Ni aibu kumkashifu kiongozi wa nchi yako ukiwa umejificha ugenini

Yupo jamaa mmoja hapa JF ambaye kwa muda mrefu amekuwa akikosoa Serikali akiwa mafichoni huko Marekani kwa jina la T.L.Marandu. Juzi amesikika kwenye You tube akimtukana na kumkashifu Rais wa Nchi yetu bila aibu wala adabu. Katika kauli zake alionesha kujaa chuki na kutoa tuhuma nyingi moja kwa moja kwa Rais kama mtu na siyo Taasisi.

Kumbe huyu jamaa anatukana akiwa Marekani amejificha kwa dada yake aliyeolewa huko! Ni aibu na upumbavu wa hali ya juu kumkashifu Rais kwa kile kilichodaiwa kufuta Ardhi ya Bwana fulani mroho aliyemiliki sehemu kubwa ya ardhi bila kuendeleza huku wananchi wa kawaida wakiteseka. Huyu mtu pia anatoa tuhuma ambazo hana uhakika nazo kwa kuihusisha Serikali na mauaji ya kijana mmoja wa CHADEMA (kama kweli anao ushahidi).

Alisikika akimlaumu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa kwa kile alichodai ulegevu na kutomchukulia hatua Rais. Haieleweki kama T.L.Marandu ndio hatokanyaga tena Tanzania au anadhani kuwa Serikali haiwezi kumpata kwa kuwa amejificha Nje ya Nchi?? Nina mashaka kama kweli huyu ni Mzalendo wa Nchi hii au anatumiwa na watu fulani kwa maslahi yao. Jamani Rais wa Nchi ni lazima apewe heshima yake maana tumemchagua wenyewe na anapodhalilishwa ni sawa na kudhalilisha Taifa pia. Vijana kumbukeni kuwa mdharau kwao ni mtumwa na tujifunze kuheshimu Viongozi wetu.
Anaongea ukweli ambayo wewe huwezi kusema wala kuongea huyo rais wako akifanya kosa lazima aambiwe. Hata mimi siwezi kumsifu rais kichaa ambae hafuati sheria kuna mazuri yake na mabaya yake. Hivi bila wanaomsema huyo MAGUFULI wako au bila upinzani ungelikuwa hapo ulipo ukapata hata cha kupost angalau ukapata pesa ya kwenda choo
 
Lugha yako inaonesha wewe sio raia wa Nchi hii ndio maana unasema 'Rais wako". Kama ungekuwa raia wa Nchi hii ungeheshimu Mamlaka ya Nchi. Sitabishana na raia wa Nchi jirani kuhusu masuala ya Nchi yangu kwa kuwa ni kupoteza muda. Isitoshe hao wapinzani unasema ndio wanakulisha? Eeeh hiyo mpya. Mimi hawajawahi kunipa riziki yangu hao wapinzani.
 
Yupo jamaa mmoja hapa JF ambaye kwa muda mrefu amekuwa akikosoa Serikali akiwa mafichoni huko Marekani kwa jina la T.L.Marandu. Juzi amesikika kwenye You tube akimtukana na kumkashifu Rais wa Nchi yetu bila aibu wala adabu. Katika kauli zake alionesha kujaa chuki na kutoa tuhuma nyingi moja kwa moja kwa Rais kama mtu na siyo Taasisi.

Kumbe huyu jamaa anatukana akiwa Marekani amejificha kwa dada yake aliyeolewa huko! Ni aibu na upumbavu wa hali ya juu kumkashifu Rais kwa kile kilichodaiwa kufuta Ardhi ya Bwana fulani mroho aliyemiliki sehemu kubwa ya ardhi bila kuendeleza huku wananchi wa kawaida wakiteseka. Huyu mtu pia anatoa tuhuma ambazo hana uhakika nazo kwa kuihusisha Serikali na mauaji ya kijana mmoja wa CHADEMA (kama kweli anao ushahidi).

Alisikika akimlaumu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa kwa kile alichodai ulegevu na kutomchukulia hatua Rais. Haieleweki kama T.L.Marandu ndio hatokanyaga tena Tanzania au anadhani kuwa Serikali haiwezi kumpata kwa kuwa amejificha Nje ya Nchi?? Nina mashaka kama kweli huyu ni Mzalendo wa Nchi hii au anatumiwa na watu fulani kwa maslahi yao. Jamani Rais wa Nchi ni lazima apewe heshima yake maana tumemchagua wenyewe na anapodhalilishwa ni sawa na kudhalilisha Taifa pia. Vijana kumbukeni kuwa mdharau kwao ni mtumwa na tujifunze kuheshimu Viongozi wetu.
Huko kwao ni kawaida...haki ya kidemokrasia,kumzungumzia rais sio issue...sio huku mambugani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona ka anza kupunguza kwenda public. Make akija public full kuropoka tu.

Atanyooshwa tu na T. Lissu

JPM KAMATA WEZI
 
Lugha yako inaonesha wewe sio raia wa Nchi hii ndio maana unasema 'Rais wako". Kama ungekuwa raia wa Nchi hii ungeheshimu Mamlaka ya Nchi. Sitabishana na raia wa Nchi jirani kuhusu masuala ya Nchi yangu kwa kuwa ni kupoteza muda. Isitoshe hao wapinzani unasema ndio wanakulisha? Eeeh hiyo mpya. Mimi hawajawahi kunipa riziki yangu hao wapinzani.
Ni rais wako sio rais wangu ckumjagua hivyo cwezi sema ni rais wangu. Nakuambia ukweli rais wako hafai anajazba ana hasira anavisasi. Rais hatakiwi kuwa na visasi ukisha kuwa rais unaachana na visasi hata kama ulitukanwa ukiwa balozi wa nyumba kumi. Katk dunia gani ya leo rais anasema yeye hataki wapinzani. Hata ndani mwake wanabishana na mkewe itakuwa kwa watz milioni 60 yaani wote waseme yes sir. Haipo io ndio maana tunasema rais wako ubunge, uwaziri na mpaka akawa rais bado hazijamsaidia kwasababu hajui dunia ya sasa inaelekea wapi yeye bado anafikiria mambo ya chato wakati akichunga ndama
 
IMG-20170831-WA0000.jpg
j
 
Back
Top Bottom