Ni aibu kubwa kwa CCM kujipongeza na kujifu kwa matokeo ya uchaguzi huu mdogo

Ndaki19

Senior Member
Mar 2, 2015
134
105
Inasikitisha kuona na kusikia makada wa chama tawala ccm wakipongezana kwa matokeo waliyoyapata ktk kata mbalimbali zilizofanya uchaguzi huu mdogo, huku wakiwakejeli wapinzani bila kujali uvunjwaji wa haki za binadamu pamoja na ukandamizaji wa demokrasia ktk uchaguzi huu.

Toka nikiwa kijana mdogo nimekuwa nikiwasikia wapinzani wakilalama juu ya hujuma wanazofanyiwa na ccm ktk chaguzi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuvurugiwa mikutano ya kampeni zao, kuibiwa kura, unyanyasaji na vitisho(kwa kutumia vyombo vya dola vilivyo chini ya serikali ya chama chao), lakini yote yalipita naa maisha yakaendelea huku yakiacha makovu, maumivu na kumbukumbu mbaya kwa baadhi ya familia kwa kuwapoteza ndugu zao.

Haya yanayotokea leo kwny chaguzi hizi ni matokeo ya malezi mabaya ya siasa chafu zilizoanza kufanywa miaka kadhaa nyuma na sasa zimekomaa kiasi cha ccm kufikia hatua ya ata kutoa uhai wa watanzania wasiokiunga mkono chama chao ilhali wapate matokeo wanayoyataka wao, na ktk kuonyesha ni mkakati wa chama na serikali ktk haya yanayoendelea si mwenyekiti wa katibu wa chama aliyeinua kinywa chake kukemea hali mbaya iliyokuwa inajitokeza wakati wa kampeni na hata kwenye upigaji kura wenyewe.

Tumesikia kauli za uchochezi na zenye kuhatarisha usalama wa raia na taifa kwa ujumla kutoka kwa makada waandamizi ndani ya chama ajabu ni kwamba hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na jeshi la polisi dhidi ya matamshi hayo kwa wahusika hii ni picha halisi kuwa serikali iliyo chini ya mwamvuli wa ccm ilipanga na ilikusudia kushinda uchaguzi huu kwa njia yoyote ile, nasema hivyo kwa kutizama mlolongo mrefu wa kamatakamata ya viongozi wa vyama vya upinzani uliojitokeza karibu maeneo yote palipofanyika uchaguzi huu, vitishio kwa wagombea, uvunjwaji wa maksudi wa sheria za uchaguzi na mambo kadha wa kadha..

Ni kweli ccm wanapaswa kujipongeza kwa matokeo haya yaliyojaa kila aina ya hila, unafiki na kujipendekeza ila wakumbuke kuwa maisha yanakwenda kasi sana, km sio leo basi ni kesho.... Kasi ya watanzania kujitambua na kutambua aina ya siasa na wanasiasa wanaowahitaji ni kubwa sana na ndi maana leo wanatumia nguvu kubwa kuendelea kujitengenezea himaya yao.... Hila, unafiki, vitisho, na mambo mengine mengi yanayoendelea ndani ya ccm na serikali hakika havitakiacha chama salama ktk kipindi kifupi kijacho na wakati mkifanya maovu yenu leo mnapaswa mkumbuke ipo siku ccm pia kitakua chama cha upinzani.

Dhambi mbaya ya ubaguzi mnayotuonyesha watanzania sasa haki haitawaacha salama.... Poleni watanzania wote ambao kwa namna moja ama nyingine uchaguzi huu utakua umeacha maumivu, majeraha, na kila aina ya matatizo ktk familia zenu.... Mwenyezi Mungu awatie nguvu na aminini ipo siku haya yote ni sehemu ya harakati kuelekea kupata uhuru wa kweli.

Mungu ibariki Tanzania
7aafeb855f05e392f4a72ed6b71cfc4a.jpg
FB_IMG_1458320580959.jpg
 
Wanaojisifu kwa ushindi wa kulazimisha wa ccm. Ni mateka wa kifikra. Mateka wa kifikra ni yule anayejiaminisha jambo ambalo nafsini mwake anajuwa kuwa sio kweli.
 
Ni uchaguzi ambao umeonesha kuwa CCM bila hawa wapuuzi police ni bureee
 
Back
Top Bottom