Ni aibu kubwa kwa TFF kwa Simba kujiandaa mchezo wa kimataifa kwa siku 14

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Nimekuwa mdau mkubwa wa ligi mbalimbali duniani wa mpira wa miguu na ndondi na mara nyingi sana ratiba za ligi mbalimbali huwa zinakwenda vizuri sana .Mfano tu ligi ya Uingereza unaona jinsi ambavyo timu inacheza ligi kuu,kimbe cha FA Europe ligi,Champion ligi bila hata kuona ratiba ya ligi kuu ikienda vibaya.

Lakini hapa Tanzania ni aibu kwa TFF kuona timu ikijiandaa na mchezo na Nkana Red D kwa siku 14 toka walipotoka huko Bondeni.

Ni ajabu sana kwa ligi yetu hapa Tanzania kuona mpaka wiki inaisha timu zinakuwa zimecheza michezo tofauti tofauti wakati ukiangalia Ligu ya Ufaransa,Ujeruman,South Africa,Kenya,Spain n.k unaona jinsi ambavyo tiimu zimecheza michezo yao kwa uwiano sawa.

Sasa hapa kuna timu imechezo michezo 12 na timu nyingine michezo 15 ni aibu kubwa sana na huoni sababu zozote za msingi

Nini ambacho kinishindikana kufuata ratiba ya TFF,CAF na FIFA
 
Kanye mbele wewe.hivi kwani ni lazima ukipenda hii timu ya Yanga ni lazima uwe umejitoa ufahamu? Hivi umesahau wakati mnashiriki michuano ya kimataifa misimu mitatu ilyopita mlikuwa mnakuwa na viporo vya mechi karibu ya kumi kwa msimu,wakati ule mlikuwa wapi kulalamika,si mlikuwa mnafurahia majibu ya shombo aliyokuwa akiyatoa yule mjinga mwenzenu ambae sasa hivi kapewa bahashishi ya UDC baada ya kupeleka serikalini uchunguzi uliotukuka kuhusu matumizi ya madawa ya Manji na biashara zake zingine za magendo.Kaa kimya kama huna la kusema kutesa kwa zamu.
 
Elewa kinachosemwa na mtoa maada, tinaona hata ulaya , man u anaweza kucheza uefa jtano na jpili anakipiga epl,
TFF wanapaswa kubadilika
 
Sio TFF hii tu hata iliyopita ilikuwa hivi.
Kwa hili wanakosea sana hata timu husika inapoteza morali inapokosa mchezo wa karibuni kwa kungoja mechi 1 kwa wiki 2.
Hali hii kwa Afrika ipo hata baadhi ya ligi kubwa afrika kama S.Afrika,morocco n.k.
Tuache ushamba tucheze mpira.
 
Mi naomba wapewe vipolo vingi zaidi hata kumi afu huku yanga na azam washinde mechi kumi mfululizo wao wakija wapige mechi rundo mfululizo mara mkoani mara taifa mara draw mara kupoteza na kuponea chupu chupu ndio watajua raha ya vipolo
 
Kanye mbele wewe.hivi kwani ni lazima ukipenda hii timu ya Yanga ni lazima uwe umejitoa ufahamu? Hivi umesahau wakati mnashiriki michuano ya kimataifa misimu mitatu ilyopita mlikuwa mnakuwa na viporo vya mechi karibu ya kumi kwa msimu,wakati ule mlikuwa wapi kulalamika,si mlikuwa mnafurahia majibu ya shombo aliyokuwa akiyatoa yule mjinga mwenzenu ambae sasa hivi kapewa bahashishi ya UDC baada ya kupeleka serikalini uchunguzi uliotukuka kuhusu matumizi ya madawa ya Manji na biashara zake zingine za magendo.Kaa kimya kama huna la kusema kutesa kwa zamu.
Aisee mkuu leo umenifungua macho,kumbe yule aliyekuwa popoma wa Yanga Jenny Murro ndo alimchomesha Yusuph Manji?ama kweli vyura ni vyura tu,akili zao kama kaa.Kumbe walaumiane wenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mimi nilijuaa wameondolewa ligi kuu wamebakizwa ligi ya club bingwa Africa make si mabingwa

Ila kwa kweliii kila kitu tz kinawezekana
 
Nimekuwa mdau mkubwa wa ligi mbalimbali duniani wa mpira wa miguu na ndondi na mara nyingi sana ratiba za ligi mbalimbali huwa zinakwenda vizuri sana .Mfano tu ligi ya Uingereza unaona jinsi ambavyo timu inacheza ligi kuu,kimbe cha FA Europe ligi,Champion ligi bila hata kuona ratiba ya ligi kuu ikienda vibaya.

Lakini hapa Tanzania ni aibu kwa TFF kuona timu ikijiandaa na mchezo na Nkana Red D kwa siku 14 toka walipotoka huko Bondeni.

Ni ajabu sana kwa ligi yetu hapa Tanzania kuona mpaka wiki inaisha timu zinakuwa zimecheza michezo tofauti tofauti wakati ukiangalia Ligu ya Ufaransa,Ujeruman,South Africa,Kenya,Spain n.k unaona jinsi ambavyo tiimu zimecheza michezo yao kwa uwiano sawa.

