Ni Afadhali Elimu kufundishwa kwa Kiswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Afadhali Elimu kufundishwa kwa Kiswahili

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Muacici, Nov 6, 2009.

 1. Muacici

  Muacici JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ifuatayo ni barua ya kweli ya kuomba kazi iliyotumwa kwa mkurugenzi wa kampuni binafsi. Kwamba kijana wa Kitanzania amekaa chini na kuandika barua hiyo. Nahofia, kwa kasi hii ya shule za kata zisizo na uhakika wa walimu bora, itafika mahali tutakuja kuiona barua hiyo hapo juu ina afadhali. Na ni vijana hawa wenye ndoto za kuja kuwa waheshimiwa siku chache zijazo. Tunahitaji msaada na hekima ya Mungu, la sivyo bora elimu ifundishwe kwa kiswahili tujue English imetushinda. Mnasemaje wana jamii, maana tunaelekea katika EAC??

  JOB APPLICATION

  I am apply to my job of security guard to you boss in you company of Shoprite. I complete to Grade 8 examination certificate in 1997. I am 27 ears to be Born of age and no mallied and no childish. My father is dead long time ago and my mother mary in Zaire country there 10 years now, no see she so nobody known to help me. My certificate is just sitting home for itself, but passes in Mathematics, Geography, Science and all subjects but fail in English because of Nyanja teacher, Mr Phiri, teaching me is jelos of myself. Me wear expenses cloth than Ngoni teacher. I here people you want security guards to you company and I tell you I Am one of that job experience for 2 years. I shot thief dead. I want to Join the company of you and chase criminal out with me AK47. Please consider my aplication careful and call me any time because me Have celphone. I am red for interview with you. I am very hornest and can speak English free.
  Yours in faith
  P. M.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,433
  Trophy Points: 280
  Jamaa ana masikio mangapi??ahahah
   
 3. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ukiona raisi wa nchi, Kikwete, hawezi kujieleza kwa kiingereza mbele ya vyombo vya habari ujue kuwa nchi yetu iko matatani.

  Lakini baya zaidi ni kuona kuwa hakuna hatua yeyote inayochukuliwa ili kuwezesha wahitimu wetu kumudu ushindani wa soko huria.

  Mbona wakuu wanapeleka watoto wao kusoma Uganda, Kenya, UK, US n.k. na sio kubanana na wengine hapo nyumbani kama elimu yetu ni nzuri?
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nakuunga mkono, ifuatayo ni nukuu kuhusu hilo kutoka kwenye utafiti kuhusu Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba (PSLE):

  In 2006, 70.7% percent of the children passed PSLE, meaning that these children were competent to enrol in and benefit from secondary education. Yet, only 48.0 percent of the children passed the English paper. This means at least 22.7 percent of the children are eligible to enrol in secondary schools even though they failed English, the language of instruction in secondary
   
 5. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #5
  Nov 6, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wanaziandika hizi barua,halafu,there is no conciousness on their part that they are doing anything wrong. Utaona hawa watu wanaandika hizi barua kuomba admission in foreign Universities.
  Hiyo barua uliyoiandika hapo sijui kama ni ya kweli au wewe umeitunga. Kwa sababu kwa jinsi nilivyoona mimi,hawa wanaoandika barua hizi,hawafanyi makosa yoyote per se,it is just what in linguistics is called ''mother tongue interference'',it is just a completely new type of english.
   
 6. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2009
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Mimi nitakubaliana na hoja ya kufundisha kiswahili mashuleni katika nyanja ifuatayo... kingereza kimekuwa ni lugha ya biashara na mawasiliano kwa ujumla duniani.. lakini utaona kuwa nchi zilizoendelea ziekuwa katika jitihada kubwa katika kuhakikisha lugha zao zinaipiku kingereza... na katika kuthibitisha hilo utaona hata katika maswala ya ajira .. ikiwa ni kampuni ya kichina au kifaransa au kijerumani basi utaona wameongeza ki sehem cha ambacho kitakufavour ikiwa tu unajua lugha ambayo kampuni hiyo wamiliki wake wanatoka... i doesnt make sense kampuni ina branch tz lakini bado wakitangaza ajira (ni lazima watoe ajira kwa wa tz ikiwa ni kutimiza moja ya masharti ya uwekezaji) utaona wameongeza kipengele hicho.. badala ya wao kujifunza lugha yetu ili kurahisisha utendaji kazi wanataka tujifunze ya kwao... lakini utaona wenzetu huko kwao swala la mtu kutojua kingereza ITS NOT A BID DEAL...yaani halitakunyima fursa yoyote ile.. sa kwa nini tukiendekeze..

  NB: tumeshakuwa waathirika wakubwa na kwasababu sisi ni mataifa tunayoitwa yanayoendelea a.k.a third world countries.. na kwa takwimu za juu juu more than 60% ya uchumi wetu na maendeleao yanategemea nje.. hatuna budi kuijua lugha zao..at leat to keep at pace with wat their r doing.. sss tutajifunza lugha ngapi ikiwa kila taia kubwa likija kussuport linataka tujifunze ya kwake.. na v kuhusu lugha yetu

  Na kwababhati mungu alivyotubariki sisi ni waasisi wa kiswahili ambacho kinapigiwa debe duniani.. lakini cha ajabu hao wakenya ambao kiasili sio cha kwao wanatengeneza fedha kupitia hicho kiswahili.. na cha kusikitisha wnaakiharibu zaidi..
  nana sisi tunakionea aibu

  OOOh nisiongee sana ninaweza nikajikuta nalia.. cha msingi mimi sina uzoefu katika maswala haya ya public relations na blah blah zingine ila naamini serikali inaweza ikachukua hatua za makusudi kwa kuita wataalam wake na hata na wa nje wakaweka mfumo ambao utakiinua kiswahili na papo hapo utawalinda na kuwasaidia wa tz katika mahusiano ya kibiashara na kazi na wageni.. huku kukiwa na njia na juhudi mbadala kuhakikisha pia wanajua hicho kingereza... yaani mkakati uwe vitu hv viende sambamba

  nimeshakutanan na wageni kibao katika maswalal ya kikazi.. hawajui kingereza zaidi ya lugha yao na wamekuja hapa kuwakilisha kampuni zao na nchi zao.. wanatoka german fance portugal..
  KHE JAMANI HV HII NCHI NI KWELI KIJOGRAFIA TULIPASWA KUISHI HUKU AU HILI ENEO LILIKUWA LIMETENGWA KWA AJILI YA WANYAMA AU PROJECT..pengine ni HII TZ NI ENEO LA MAKABURI HAIWEZEKANI SISI KILA KITU TUNAFANYA KWA KUBAHATISHA NA PASIPO NA SULUHISHO SAHIHI kila kitu mpaka tuathirike ndio tuombe msaada nje wa kututatulia sio tutatue wenyewe..

  JAMANI NISAMEHENI KWA LUGHA NILIZOTUMIA ILA NAHISI KUNA UMUHIMU WA KUJICHUKULIA RB UNAWEZA UKAJIKUTA UNAUA PASIPO KUKUSUDIA. kwa haya yanayotokea hapa tz.

  ******************************************
  ni bora ukakaa kimya watu wakakuhisi ni mpumbavu kuliko ukafungua mdomo wako na kuwahakikishia kuwa kweli wewe ni mpumbavu
   
Loading...