Ni aibu kubwa mwanasiasa kujidhalilisha kiasi hiki...

Hivi UPDP ni chama kinachomwakilisha nani hasa, kina madiwani wangapi, wabunge wangapi na kiko katika mikoa ipi hapa Tanzania?

Mikoani hakijulikani kabisa,kipo dar tu ni Magamba typ hana lolote,labda anafikiri atatoka kwa style hiyo?Mfa maji bwana.
 
UPDP yaitupia CHADEMA kombora la shutuma


Na Rabia Bakari

CHAMA cha UPDP kimekitupia shutuma Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kudai kuwa kelele zinazopigwa na chama hicho kupinga serikali ya
Rais Jakaya Kikwete, lakini kimekuwa kikipenyeza maombi ya siri ya kusaidiwa ili kujipanua.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya Bakhresa Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa UPDP, Bw. Fahmi Dovutwa alisema kuwa CHADEMA wamekuwa wakisimama na kumpinga Rais Kikwete, ambapo wamefikia hatua ya kuomba asifike mwaka 2015,

Alisema hata hivyo wamekuwa wakifanya mawasiliano ya siri na Rais Kikwete kuomba msaada wa fedha ili kuimarisha chama mfano msaada wa elimu walioomba katika jimbo linaloongozwa na mbunge wa chama hicho.


"Maombi hayo yamefanya na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Zitto Kabwe kwa niaba ya chama chake, bila shaka ameambiwa na Katibu Mkuu Bw. Wilbrod Slaa mbaye naye ameelekezwa na sekretarieti. CHADEMA hawakuishia hapo tu kwa Rais Kikwete bali wametembeza bakuli hata kwa wanaowatuhumu kuwa ni
mafisadi, wameomba na wamepewa watu hawa wanatuchezea shere,"alisema Bw. Dovutwa.

Alisema kuwa kwa matusi na kebehi zinazofanywa na CHADEMA dhidi ya Rais Kikwete bila aibu mchana, lakini ajabu wamekuwa wakizungumza na CCM usiku, na kufika mbali zaidi kwamba kwa kitendo hicho ni cha kisaliti na kama kweli CHADEMA kungekuwa na waadilifu, Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe na Dkt. Slaa wangejiengua.

Aliionya CHADEMA kujifunza kupitia chama cha FORD cha nchini Kenya, ambacho kiligawanyika baada ya kiongozi wa kutokea magazetini asubuhi Ikulu na aliyekuwa Rais wa Kenya Bw. Daniel Moi, na kuonya viongozi hao kuacha usaliti kwa wafuasi wao.

Bw. Dovutwa alitoa jukumu la amani na utulivu wa nchi kuwa mikononi mwa waandishi wa habari, na kuepuka uchochezi wa CHADEMA ambao mnamo miaka ya hamsini, vita vingi vilivyopiganwa vimetokana na mikono ya waandishi wa habari.



ivi mnajua fahim dovutwa ni kibaraka wa CCM kwani yeye anatakaje? embu tujiulize yeye anatakaje then ndio tutaelewa
 
Uhuru na Jambo Leo hayawezi kunifanya nitoe hela yangu ya ngama, ni taka taka kabisa.Huyo TOVUTI alishapoteza mvuto zamani sasa anaganga njaa tu.
 
Akipata maelekezo

mwambene%2B604.jpg
 
Ni kweli imetokea ingawa ni kama utani.Juzi vyombo mbalimbali vya habari vilitangaza kwa mbwembwe kwamba chama cha UPDP kitafanya mkutano wake wa hadhara jana katika viwanja vya bakhresa manzese.Lengo likasemwa ni kuwashukuru wapiga kura na kuimarisha chama.Ilipofika jana viwanja vilipambwa kwa maandalizi ya nguvu.Sisi wengine tukajiuliza nguvu hii ya maandalizi makubwa kwa UPDP imetoka wapi? Muda ulipowadia mkutano ukaanza na mwenyekiti wa UPDP Fahm Dovutwa akapanda jukwaani.Badala ya kutangaza sera kama walivyodai,akaanza kuporomosha matusi dhidi ya chama cha Chadema na viongozi wake.Aliongea mpaka mishipa ikamtoka huku akiomba msajili wa vyama John Tendwa akawapime akili viongozi na wanachama wa chadema.Alisema atapambana na chadema mpaka mwisho ili kulinda amani ya watanzania.Nikadhani kwa upupu ule alioongea hakuna chombo cha habari ambacho kingeripoti habari ile.Lakini asubuhi magazeti pendwa ya UHURU na JAMBA LEO yameongoza na kupamba ukurasa wa mbele kwa upupu wa Dovutwa kana kwamba hakuna habari yoyote muhimu iliyotokea jana.
Mimi nadhani ifike mahali wanasiasa uchwara wanaotukana wenzao badala ya kutangaza sera za vyama vyao wazomehe kila wanapohutubia mpaka watakapoachana na tabia zao mbaya kwa vyama vingine...

Kwani wewe nani alikwambi ukasome magazeti kama uhuru na jamboleo, hayo magazeti yanafuata mfumo wa kikomunist (Suppression of peoples conciousnes to rule them like mbumbus. Watakumbumbumbu ukiendelea kusoma magazeti hayo. Kama huna magazeti ya kusoma tafuta ya udaku afadhali kidogo utapata usingizi. Free Coucelling.:A S 103: Halafu huyo dovutwa angerudi tu CCM, labda angepata uenyekiti wa serikali za mtaa kule kijijini kwake.:smow:
 
huyo Dovutwa wa updp ana mpuuzi mwenzake anaitwa Chipaka wa Tadea wote wanatumiwa hawa nakupewa ufadhili na magamba
 
huyu jamaa anatumiwa sana n ccm......akili zae ni sawa na za nape
 
Vipi Jk bado hajamteua hata ukuu wa wilaya. Maana jamaa anaonyesha njaa imembana sana. Huyu dovutwa ni mtu wa ajabu sana hata mama yake mzazi hajui mwanae alikua anagombea chama gani.
 
na kama alivyosema kuwa cdm wapimwe akili, unaweza kuona anayestahili kupimwa akili ni nani katika hili! By the way na huyu alitaka kuwa raisi ati!!!! ....hii institution ya uraisi imeshushwa hadhi kiasi cha kutisha, nafikiri atakuwa amekuza hii picha akiwatambia "wenzake" kuwa ..."niliwahi kupiga/kuongea picha na JK". Kazi tunayo
Akipata maelekezo

mwambene%2B604.jpg
 
Crap crap crap hana jipya kwanza ana kura ngapi za urais, CCM kweli wamechoka mpaka Dovutwa sasa atawasaidia nini yeye mwenyewe kwishney sasa atatuambia nini.. crap crap
 
Mwenyekiti wa Chama cha (UPDP), Fahmi Dovutwa, amemshauri Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kuwa na utaratibu wa kuwapima akili wagombea wa vyama mbalimbali kabla ya kupewa fursa ya kugombea nafasi za kisiasa.

Amesema wanasiasa wengi nchini ndio wamekuwa vyanzo vya vurugu, uchochezi wa kuvunja amani ya nchi, na kuweka utashi wa maslahi yao wenyewe badala ya kuelimisha wananchi haki na wajibu wao.

Dovutwa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipowakilisha viongozi wa vyama vya siasa nchini katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ziara ya utalii ya Balozi wa Amani wa Universal Peace Federation (UPF), Risasi Mwaulanga.

Aliongeza kuwa wanasiasa wapimwe akili zao kutokana na mambo wanayoyafanya kuwa kinyume na taratibu za uongozi kwani wanatakiwa wawe wazalendo na watumie haiba walizonazo kwa kuwaelimisha wananchi katika masuala mbalimbali, likiwemo la kutembelea vivutio vya ndani ya nchi ili kukuza pato la nchi.

