NHIF Wanaulaghai umma wa Watanzania?

msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,801
1,191
Sizingumzii gharama kwa sababu wote hatulingani na serikali kupitia wakala wake NHIF wameamua hivyo lakini naomba niseme kuhusu ulaghai huu ambao wanawafanyia Watanzania.

Mimi kulingana na uwezo mdogo sana, gharama za Bima ya Afya nililipia zile za watoto tu za Shilingi 50,400 kwa mwaka, huu ulikuwa unaingia mwaka wa 3 sasa nikitumia huduma hizo. Sasa mwezi huo kadi hizi zilikuwa zinaisha muda wake tukaenda kufanya RENEW za hizo kadi kwenye tarehe 20 hivi Novemba. Pale ofisi za Kinondoni jengo karibu na Mawasiliano.

Tulifanya taratibu zote za kujaza fomu na kulipia na kukabidhi kadi ambazo zilikuwa zimekaribia kuisha.

Tuliambiwa tuzifuate baada ya siku 9 za kazi, ila hatukipata hadi leo (2 Jan 2020) ndio tumeenda na kukuta ziko lakini jambo la kushangaza ni kwamba zimeandikwa tarehe za kuanza kutumika ni 24 Februari 2020. Je, huu sio ulaghai kwa wananchi?

Kwanini serikali inafanya namna hii? Je, ni kukwepa kuwahudumia wananchi wake?

Tukumbuke kwamba lengo la Bima ya Afya kwa watoto ilikuwa ni kuendana na malengo ya MDGs ya kupunguza vifo vya watoto, na malengo ya serikali ya kuhakikisha watoto wanapata matibabu lakini kinachofanywa na serikali kwa sasa ni aidha kutoa maelekezo ya siri kwa namna ya kukata au kupunguza huduma hizi kwa watoto kwa siri na kwakutumia mbinu ya 'WAGAWE UWATAWALE'.

Hii ni kwa sababu ukifika kufanya RENEW ya kadi utaambiwa kwamba huduma zitaendelea lakini ukienda kuchukua kadi unakuta huduma imesimamishwa na kusogezwa mbele kwa miezi mitatu (siku 90) na kwa kuwa umepewa kadi muda huo na hawana muda wa kukusikiliza watakughasi na utaondoka kwakuwa hauna la kufanya.

Huu ni mpango ovu kwa serikali hii ya Tanzania kwa watu wake.

Labda niliweke hili wazi kwamba watanzania wengi ambao wanatumia BIMA YA AFYA has NHIF ni wale ambao sheria inawalazimisha lakini wengi ambao sheria haiwalazimishi wanakata kwa ajili ya watoto wao tu kwa sababu ya hali za kiuchumi na gharama hizo kuwa kubwa na kwamba zinapaswa kulipwa kwa mkupuo mmoja.

Naamini hata hawawafanyakazi wanaolazimishwa sheria wangeambiwa walipe kwa mkupuo mmoja bila kulazimishwa basi NHIF isingekuwa na wateja.

Ni ngumu sana kwa maisha yetu hasa watu kama mimi kuniambia nilipe TZS 1.5M kwa mkupuo mmoja kama Bima ya AFYA nikaweza. Mwisho wa siku tunaendelea kumuomba Mungu tu atuweke salama na hata ukiugua basi utameza panadol na mseto ili upone na wakati mwignine bila hata kupima na sio kwamba tunapenda ila ni hali za maisha.

Watanzania wengi hatuwezi jamani hizi gharama, haiwezekani kabisaaaa.

Najua hamjali kwa sababu nyie mnatibiwa kwa kodi hata tunayolipa sisi hamuwezi kuelewa hiki nasema hapa.

Kuanzia rais hadi mawaziri,makatibu hadi wafanyakazi wa NHIF hamuwezi kuelewa haya, labda siku moja tubadilihane maisha.

Mungu ninakuomba endelea kunilinda mimi na watanzania wenzangu wote ambao wenye mamlaka wameamua kututenga ila kwenye kura wanakuja kwetu
 
Eka na hio picha tuone hio tarehe husika iliyowekwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitaangalia namna ya kufanya kuweka picha ila simu yangu uwezo mdogo wa kufanya editing ili isilete shida kwa watoto wangu na mimi kwa sababu kwa sasa uhuru tunao JF pekee na sio nje ya hapo. Ila nilichoandika ni kweli kabisa labda kama kuna mwingine atakuja kuthibitisha hili.
 
Kipimo cha widal test kwa ajili ya kupima typhoid na dawa za dufaston wameondoa kwenye huduma. Hawa jamaa ni wa ajabu sana. Sijui mfuko ulikuwa unaelekea kuanguka au ni vip

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipimo cha widal test kwa ajili ya kupima typhoid na dawa za dufaston wameondoa kwenye huduma. Hawa jamaa ni wa ajabu sana. Sijui mfuko ulikuwa unaelekea kuanguka au ni vip

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ni eneo lingine ambalo sijaliongelea kwa sababu sijakumbana nalo ila nimesikia pia kupunguza huduma baadhi za matibabu na haya yanafanyika kwa sababu wengi wanaotumia huduma TOTO AFYA ni watu duni wenye kipato cha chini wasio na uwezo wa kufuatilia kwahiyo unaweza kuwa na kadi ya bima ya afya NHIF ila ni kwa ajili ya matibabu ya malaria tu
 
Sizingumzii gharama kwa sababu wote hatulingani na serikali kupitia wakala wake NHIF wameamua hivyo lakini naomba niseme kuhusu ulaghai huu ambao wanawafanyia Watanzania.

