NHIF tuondoleeni utaratibu huu

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Pamoja na dhamira njema ya Mh Rais Magufuli kuwekeza Bajeti kubwa kwenye Sekta ya Afya lakini bado kuna baadhi ya watendaji wanamuangusha Rais

Kwenye vifurushi vya Bima ya afya walivyonavyo NHIF kipo kifurushi cha mtoto afya ambacho watoto chini ya miaka 18 wanalipia 50.400 tu kwa mwaka

Ilikuwa ukilipia inachukua mwezi mmoja kuweza kupata Kadi ya Matibabu,

Sasa tunaona utaratibu umebadilika kutoka mwezi mmoja mpaka miezi mitatu kitu ambacho kimeleta usumbufu kwa Wananchi

Yaani mtoto amezaliwa leo inachukua miezi mitatu ndo aje apate Kadi ya Matibabu kwahiyo ikitokea ameugua kabla ya muda huo inakuwa shida na hasa kama familia haina pesa

Rai yangu kwa Waziri wa afya na Bodi nzima ya NHIF kushughulikia hili haraka na sio lazima kila kitu mpaka aje Mh Rais kutengua

Watoto ni Taifa la kesho na lazima tuonyeshe UTU kwa kuwalinda hasa wanapougua

Ni matumaini yangu NHIF watarudisha ule utaratibu wa zamani wa mwezi mmoja tu na sio huu wa miezi mitatu

Alex Fredrick
 
Mkuu Nina huwa inakatwa ili kujilinda na majanga pindi yatakapotokea...bima haikatwi ili kumtibu mtoto. So unapaswa kuchangia kwa kipindi fulani ndo update huduma..si hii mtoto amelazwa then unahaha kumtafuta bima
 
Alex Fredrick, Sera ya afya kwa Tanzania, watoto chini ya miaka mitano wanatibiwa bure hospital na vituo vyote vya tiba vinavyomilikiwa na serikali

Ushauri wangu katika kifurushi ulicholalamikia, wakiondoe kabisa kianzie watoto wa miaka mitano nakuendelea kisha watoe ruzuku kwa vituo binafsi navyo viwe na hayo matibabu bure kwa watoto chini ya miaka mitano
 
Back
Top Bottom