"Kama sera ya utalii nchini inavyojieleza kuwa jukumu la kuutangaza utalii na kuendeleza ni la kila Mtanzania, wanasiasa na vyama vyao wanawajibu usiokwepeka katika suala zima la kutangaza na kuendeleza vivutio na maliasili zetu za nchi," alisema Dovutwa.

Alisema wanasiasa ni sehemu ya Watanzania wengi ambao wapo katika lindi la usingizi na kukosa ufahamu kwa kuamini utalii ni maalum kwa wageni tu kitu ambacho kimezorotesha idadi ya watalii wa Kitanzania katika hifadhi za nchini.

Naye Balozi huyo wa Amani wa UPF, alisema katika ziara yake aliyoifanya Mei 8, mwaka huu katika Hifadhi za Tarangire na Manyara mkoani Arusha pamoja na Ngorongoro, aliona kasoro ambazo zinapaswa kurekebishwa kama ukosefu wa matangazo mengi na juhudi za kizalendo, ujangili na uvunaji ovyo wa rasilimali hasa misitu na nyuki.

Kasoro nyingine alisema ni kutotumia vizuri fursa zinazojitokeza kutokana na haiba ya Rais Jakaya Kikwete kukubalika katika Jumuiya za Kimataifa ikiwemo ya wanasiasa na wafanyabiashara hivyo wadau wa sekta ya utalii watumie fursa hizo kukuza pato la taifa kupitia vivutio vilivyopo.

CHANZO: NIPASHE

Ningeshauri aonyeshe mfano yeye kwanza kwa kupimwa akili pindi atakapogombea.
 
Mwenyekiti wa Chama cha (UPDP), Fahmi Dovutwa, amemshauri Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kuwa na utaratibu wa kuwapima akili wagombea wa vyama mbalimbali kabla ya kupewa fursa ya kugombea nafasi za kisiasa.

Amesema wanasiasa wengi nchini ndio wamekuwa vyanzo vya vurugu, uchochezi wa kuvunja amani ya nchi, na kuweka utashi wa maslahi yao wenyewe badala ya kuelimisha wananchi haki na wajibu wao.

The man has guts!!! Hivi si huyu huyu Dovutwa alikuwa ananadi ilani ya uchaguzi mwaka jana kuwa chama chake kikichaguliwa atajenga kiwanda cha SILAHA somewhere in Dar es Salaam? so where does he get the moral authority kusema viongozi wa kisiasa wapimwe akili? Tendwa ana utalaam gani kwa kupima watu akili? All I can say is DOVUTWA is just a pain on the wrong side of the body! sorry my french.
 
unajua dalili moja ya ukichaa ni kuwaona wanzako vichaa na wewe mzima, mi naona wangeanza na yeye. Kwenye suala la kutangaza utalii bodi ya utalii in kazi gani? Wao si ndo wako kwa kazi hiyo, mi naona yeye angeendelea kutangaza sera na itikadi za chama chake na si kuwa vuvuzela wa magamba. Asitafutie umaarufu kwa migongo ya wenzake na chama chake cha msimu ambacho kinaishia ubungo
 
Naona yeye ndo anatakiwa apimwe kichwa chake kwanza-maana alichanganya wananchi wake kipindi cha uchaguzi baada ya kujitoa na kuomba kura zake apewe jk,kama si kuwa na tatizo la kiakili ni nini huku?
 
Kwa hivo yeye alipojitowa mwaka jana alipima akili akakutwa ni wazimu ndio maana hakugombea? Sasa amepona au vipi?
 
MWAULANGA.jpg


Ndugu Risasi Mwaulanga Balozi wa Amani wa Chama cha Universal Peace Federation na kulia ni Nangasu Warema ni Mwenyekiti wa Amani Foundation isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na Amani Demokrasia Tanzania wakizungumzia amani Tanzania bila ya kutofautiana kuendeleza amani iliyopo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom