overgraze. Kumbe ni Raisi asie jua kazi zake.... Anajua global warming na climate change are Goddy while the whole world including his kids knows its man made.
  JK anajua kilimo kwanza kufanikiwa ni kuwa na ardhi nyingi na kuwapa wakulima ma-trekta.... kumbe it's smthg that needs an integrated approach.... miti iwe mingi, nishati ya kupikia ibadilike etc... No wonder Tevezya anakuja na maazimio ya Cancun kwamba watu wasikate miti, kesho yake Wizara ya MAliasili na Utalii wanatoa tangazo redioni kuhamasisha watu walipie MKAA waliokata ili kuzidisha kodi kwa serikali.

  JK anajua kuwa na shule nyingi na chuo kikuu kikubwa ndio kuwa na elimu bora etc......

  KIFUPI JK kwa maana ya Jakaya Kikwete HAJUI KITU....................... NI AIBU. Remember birds of same feather flock together, hata mawaziri wake ni vivyo hivyo....
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Umesomeka mkuu
   
Loading...