nzagambadume
JF-Expert Member
- Apr 9, 2018
- 2,430
- 5,769
Kama anakuja mgeni mwanza unamuambia eti mwanza ndilo jiji la pili Tanzania atakushangaa sana,last time nilikuwepo huko 6 years ago kulikuwa na ahueni,nipo huku sasa kwa miezi kadhaa tangu mwaka jana
Ndugu zangu ambao hamjaja mwanza muda mrefu hali ya huku ni kichekesho,ngoja niseme machache tu:
-Ukiingia mwanza ile stend ya zamani imevunjwa kwa mbwembwe ikasogezwa kwa mbele yako tu kichekesho sasas,ile stendi ya zamani hakuna kinachoendelea hata tofali moja halijawekwa ingawa ni takribani miezi minne,wanadai kuna kesi utajiuliza haraka ya kuvunja ilikuwa ni nini?hapo walipohamia sasa nakuhakikishia hata stendi ya Nanjilinji ni kali kuliko huo upuuzi hapo kwanza imekuwa ni maficho ya vibaka,ni pachafu kama li mwanza lilivyo sasa hivi
_Ukifika mjini kati sasa utacheka,soko kuu lilifungwa wale wauzaji wamesambaa pale mjini hakufai narudia tena HAKUFAI,na soko lenyewe haijulikani ni kinaendelea ni kama vile hela hakuna sijui?
-Barabara ni chafu hazisafishwi ipasavyo hapo nazungumzia za lami,taa za barabarani zile za security zipo lakini haziwashwi,uende nyasaka,igoma,nyegezi umeme ukikatika usiku inasikitisha sana ni giza tororo
-Barabara za mitaani kama kwa mbunge mabula anayejifanya mzalendo ni kituko kama siyo wale vijana wanaotupiaga vi gunia vya mchanga kuziba mashimo na baadaye kuomba hela basi hata bwana mabula ile barabara ya majengo kufika kwake angeshindwa,nimeambiwa halmashauri hazina hata hela ndogondogo maana zote zinapelekwa hazina kwa matumizi ya maana kama vile kununua mandege kwa cash
MWANZA IMEDODA<IMECHOKASANA)kwa mwendo huu wa halmashauri kukosa hata hela ya kujaza magunia ya mchanga barabarani tuendelee kusubiri miujiza ila tusirudie kujivunia kwamba ni jiji la pili ni aibu sana