Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,086
- 4,879
Hakika haiingi akilini kuona viongozi wa CCM ndio wako na vipaza sauti wakipinga Upatikanaji Wa Katiba Mpya kwa kisingizio cha tunajenga uchumi na eti Wananchi wanataka Elimu Maji na MaDawa
ujenzi wa uchumi ni Mchakato endelevu toka awamu ya 1 mpaka mwisho wa dunia Ujenzi wa UCHUMI hautakoma.
Pili huduma za Elimu,Maji na Madawa ni endelevu toka mkoloni alikuwa Anazitoa na Zitaendelewa kutolewa mpaka mwisho wa dunua kwa hiyo hakuna wakati zitakoma kwa hiyo viongozi kujikita kwenye hoja hizi ni hoja dhaifu sana.
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCCM ndiye aliyesema kuna haja ya kuwa na katiba mpya kwani miaka 50 ya Katiba iliyopo imepitwa na WAKATI kutokana na mabadiliko mengi yaliyotokea Tanzania na duniani na pia katiba iliyopo haikuwashirikisha wananchi pamoja na kuanzisha huo mchakato aliendelea kujenga uchumi na kuwapatia Wananchi huduma za Elimu Maji na Madawa kwa sababu ni huduma endelevu
Viongozi Acheni kutoa hoja nyepesi nyepesi kwenye jambo zito
Kumbukeni wabunge wa Bunge la Katiba Wamelipwa posho lakini kazi hawajakamilisha wana deni la katiba mpya
Katiba ni ya wananchi tunaihitaji