Ni aibu kubwa mwanasiasa kujidhalilisha kiasi hiki... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni aibu kubwa mwanasiasa kujidhalilisha kiasi hiki...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, May 27, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kweli imetokea ingawa ni kama utani, juzi vyombo mbalimbali vya habari vilitangaza kwa mbwembwe kwamba chama cha UPDP kitafanya mkutano wake wa hadhara jana katika viwanja vya Bakhresa Manzese.

  Lengo likasemwa ni kuwashukuru wapiga kura na kuimarisha chama.I lipofika jana viwanja vilipambwa kwa maandalizi ya nguvu. Sisi wengine tukajiuliza nguvu hii ya maandalizi makubwa kwa UPDP imetoka wapi?

  Muda ulipowadia mkutano ukaanza na mwenyekiti wa UPDP Fahm Dovutwa akapanda jukwaani. Badala ya kutangaza sera kama walivyodai, akaanza kuporomosha matusi dhidi ya chama cha CHADEMA na viongozi wake.

  Aliongea mpaka mishipa ikamtoka huku akiomba msajili wa vyama John Tendwa akawapime akili viongozi na wanachama wa CHADEMA. Alisema atapambana na CHADEMA mpaka mwisho ili kulinda amani ya watanzania.

  Nikadhani kwa upupu ule alioongea hakuna chombo cha habari ambacho kingeripoti habari ile. Lakini asubuhi magazeti pendwa ya UHURU na JAMBO LEO yameongoza na kupamba ukurasa wa mbele kwa upupu wa Dovutwa kana kwamba hakuna habari yoyote muhimu iliyotokea jana.


  Mimi nadhani ifike mahali wanasiasa uchwara wanaotukana wenzao badala ya kutangaza sera za vyama vyao wazomewe kila wanapohutubia mpaka watakapoachana na tabia zao mbaya kwa vyama vingine.
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Dovutwaaa...
   
 3. i

  issenye JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  UPDP yaitupia CHADEMA kombora la shutuma


  Na Rabia Bakari

  CHAMA cha UPDP kimekitupia shutuma Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kudai kuwa kelele zinazopigwa na chama hicho kupinga serikali ya
  Rais Jakaya Kikwete, lakini kimekuwa kikipenyeza maombi ya siri ya kusaidiwa ili kujipanua.

  Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya Bakhresa Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa UPDP, Bw. Fahmi Dovutwa alisema kuwa CHADEMA wamekuwa wakisimama na kumpinga Rais Kikwete, ambapo wamefikia hatua ya kuomba asifike mwaka 2015,

  Alisema hata hivyo wamekuwa wakifanya mawasiliano ya siri na Rais Kikwete kuomba msaada wa fedha ili kuimarisha chama mfano msaada wa elimu walioomba katika jimbo linaloongozwa na mbunge wa chama hicho.


  "Maombi hayo yamefanya na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Zitto Kabwe kwa niaba ya chama chake, bila shaka ameambiwa na Katibu Mkuu Bw. Wilbrod Slaa mbaye naye ameelekezwa na sekretarieti. CHADEMA hawakuishia hapo tu kwa Rais Kikwete bali wametembeza bakuli hata kwa wanaowatuhumu kuwa ni
  mafisadi, wameomba na wamepewa watu hawa wanatuchezea shere,"alisema Bw. Dovutwa.

  Alisema kuwa kwa matusi na kebehi zinazofanywa na CHADEMA dhidi ya Rais Kikwete bila aibu mchana, lakini ajabu wamekuwa wakizungumza na CCM usiku, na kufika mbali zaidi kwamba kwa kitendo hicho ni cha kisaliti na kama kweli CHADEMA kungekuwa na waadilifu, Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe na Dkt. Slaa wangejiengua.

  Aliionya CHADEMA kujifunza kupitia chama cha FORD cha nchini Kenya, ambacho kiligawanyika baada ya kiongozi wa kutokea magazetini asubuhi Ikulu na aliyekuwa Rais wa Kenya Bw. Daniel Moi, na kuonya viongozi hao kuacha usaliti kwa wafuasi wao.

  Bw. Dovutwa alitoa jukumu la amani na utulivu wa nchi kuwa mikononi mwa waandishi wa habari, na kuepuka uchochezi wa CHADEMA ambao mnamo miaka ya hamsini, vita vingi vilivyopiganwa vimetokana na mikono ya waandishi wa habari.
   
 4. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Fahmi Dovutwa? Not AGAIN!!!
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  magazeti ya chooni ya kikosa cha kuandika hutafuta headlines kupitia wanasiasa uchwara
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  nilidhani ni mtu mwenye akili timamu kumbe kasema chizi
   
 7. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Huyo si ametumwa?
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  updp???????????????hhahahahahahahahah:mod::mod:
   
 9. O

  Omumura JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mpuuzi na kibaraka mkubwa huyo, hana jipya!
   
 10. Pilato2006

  Pilato2006 Senior Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa anaitwa TOVUTI
   
 11. e

  emrema JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Njaa mbaya jamani binadamu wanageuza hata miili yao kuganga njaa hapa TUSISHANGAE Jina lenyewe DOV..... UNATEGEMEA NINI HAPO!
   
 12. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimesikia katoa ushauri kila anaetaka kugombea cheo cha kisiasa apimwe akili, nimebaini anatakiwa yeye asihangaike kwenda kupimwa as it seems tayari akili zake zina shida
   
 13. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  -Hivi huyu bwana ni Press Secretary wa Magamba? au ni wa Serikali?

  -Siasa za sampuli hii ya "Upinzani" ziko Tanzania tu!

  -Mwenye picha za waliohudhuria mkutano huo atuwekee tuone idadi ya "wapuuzi" wenzake.
   
 14. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msela anahangaikia sosi la wanawe,hapo katumwa walau aropoke ili apewe unga!Hv siyo yule aliyesema anawapa ccm kura zake maana jina lake lilikosewa?km ndiye unategemea nn.Huyo ubwabwa na shosti wa ccm
   
 15. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ninamshauri Tendwa aanze kupima alili ya huyo Dovutwa kwanza, wanasiasa vilaza na mamluki wa aina yake ni hatari sana kwa ustawi wa demokrasia.
   
 16. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ....mti wenye matunda mazuri ndio hupopolewa mawe!!!
   
 17. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ???????????
   
 18. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  dovutwa (tamka 'duu-vutwa) yaani anavutwa na njaa/tumbo lake!!
   
 19. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  anahitajwi apewe semina elekezi kuelezwa nini lengo mama la chama cha siasa cha upinzani PERIOD
   
 20. P

  Pagi Ong'wakabu Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njaa mbaya Mhe huyu atafanya lolote ili ale, chama cha updp ni tawi la chama cha magamba hivyo anatimiza wajibu wake vinginevyo atafutwa kwenye ulaji (bila jitihada za kutetea mafisadi hawezi kumudu maisha)
   
Loading...