Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,508
- 23,710
Huwa najiuliza hizi ziara za kushtukiza lengo lake huwa ni kugundua nini? Unaweza shtukiza shambani kujua kama uliowapa kazi ya kulima wanalima au wamelala chini ya vivuli.
Kinyume na hapo dunia ya leo haina wavivu wa namna hiyo au wafujaji wa namna hiyo, ina watu ambao wapo kazini lakini si efficient au ni wezi. Hawa huwezi wagundua kwa kushtukiza kuwa ukienda kwa kunyata utamkuta amebeba container analificha nyuma ya ofisi.
Au ukienda Hosp utakuta Dr. Amelala ofisini wagonjwa wapo kwenye mstari. Hapo unamshtukiza. Kwa level ya Rais mi huwa sioni wanachoshtukiza katika ziara zao. Msafara wa Rais ni mkubwa sana.
Lakini pia Rais ana mikono mirefu anaweza fanya uchunguzi wake bila kwenda kwa kunyata sehemu. Kwenda sehemu na kuuliza maswali kwa ukali, kufoka na kutoa macho haioneshi kuwa hapo Rais umefanya kazi kubwa sana.
Tuacheni usanii wanasiasa hasa wa Afrika. Tufikie hatua mtuheshimu na sisi Wananchi wenu. Kwa nini kila wakati mnatuona kama ni watoto wadogo sana? Please tuheshimiane. Usanii hautusaidii katika maendeleo.