NHIF watolea ufafanuzi madai ya Wananchi wa Mwanza yaliyowekwa JamiiForums. Kuchukua hatua

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetolea ufafanuzi malalamiko ya wadau wake mkoani Mwanza.

Watoa huduma wamekumbushwa kuzingatia miongozo na mkataba kati yao na mfuko. Kikao kitaitishwa ili kulipatia ufumbuzi suala hili.

Kwa hili, huu ndo uwajibikaji kwa vitendo. Hongera NHIF kwa kutoshupaza shingo.

IMG_3212.jpg

Majibu haya yamekuja kufuatia kuibuka kwa mjadala huu > NHIF matatani, kilio cha wamiliki wa hospitali binafsi kukatwa mabilioni ya fedha chaibuka
 
Hii dawa mkoa wa mwanza inauzwa Tsh 12,000 bei ya reja reja. Dawa hiyo hiyo mkoa wa arusha na Kilimanjaro inauzwa Tsh 3,000 bei ya reja reja. Jamani Bima ya Afya ni JIPU. Mungu anawaona.
Aaiseee, kama hii ni kweli, basi mkuu 'peno hasegawa' umetoa mchango wenye ushahidi mzuri sana.
Ni juu ya wahusika kuufanyia kazi ushahidi huo na kuchukua hatua stahiki.

Michango ya aina hii ndio inayokosekana sana hapa jamvini. Tumebaki tu na mipasho isiyo na manufaa.
 
Kule Kibo pharmacy,iliyopo mkoa wa Kilimanjaro dawa hiyo ni Tsh 3,000 .Hapa mkoa wa mwanza Tsh 12,000 ukiuliza kwanini bei. Ni juu zaidi wanakujibu hapa kazi tu. Namba ya Kibo pharmacy 0684 482 841 kwa ushahidi zaidi.
Eeenh, una maana hao wa Mwanza ndio wanaoamini zaidi 'philosophy' ya "Hapa ni Kazi Tu"!
Tuwape pongezi zao za kutimiza wito waliopewa na mwasisi wake.
 
Kule Kibo pharmacy,iliyopo mkoa wa Kilimanjaro dawa hiyo ni Tsh 3,000 .Hapa mkoa wa mwanza Tsh 12,000 ukiuliza kwanini bei. Ni juu zaidi wanakujibu hapa kazi tu. Namba ya Kibo pharmacy 0684 482 841 kwa ushahidi zaidi.
Je, inawezekana ni dawa hiyo hiyo lakini brand tofauti? Najaribu kuangalia kwa angle zote tu na sikupingi au kuwatetea wahusika. Nasema hivi kwa sababu baadhi ya dawa bei zinatofautiana sana japo ni dawa zile zile kutokana na manufacturer. Kwa mfano kuna hizi ''generic brand'' mara nyingi bei zake ziko chini kabisa kulinganisha na ''brand name''.
 
Mfuko wa Taaida wa Bima ya Afya (NHIF) umetolea ufafanuzi malalamiko ya wadau wake mkoani Mwanza.

Watoa huduma wamekumbushwa kuzingatia miongozo na mkataba kati yao na mfuko. Kikao kitaitishwa ili kulipatia ufumbuzi suala hili.

Kwa hili, huu ndo uwajibikaji kwa vitendo. Hongera NHIF kwa kutoshupaza shingo.

View attachment 1637352

Majibu haya yamekuja kufuatia kuibuka kwa mjadala huu > NHIF matatani, kilio cha wamiliki wa hospitali binafsi kukatwa mabilioni ya fedha chaibuka
NHIF hawajawahi kusema ukweli mkuu , si wa kuwaamini na wala hawajawahi kuaminika , sipendi kufunguka zaidi kwa sababu maalum , lakini nakuomba ufuatilie hicho kikao na wadau kwanza sidhani kama kitafanyika na hata kikifanyika usikie kitakachojiri .
 
Hii dawa mkoa wa mwanza inauzwa Tsh 12,000 bei ya reja reja. Dawa hiyo hiyo mkoa wa arusha na Kilimanjaro inauzwa Tsh 3,000 bei ya reja reja. Jamani Bima ya Afya ni JIPU. Mungu anawaona.
Emdelyn local made kutoka Mansoor Daya hata kwa uchawi haiwezi kuuzwa elfu 12 , na wala hakuna hata duka linaloweza kuiuza hata zaidi ya elfu 4
 
Back
Top Bottom