Ni aibu kusema Mwanza ni jiji la pili, limechoka, linachekesha, halmashauri hazina hela

Duh, nashangaa kwamba kuna watu wanapinga juu ya ukweli uliowekwa na mtoa mada.

Mwanza, uliyojaribu kuieleza ndio ukweli, ingawa umeeleza kifupi sana. Ni janga kujaribu kulinganisha mitaa ya mjini kati na maeneo mengine, hata kwa barabara ambazo ni mahandaki na zisizopitika. Acha kwa mbunge, nyingi in majanga.
 
mwanza inajengwa na itazidi kujengwa,
Soko jipya linajengwa na routes za daladala zimebadilishwa ili kupisha ujenzi wa soko,karibu na soko daladala hazitopita tena,

Stendi mpya ya kisasa inajengwa,
Vurugu zoote za jamu ya machinga zitakoma soko likikamilika,machinga woote watawekwa kwa mpangilio mzuri ndani ya soko jipya litakapo isha,

utanuzi wa barabara ya shinyanga road kuwa 4ways utaanza mapema mwaka huu,

After 2 years Mwanza itakua levo nyingine kwa hapa bongo,
kuna miradi mikubwa ya kuboresha jiji la mwanza mingi na ya kuvutia,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAWATAFUNA,
aiseee wacha bwana,hujajibu hata suala la taa barabarani na ni muda gani zipo gizani,vipi kuhusu halmashauri kufulia,nimeshangaa jana hata lile billboard kubwa pale karibu na passion hotel limepata tangazo la sayona...hahahahaha
eti 2 years,mi naongeza na mingine mitatu hakuna kitakachofanyika,tunza hii comment.
 
aiseee wacha bwana,hujajibu hata suala la taa barabarani na ni muda gani zipo gizani,vipi kuhusu halmashauri kufulia,nimeshangaa jana hata lile billboard kubwa pale karibu na passion hotel limepata tangazo la sayona...hahahahaha
eti 2 years,mi naongeza na mingine mitatu hakuna kitakachofanyika,tunza hii comment.
basi nishafahamu,kumbe ww unataka ligi,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali siyo nzuri Mwanza. (1) machinga wamejazana mbele ya maduka hasa Barabara ya Nyerere na hakuna cha kuwafanya. Katika nchi iliyo na maendeleo lazima kuwe na mpangilio wa kila kitu ndiyo maana kuna Idara katika Halmashauri zetu inayoitwa Idara ya Mipango Miji. Machinga wanatakiwa wapewe sehemu yao maalum lakini hawaguswi na viongozi wa Jiji ukiwaeleza kuhusu machinga hawana la kufanya.

(2) Soko Kuu lilivunjwa kwa nia nzuri kabisa ya kujenga soko la kisasa lakini sasa yapata kama miezi mitano hakuna kinachoendelea. Labda kuna sababu ya maana lakini hata hivyo basi wananchi tungeelezwa juu ya ucheleweshaji huo.

(3) Serikali ione uwezekano wa kuwapa Halmashauri fedha za kutekeleza shida ndogo ndogo zinazojitokeza ili zirekebishwe mara moja.

(4) Soko ambalo wafanyabiashara wamehamia kutoka soko kuu linasikitisha. Kwa kweli ni pachafu na hasa Jumapili wafanyabiashara wanapanga bidhaa zao mpaka barabarani. Hapa Mwanza kuna tatizo. Mwanza kunihitajika Idara ya Mipango Miji ambayo haingiliwi vinginevyo kila mtu atakuwa ndiye Afisa Mipango Miji.
Tanzania hakuna miji kuna vijiji
Mkuu ni kweli Tz Hakuna miji..ni vijiji...Juzi nilipita Mwanza Kuna barabara ipo Mlango 1 Hapo karibu na Aspen hotel..Imechimbika Yaani ni shimo ukiwa na hizi gari ndogo safari yako inaweza kuishia hapo... Tafadhali Tarura fikeni hapo Aspen Mlango 1..Rekebisheni icho kipande..Siyo mpaka tupige picha na video mseme sisi siyo wazalendo na tumezuia watalii kuja kuangalia Mawe na ziwa Victoria..
 
Mleta mada acha kupanic. Mwanza bado inajengwa tatizo mnapenda kuipandisha hadhi kuliko uwezo wake,na wenyeji wameshakubaliana na hali hio ila wale mnaotaka jiji liwe la tano sijui la sita litoke kwenye mbili ndio mnaokasirika ovyo

Kila ujenzi hua unachukua muda mrefu kuanza hadi kukamilika(hapo hapo kuna wapigaji,kuna kesi za hapa na pale,pesa za mradi kuchelewa kutoka)

Umeionea ile shule kusema ni shule ya udongo hapana kwa kweli. Ungesema stend yenyewe mbaya hapo sawa ila hakuna majengo ya udongo pale. Hakunaaina kali ya vibaka wa aina uliyoitaja(kila stand ina vibaka usiku)

Uzi umejaa kashfa kuliko solutions. Kwa kifupi mkuu shida yako ni MABULA na sio madhaifu ya jiji la Mwanza

Umeshaongelea pesa kupelekwa kununua ndege hapo hapo unalaumu ujenzi kutoanza sasa wao halmashaur watoe wapi pesa wakati pesa wanakusanya kupeleka juu

Wanaokuwekea picha wanakuonyesha bado mwanza ina mazuri kama dar so usipanic na kutukana ovyo. Umeleta hoja tulia wenyeji wazifafanue vizuri badala ya kumwaga povu jiiingiii lisilo na staha
 
Ni kweli Jiji la mwanza kwa sasa limekuwa km nyumba unayotaka kuikarabati au kuipanua na kuongeza vyumba wakati bado umo ndani, utajikuta sebuleni pamejaa tope la simenti,au mchanga na vyumbani pamejaa vumbi la ukuta uliobomoka,

Kwaiyo kwa kifupi ni kwamba mji kwa sasa auko vizuri ktk swala zima la usafi na mpangilio wake umekaa vibaya kutoka na miundombinu mingi kutotumika km desturi ya siku zote, lkn yote iyo nikuweza kufanya wepesi wa namna mji utakavyoweza kujengwa upya, ndo maana mnaona Barbara km ya pamba pale sokoni imefungwa kwa route za dalala za igoma/kishiri to nyashishi kupisha ujenzi wa solo kuu.

Na kuhusu Stendi yetu ya nyegezi mda mchache ujao ujenzi pia utaanza kwa speed Kali sana,worry not.
Kuhusu barabara za mitaani km iyo ya majengo mapya kuelekea uko malitaulo na kwa mbunge mabula na zingine zote za km nyaingi to SAUT na mkolani to relini, zote zipo kwenye mpango kazi, ni vile tu kipindi ichi mvua zimekuwa nyingi sana na kusababisha uharibifu wa miundombinu mingi sana, na kuwia ngumu ukarabati kwa kila Barbara ya mtaa kwa muda muafaka,
Ebu tuwe na subira mambo mazuri ayataki haraka.
Karibuni mwanza.
 
Mkuu ni kweli Tz Hakuna miji..ni vijiji...Juzi nilipita Mwanza Kuna barabara ipo Mlango 1 Hapo karibu na Aspen hotel..Imechimbika Yaani ni shimo ukiwa na hizi gari ndogo safari yako inaweza kuishia hapo... Tafadhali Tarura fikeni hapo Aspen Mlango 1..Rekebisheni icho kipande..Siyo mpaka tupige picha na video mseme sisi siyo wazalendo na tumezuia watalii kuja kuangalia Mawe na ziwa Victoria..
Hicho kipande nakipata na nikidogo tu katika barabara... Lakini hicho kipande kisiwe sababu ya kushusha hadhi ya mji... Je mlingano wa barabara nzur na mbaya katika huo mji ukoje.
 
Ukweli tu usemwe. Mwanza inatisha kwa uchafu, barabara hazipitiki, machinga wamejaza bidhaa zao kila mahali. Mjini kati hakuna parking, soko hakuna, stendi ya mabasi hakuna.......orodha ni ndefu mno!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: ram
kama kila kitu kina chopostiwa humu ilitakiwa watu wkaulize basi kusingekuwa na posts kabisa.
Hizo pics zinaondoa ukweli gani kwamba barabara za mwanza hazifagiliwi,security lights haziwaki,barabara za mtaani ni mahandaki,stendi mpya ya mkoa ni kituko cha karne na kwamba wamachinga wame flood mjini hadi mbele ya maduka ya watu
hiyo picha ya mdau drone hapo juu ya kwanza nje ya soko sijui ilipigwa mwaka gani maana hata akienda jumapili hii ausbuhi hupati pic kama hiyo,ni vurugu na uchafu wamama wauza vitumbua hadi barabarani kwenye lami
ni vuluvulu,ndiyo maana nilianza kwa kusema mgeni akiingia mwanza leo atashangaa sana haswa ukichukuliwa lango la kuingilia ni nyegezi..hahahahahha
Nimeona hakuna majibu zaidi ya kubishana ndio maana nikakupa hizo location za ofisi maana inaonekana umepita kila kona za mji itapendeza ukapita na kwenye ofisi hizo na huenda wakati unakwenda ukakutana na story nyingine ya kujazia kwenye uzi. Hiyo usiite stand mpya kwa kuwa kimsingi hapo sio stand ni wamevamia kwa muda kama ilivyokuwa stand ya Ngangamfumuni kule Moshi wakati wanapisha stand ya sasa, pia kama ilivyo stand ya Dodoma kule Ihumwa wakisubiri stand mpya inayojengwa upande wa pili wake.

Kimsingi Mwanza ilikuwa na stand nzuri kabla ya mikoa yote (labda na Arusha) kwa ile ya Buzuruga na Tanganyika kwa enzi zile hivyo viongozi wakajisahau wakati mikoa mingine wapo busy kujenga stand mpya nzuri na muasisi ilikuwa mkoa wa Kilimanjaro mwaka 2000 ndipo na mikoa mingine ikaanza kujitutumua sasa baada ya kuona kumbe inawezekana ila wananzengo wao wakawa wame-relax mpaka juzi kati ndio wakaibuka na of course wanajenga stand 2 ambapo moja ipo Nyamgholo (kwa ajili ya gari zinazotoka uelekeo wa Musoma, Tarime na Nairobi) tayari imeanza na hiyo ya Nyegezi (kwa ajili ya gari za uelekeo wa Shy, TBR, Singida, Dom) sijui kama imeanza (angalau kwa stand tuwapigie makofi basi japokuwa hazijaanza na hata zile zilizokuwepo yaani ya Nyegezi iliyofungwa na ya Buzuruga ni mfano tosha kwamba kumbe inawezekana mji kuwa na Stand 2 kutokana na uelekeo wa Buses

Kweli panaboa lakini kama wameanza kujishitukia maana sasa hivi daladala wamezipiga pini kupita kwa baadhi ya njia ikiwa pamoja na hiyo ya sokoni ili kupisha ujenzi wa hilo soko ambapo anytime wanaanza kujenga
 
sure,m npo huku mambo c mambo ukianzia hapo makoroboi,na nahc mipango mij n ovyo ndo maana hata imesababisha juz vibanda almost 32 kuungua,nafikir halmashauri zitafute muarobain wa hawa machinga
 
Back
Top Bottom