msani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 1,801
- 1,191
Sizingumzii gharama kwa sababu wote hatulingani na serikali kupitia wakala wake NHIF wameamua hivyo lakini naomba niseme kuhusu ulaghai huu ambao wanawafanyia Watanzania.
Mimi kulingana na uwezo mdogo sana, gharama za Bima ya Afya nililipia zile za watoto tu za Shilingi 50,400 kwa mwaka, huu ulikuwa unaingia mwaka wa 3 sasa nikitumia huduma hizo. Sasa mwezi huo kadi hizi zilikuwa zinaisha muda wake tukaenda kufanya RENEW za hizo kadi kwenye tarehe 20 hivi Novemba. Pale ofisi za Kinondoni jengo karibu na Mawasiliano.
Tulifanya taratibu zote za kujaza fomu na kulipia na kukabidhi kadi ambazo zilikuwa zimekaribia kuisha.
Tuliambiwa tuzifuate baada ya siku 9 za kazi, ila hatukipata hadi leo (2 Jan 2020) ndio tumeenda na kukuta ziko lakini jambo la kushangaza ni kwamba zimeandikwa tarehe za kuanza kutumika ni 24 Februari 2020. Je, huu sio ulaghai kwa wananchi?
Kwanini serikali inafanya namna hii? Je, ni kukwepa kuwahudumia wananchi wake?
Tukumbuke kwamba lengo la Bima ya Afya kwa watoto ilikuwa ni kuendana na malengo ya MDGs ya kupunguza vifo vya watoto, na malengo ya serikali ya kuhakikisha watoto wanapata matibabu lakini kinachofanywa na serikali kwa sasa ni aidha kutoa maelekezo ya siri kwa namna ya kukata au kupunguza huduma hizi kwa watoto kwa siri na kwakutumia mbinu ya 'WAGAWE UWATAWALE'.
Hii ni kwa sababu ukifika kufanya RENEW ya kadi utaambiwa kwamba huduma zitaendelea lakini ukienda kuchukua kadi unakuta huduma imesimamishwa na kusogezwa mbele kwa miezi mitatu (siku 90) na kwa kuwa umepewa kadi muda huo na hawana muda wa kukusikiliza watakughasi na utaondoka kwakuwa hauna la kufanya.
Huu ni mpango ovu kwa serikali hii ya Tanzania kwa watu wake.
Labda niliweke hili wazi kwamba watanzania wengi ambao wanatumia BIMA YA AFYA has NHIF ni wale ambao sheria inawalazimisha lakini wengi ambao sheria haiwalazimishi wanakata kwa ajili ya watoto wao tu kwa sababu ya hali za kiuchumi na gharama hizo kuwa kubwa na kwamba zinapaswa kulipwa kwa mkupuo mmoja.
Naamini hata hawawafanyakazi wanaolazimishwa sheria wangeambiwa walipe kwa mkupuo mmoja bila kulazimishwa basi NHIF isingekuwa na wateja.
Ni ngumu sana kwa maisha yetu hasa watu kama mimi kuniambia nilipe TZS 1.5M kwa mkupuo mmoja kama Bima ya AFYA nikaweza. Mwisho wa siku tunaendelea kumuomba Mungu tu atuweke salama na hata ukiugua basi utameza panadol na mseto ili upone na wakati mwignine bila hata kupima na sio kwamba tunapenda ila ni hali za maisha.
Watanzania wengi hatuwezi jamani hizi gharama, haiwezekani kabisaaaa.
Najua hamjali kwa sababu nyie mnatibiwa kwa kodi hata tunayolipa sisi hamuwezi kuelewa hiki nasema hapa.
Kuanzia rais hadi mawaziri,makatibu hadi wafanyakazi wa NHIF hamuwezi kuelewa haya, labda siku moja tubadilihane maisha.
Mungu ninakuomba endelea kunilinda mimi na watanzania wenzangu wote ambao wenye mamlaka wameamua kututenga ila kwenye kura wanakuja kwetu