Mimi kulingana na uwezo mdogo sana, gharama za Bima ya Afya nililipia zile za watoto tu za Shilingi 50,400 kwa mwaka, huu ulikuwa unaingia mwaka wa 3 sasa nikitumia huduma hizo. Sasa mwezi huo kadi hizi zilikuwa zinaisha muda wake tukaenda kufanya RENEW za hizo kadi kwenye tarehe 20 hivi Novemba. Pale ofisi za Kinondoni jengo karibu na Mawasiliano.

Tulifanya taratibu zote za kujaza fomu na kulipia na kukabidhi kadi ambazo zilikuwa zimekaribia kuisha.

Tuliambiwa tuzifuate baada ya siku 9 za kazi, ila hatukipata hadi leo (2 Jan 2020) ndio tumeenda na kukuta ziko lakini jambo la kushangaza ni kwamba zimeandikwa tarehe za kuanza kutumika ni 24 Februari 2020. Je, huu sio ulaghai kwa wananchi?

Kwanini serikali inafanya namna hii? Je, ni kukwepa kuwahudumia wananchi wake?

Tukumbuke kwamba lengo la Bima ya Afya kwa watoto ilikuwa ni kuendana na malengo ya MDGs ya kupunguza vifo vya watoto, na malengo ya serikali ya kuhakikisha watoto wanapata matibabu lakini kinachofanywa na serikali kwa sasa ni aidha kutoa maelekezo ya siri kwa namna ya kukata au kupunguza huduma hizi kwa watoto kwa siri na kwakutumia mbinu ya 'WAGAWE UWATAWALE'.

Hii ni kwa sababu ukifika kufanya RENEW ya kadi utaambiwa kwamba huduma zitaendelea lakini ukienda kuchukua kadi unakuta huduma imesimamishwa na kusogezwa mbele kwa miezi mitatu (siku 90) na kwa kuwa umepewa kadi muda huo na hawana muda wa kukusikiliza watakughasi na utaondoka kwakuwa hauna la kufanya.

Huu ni mpango ovu kwa serikali hii ya Tanzania kwa watu wake.

Labda niliweke hili wazi kwamba watanzania wengi ambao wanatumia BIMA YA AFYA has NHIF ni wale ambao sheria inawalazimisha lakini wengi ambao sheria haiwalazimishi wanakata kwa ajili ya watoto wao tu kwa sababu ya hali za kiuchumi na gharama hizo kuwa kubwa na kwamba zinapaswa kulipwa kwa mkupuo mmoja.

Naamini hata hawawafanyakazi wanaolazimishwa sheria wangeambiwa walipe kwa mkupuo mmoja bila kulazimishwa basi NHIF isingekuwa na wateja.

Ni ngumu sana kwa maisha yetu hasa watu kama mimi kuniambia nilipe TZS 1.5M kwa mkupuo mmoja kama Bima ya AFYA nikaweza. Mwisho wa siku tunaendelea kumuomba Mungu tu atuweke salama na hata ukiugua basi utameza panadol na mseto ili upone na wakati mwignine bila hata kupima na sio kwamba tunapenda ila ni hali za maisha.

Watanzania wengi hatuwezi jamani hizi gharama, haiwezekani kabisaaaa.

Najua hamjali kwa sababu nyie mnatibiwa kwa kodi hata tunayolipa sisi hamuwezi kuelewa hiki nasema hapa.

Kuanzia rais hadi mawaziri,makatibu hadi wafanyakazi wa NHIF hamuwezi kuelewa haya, labda siku moja tubadilihane maisha.

Mungu ninakuomba endelea kunilinda mimi na watanzania wenzangu wote ambao wenye mamlaka wameamua kututenga ila kwenye kura wanakuja kwetu
Hallo Msani Hongera kwa majukumu.
Mimi ni mmoja wa mwanachama ambaye ninatumia Bima ya Afya ya NHIF kwa Muda mrefu na ninahudumiwa na ofisi ya Kinondoni.

Ninavyojua utaratibu wa TOTO AFYA UPO KAMA IFUATAVYO KWA SASA.
1. Garama za kupata kitambulisho cha TOTO AFYA ni TZS 50,400 kwa mwaka
2. Mtoto anayekatiwa Bima ya Afya akiwa mmoja mmoja kwa mara ya kwanza lazima asubiri kwa muda wa siku 90 ndo kuanza huduma na hizi siku zinafidiwa kwenye kadi yake mbele.
3. Mfuko unatoa kadi yenye muda wa matumizi miaka mitano (5) lakini mwanachama anatakiwa kulipia michango kila mwaka ili aweze kupata huduma.
4. Mwanachama wa TOTO AFYA KADI anatakiwa KUHUISHA Uanachama wake ndani ya siku 30 baada ya kukoma uanachama . Endapo mwanachama atashindwa kuhuisha uanachama wake ndani ya kipindi tajwa atalazimika kuanza upya na taratibu za kujiunga na ataingia kwenye sharti number 2 hapo juu
5. Watoto ambao wanajiunga na Mfuko kwa utaratibu wa kupitia mashuleni kwa umoja wao hawana muda wa kusubiria huduma kwa sababu wanajiunga kwa pamoja na kwa wingi wao. HIVYO WAZAZI mnasisitizwa kuhakikisha watoto wanajiunga na bima ya afya kupitia mashule na kwa wingi wao ndo inaleta mshikamano wa kuwahudumia.

Mambo yote niliyoandika hapo yapo kwenye form ya kujiunga na kila mwanachama anayejiunga anatakiwa kusoma na kuelewa. HIVYO BWANA MSANI tunaomba kufahamu wewe ulikwama wapi haswa na je hukuchelewa kulipia kadi yako ndo maana ukaanza upya??
 
Mkuu nikuulize NHIF wako na utaratibu wa kuwapatia watu wazima bima ya kujilipia ama Ni watotot tu!??

uliyoandika andika ni kweli tupu,mi nimeshakutana nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom