Mtukutu wa Nyaigela
JF-Expert Member
- Sep 4, 2018
- 6,516
- 11,037
Chinga wanapewa viburi na waomba kura waoHali siyo nzuri Mwanza. (1) machinga wamejazana mbele ya maduka hasa Barabara ya Nyerere na hakuna cha kuwafanya. Katika nchi iliyo na maendeleo lazima kuwe na mpangilio wa kila kitu ndiyo maana kuna Idara katika Halmashauri zetu inayoitwa Idara ya Mipango Miji. Machinga wanatakiwa wapewe sehemu yao maalum lakini hawaguswi na viongozi wa Jiji ukiwaeleza kuhusu machinga hawana la kufanya.
(2) Soko Kuu lilivunjwa kwa nia nzuri kabisa ya kujenga soko la kisasa lakini sasa yapata kama miezi mitano hakuna kinachoendelea. Labda kuna sababu ya maana lakini hata hivyo basi wananchi tungeelezwa juu ya ucheleweshaji huo.
(3) Serikali ione uwezekano wa kuwapa Halmashauri fedha za kutekeleza shida ndogo ndogo zinazojitokeza ili zirekebishwe mara moja.
(4) Soko ambalo wafanyabiashara wamehamia kutoka soko kuu linasikitisha. Kwa kweli ni pachafu na hasa Jumapili wafanyabiashara wanapanga bidhaa zao mpaka barabarani. Hapa Mwanza kuna tatizo. Mwanza kunihitajika Idara ya Mipango Miji ambayo haingiliwi vinginevyo kila mtu atakuwa ndiye Afisa Mipango Miji.
Hapa Tanzania na Afrika viongozi hufanya vitu ili wasinyimmwe kura.
Nakuunga mkono. mji wote umejaa chinga