Sasa hapa kuna timu imechezo michezo 12 na timu nyingine michezo 15 ni aibu kubwa sana na huoni sababu zozote za msingi

Nini ambacho kinishindikana kufuata ratiba ya TFF,CAF na FIFA
Utaratibu huu wa kipumbavu niliuanzishia Uzi mwaka juzi nikawaambia wazi TFF mnaua soka la Tanzania kwa Uzwazwa. Mkuu Tatum huu siyo ushamba ni upumbavu eti kwa kuziogopa Simba&Yanga . Upuuzi huu hauna tofauti na kipindi Fulani mechi ya Yanga Vs Simba ilinunuliwa mipira 2 mmoja wenye rangi njano na nyeusi na mwingine rangi nyeupe na nyekundu. Kila mmoja ikaamriwa uchezwe kipindi kimoja ETI kutoa haki. Hatutaki haki hizi za kifala.
 
Ligi (TPL) haina mdhamini hadi Leo huku TFF wakisema mbona hata England (EPL) nayo mdhamini hawana?
hivyo ni sawa tu

viongozi wa TFF wamebaki kupingana wao kwa wao na kuunda makundi huku wengine wakikimbilia mahakamani ili kupata haki zao ilihali wote walichaguliwa kwa njia sawa!

Mbona wiki hii EPL timu zote zitakazocheza UEFA Jumanne basi mechi zao zilichezwa Jumamosi ili wapumzike Jumapili na Jumatatu
Mfano Man utd, Liverpool, Barca n.k

Na iwapo ratiba yako ya UEFA ipo Jumatano basi walicheza Jumapili ili wapumzike Jumatatu na Jumanne
mfano Real Madrid n.k

kwa zile za Alhamisi ni kuenenda tu na ratiba ili vipolo visiwepo
Kumbe timu inaweza kupumzika masaa 48 tu wakakipiga?

Ila hiyo ya siku 14 labda timu ya Taifa na matokeo hahaha yakawa mabaya kule Lesotho

Huenda pia kuna timu ziliwahi kubebwa na ratiba kama hivi ila inabidi sasa tubadili mfumo
Kupunguza pengo la michezo iliyochezwa kati ya timu na timu regardless inashiriki michezo gani ya nje

KIKUBWA TFF UONGOZI USIONGEZEWE MUDA UPIGWE CHINI KABISA WAPEWE WATU WALIOWAHI KUCHEZA MPIRA TUACHE MAZOEA KARIA KUWA RAIS TFF BORA ANGEBAKI ALIYEPO SEGEREA
 
Huu utaratibu sio kwa Tanzania tu ni nchi nyingi za Africa zina utaratibu huu wa kihuni Al Ahly ya Egypt mpaka anamaliza kucheza Fainali walikuwa na vigoro vya mechi 11
 
Mbona mna stress kwa ligi hii ya bure? Sijawahi kuona mtu anafanya kazi asiyokuwa na uhakika na ujira wake, tukipata taarifa kuwa mdhamini kapatikana utaona kasi tutakayo kuja nayo.
 
Kanye mbele wewe.hivi kwani ni lazima ukipenda hii timu ya Yanga ni lazima uwe umejitoa ufahamu? Hivi umesahau wakati mnashiriki michuano ya kimataifa misimu mitatu ilyopita mlikuwa mnakuwa na viporo vya mechi karibu ya kumi kwa msimu,wakati ule mlikuwa wapi kulalamika,si mlikuwa mnafurahia majibu ya shombo aliyokuwa akiyatoa yule mjinga mwenzenu ambae sasa hivi kapewa bahashishi ya UDC baada ya kupeleka serikalini uchunguzi uliotukuka kuhusu matumizi ya madawa ya Manji na biashara zake zingine za magendo.Kaa kimya kama huna la kusema kutesa kwa zamu.
Acha akili zako za kifisi wewe nyinyi pamoja na TFF yenu mliwalazimisha Yanga kucheza kwa ratiba ngumu mpaka wakapoteza ubingwa wao! Iweje lililowezekana Yanga kwa Simba iwe mwiko?
 
Utaratibu huu wa kipumbavu niliuanzishia Uzi mwaka juzi nikawaambia wazi TFF mnaua soka la Tanzania kwa Uzwazwa. Mkuu Tatum huu siyo ushamba ni upumbavu eti kwa kuziogopa Simba&Yanga . Upuuzi huu hauna tofauti na kipindi Fulani mechi ya Yanga Vs Simba ilinunuliwa mipira 2 mmoja wenye rangi njano na nyeusi na mwingine rangi nyeupe na nyekundu. Kila mmoja ikaamriwa uchezwe kipindi kimoja ETI kutoa haki. Hatutaki haki hizi za kifala.
Nakubaliana na wewe kabisa...soka letu haliwezi kukua kabisa kwa utamaduni na desturi hizi zikiendelea.
 
Huu utaratibu sio kwa Tanzania tu ni nchi nyingi za Africa zina utaratibu huu wa kihuni Al Ahly ya Egypt mpaka anamaliza kucheza Fainali walikuwa na vigoro vya mechi 11
pamoja na kama kuna sehemu nyingine za africa zinafanya hivyo huo ni ujinga uliopitiliza husaidii kukua kwa soka.
 
Back
Top Bottom