Ni aibu kuu wazazi wako wakulee halafu bado waje walee tena mkeo na watoto wako

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,124
11,114
Hii tamaduni ilianzia maeneo ya pwani hasa kwa wazaramo ndio ilikuwa tabia yao yaani mtu mzima bado anaishi kwao hana kazi yoyote, anaenda kuzalisha huko alafu mke na mtoto analeta nyumbani wazazi wake ndio wanalea

Wengine walikuwa wanakimbilia mjini wanacheza rafu wanazalisha wanawake alafu wanawapandisha kwenye mabasi kuwapeleka vijijini kwa wazee wao kwa kisingizio cha maisha magumu

Lakini sasa imekuwa ni rasmi wakuu kila sehemu hapa tz vijana wanatesa wazazi wao, vijana tumeshindwa kuwaonea huruma waliotulea, badala ya kuwasaidia waliotulea sisi ndio tunazidi kuwaongezea mizigo

Naongea hayo maana kuna jirani yangu hapa mmama wa kindengereko aliolewa na mzaramo kwa bahati mbaya mmewe alifariki wakati watoto wa dogo, ana watoto watatu, mama kajikaza kulea watoto hadi wakawa wakubwa

Mmoja wakike kazalia watoto wawili hapo hapo Nyumbani, na wengine wawili wa kiume wameleta hapo hapo nyumbani wanawake zao na watoto juu na kazi hawafanyi yani mama yao ndio anachakarika tu na biashara ndogo ndogo kulea huo mzigo.

Vijana hebu tubadilike jamani
 
Kosa ni la huyo mzazi,japo uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi ila mtoto akifika umri fulani "fyekelea mbali" ili akapate akili huko mbeleni,kuendelea kuwalea na kuwalea watoto na wake zao ni kuzidi kuwatia uvivu na kuwafanya kuona kua hayo ndio maisha yao tayari na hapo ndio wameshafika,

"Kamata huyo mwanao,mkewe na watoto wao kisha shuka nao jumla jumla kwa kuwafyeklea mbali"
 
Ni muhimu kuwakumbusha watu wa aina hiyo, ila kiukweli asilimia kubwa ni waoga wa kuFace Life.. Lakini pia mbeleni Uwa wajiona watu wasio heshimika na ni wapiga mizinga mashuhuli na wenye mambo ya kulaumu laumu kila wakati pamoja na Usmart wa nguo kumbe kichwani Empty.
 
Maisha magumu, wacha tuendelee kukaa kaa angalau awamu hii ipite.
Muda haurudi nyuma ndugu. Ukipangilia leo yako vizuri kesho ni Utamu na burudani huoni vizee vya kizungu vinavyo kula Bata Afrika? Mpaka dada na kaka zetu wanajipitisha pitisha?
 
ni aibu ila maisha ya sasa kwenda kinyune na mipango/ulivyo tarajia ni rahisi mno cha msingi ni kuomba backup ya wazazi wakati ukiendelea kupambana.

hao wanaowapa mzigo wazazi hawakupenda...!
 
Huwa naamini hakuna binadamu ambaye hapendi maisha mazuri, hapendi kukaa bila kazi , hapendi kuishi hayo maisha unayosema.

Wote tunapenda kuwa na kazi, maisha mazuri nk ila huwa yatukuta tu.
 
Sioni aibu hapo.
Damu nzito kuliko Maji.

Hata mwana mpotevu baada ya kuondoka nyumbani na kwenda kupata tabu...akaamua kurudi nyumbani kwa baba maana kule wanakula na kusaza.
 
Tabia ya binadamu, ukimuonesha unaweza kuwalea nas atakuletea na wajukuu uwalee na yy anakaa tu kwasbb anajua unaweza.
Hii tamaduni ilianzia maeneo ya pwani hasa kwa wazaramo ndio ilikuwa tabia yao yaani mtu mzima bado anaishi kwao hana kazi yoyote, anaenda kuzalisha huko alafu mke na mtoto analeta nyumbani wazazi wake ndio wanalea

Wengine walikuwa wanakimbilia mjini wanacheza rafu wanazalisha wanawake alafu wanawapandisha kwenye mabasi kuwapeleka vijijini kwa wazee wao kwa kisingizio cha maisha magumu

Lakini sasa imekuwa ni rasmi wakuu kila sehemu hapa tz vijana wanatesa wazazi wao, vijana tumeshindwa kuwaonea huruma waliotulea, badala ya kuwasaidia waliotulea sisi ndio tunazidi kuwaongezea mizigo

Naongea hayo maana kuna jirani yangu hapa mmama wa kindengereko aliolewa na mzaramo kwa bahati mbaya mmewe alifariki wakati watoto wa dogo, ana watoto watatu, mama kajikaza kulea watoto hadi wakawa wakubwa

Mmoja wakike kazalia watoto wawili hapo hapo Nyumbani, na wengine wawili wa kiume wameleta hapo hapo nyumbani wanawake zao na watoto juu na kazi hawafanyi yani mama yao ndio anachakarika tu na biashara ndogo ndogo kulea huo mzigo.

Vijana hebu tubadilike jamani
 
Kosa ni la huyo mzazi,japo uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi ila mtoto akifika umri fulani "fyekelea mbali" ili akapate akili huko mbeleni,kuendelea kuwalea na kuwalea watoto na wake zao ni kuzidi kuwatia uvivu na kuwafanya kuona kua hayo ndio maisha yao tayari na hapo ndio wameshafika,

"Kamata huyo mwanao,mkewe na watoto wao kisha shuka nao jumla jumla kwa kuwafyeklea mbali"
Fact
 
kuna watu wamezalisha nje, wakaamua chukua watoto wakae na bibi zao (kwa kuwa aliye zaa kaolewa, kafariki, kuna mfarakano). huku akimuhudumia mama yake n mwanae kuna aibu gani hapa.

kuna wamama hawapendi wajukuu zao kukaa mbali ama kwa shida hivyo kulazimishi wahusika (watoto) wao kuleta wajukuu nyumbani.

Hii aibu muionayo ni zao la zinaa, wengi umepata watoto bila ya kutarajia na hatuna mapenzi kwa mama zao ivyo suruhisho ni kuchuka watoto kwa bibi zao.
 
Kama maisha magumu kwako wewe kijana kwa baba na mama yako ambao Ni wazee Ni rahisi kwa kiwango gani? MBONA HAMNA AIBU NYIE VI DUME WA DAR NA USWAHILINI KWA UJUMLA??
 
kuna watu wamezalisha nje, wakaamua chukua watoto wakae na bibi zao (kwa kuwa aliye zaa kaolewa, kafariki, kuna mfarakano). huku akimuhudumia mama yake n mwanae kuna aibu gani hapa.

kuna wamama hawapendi wajukuu zao kukaa mbali ama kwa shida hivyo kulazimishi wahusika (watoto) wao kuleta wajukuu nyumbani.

Hii aibu muionayo ni zao la zinaa, wengi umepata watoto bila ya kutarajia na hatuna mapenzi kwa mama zao ivyo suruhisho ni kuchuka watoto kwa bibi zao.
Tatizo SI kuleteta watoto kea mzazi na kuwahudumia tatizo Ni palee na JITU ZIMAA NA KOROKORO LAKE WANAPO BEBANA KWENDA KUISHI KWA WAZAZI WAO NA WATOTO WAO
 
mbona waarabu wanaishi hivyo na wanatushinda maisha bora, sema sie wabongo roho mbaya tu.

yaani mie kuishi kwa mzee wangu n mke wangu eti jirani imuume kweli. roho mbaya tu
 
Back
Top Bottom