NHIF mnaumiza wanachama wenu

Status
Not open for further replies.
MGURUGENZI WA NHIF MULIKA WATUMISHI WA NHIF HOSPITALI YA WILAYA YA NZEGA.

- Kwanza muda mwingi hawapo kazini.Mfano, JUMAMOSI,JUMAPILI,na nyakati zs USIKU!!! Je WAGONJWA WA BINA NYAKATI HIZO HUWA HAWAUMWI?? NDIVYO MLIVYOAGANA NAO KWAMBA NYAKATI HIZO WAGONJWA WANAOTUMIA BIMA HAWAPASWI KUUMWA NA IKITOKEA WAMEUMWA NYAKATI HIZO WANAPASWA WAJIGHARAMIE MATIBABU ILIHALI WANABI A KISA MJAZAJI WA FORMU HAYUPO KAZINI?????????

-Kadi la Mgonjwa Lile gumu ,Unaambiwa kanunue dafutari dogo hapo getini kwao!!! Huo huenda ni mradi wa mtu.!!

- Dawa nyingi Unaambiwa hazipo kanunueNi wajibu wenu kuhakikisha Dawa zote zipo kwa wagonjwa wa Bima.Vinginevyo mtupage na hela za kununulia HIZO Dawa maduka ya Phamarcy.

MKURUGENZI HAKIKISHA WATUMISHI WAPO MUDA WOTE HASA NYAKATI ZA USIKU NA WIKENDI.HILI NI KEROOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Huko Hakuna mkurugenzi , mkuu wa wilaya , Mbunge ?

Kwanini msiwafuate?
 
Jana nimekua nafanya research mimi na familia tujiunge NHIF kile kifurushi cha bei ya juu kabisa. Inatakiwa km milioni moja na laki hivi. Nikacheki AAR kifurushi cha dizaini hiyo ila cha chini kidoogo ni mara mbili yake.
Sasa kuokoa cost nika make conclusion ngoja nikate NHIF ila mimi nimezoea sana kwenda Agakhan hospital. Sasa nikasema ngoja niwapigie Agakhan kuwauliza vp mnapokea wenye bima za NHIF.
Nikajutaa. Eti wenye bima za NHIF wanaopokewa hapa Agakhan ni wafanyakaz wa TRA, Benki Kuu sijui na kampuni gani nimesahau jina. Wengine wote hatupokei labda uende kwenye vile vijibranch vya Agakhan.
Nilichoka kwa kweli.
Uzalendo utanishinda itabidi nijichange nikate tu AAR sasa.
Tena na watu hapa wanakatisha tamaa sijui dawa gani hupewi duh!

Mzalendo mwenzangu....kwa nini uwaze Agakhan ambayo ni Zonal level Usiwaze Muhimbili ambayo ni National level?

Leo hii ukienda huko unakowaza wakikushindwa utahamishiwa Muhimbili ambako ukiwa na NHIF Kifurushi unafika bila tatizo lolote.

MI NADHANI TUACHE KUWA MADALALI......
 
Wanaboa kwa kweli. Wanajua magonjwa yanayowaandama wastaafu wengi, wamezuia fawa muhimu nyingi. Mfano dawa Za kisukari nyingi, Za hypertensjon nk unaenda dukani wanakwambia dose ya mwezi ni 170,000na hiyo ni moja. Daktari anasema wafanyakazi wadi TRA. Benki wanaruhisiwa bilar shida. Ubaguzi gani huo. Au ninyi hamtazeeka na kustaafu?
Majanga😭😭😭😭😭Nilikuwa sifahamu hili
 
NHIF Pale Hospital ya Wilaya ya Nzega ni hovyo kabisa.

Kazini muda mwingi hawapo!! USIKU PIA HAWAPO!!! JUMAMOSI NA JUMAPILI HAWAPO!!!!

Wagonjwa wanaotumia Bima ni shida tupu!!!

HIVI USIKU ,AU SIKU ZA WIKENDI WAGONJWA WANAOTUMIA BIMA WAMEAGANA NAO KUWA HUWA HAWAUMWI????

Mike wangu alilazwa na mtoto mdogo lakini aliambiwa wahudumu was kujaza Form za NHIF hawapo!!! Hivyo alipie matibabu pamoja na dawa!!! USIKU ule niliwapigia simu watu was Bima! Bahati mbaya wakataka wazungumze na mtu aliyepo Hospitalini!! Mke wangu na ndugu wakashauri ni Bora kulipia mtoto apone maana hali ilikuwa ni mbaya zoezi likashindikana!!!!

Hospital ya Nzega ya Wilaya kitengo Cha BIMA KIMULIKWE VIZURI.

Kadi za kumuandikia mgonjwa unaambiwa kanunue dafutari nje ya pale kwenye geti la kuingilia!!! No biashara ya mtu ile!!!
Pole sana ndugu yangu.
Sasa hilo siyo la NHIF ila ni uzembe wa hospitali husika .....NHIF huingia mikataba na watoa huduma ili waweze kuwahudumia wanachama wake na baada ya huduma NHIF humlipa mtoa huduma kulingana na huduma iliyotolewa.

Sasa wapo watoa huduma ambao wanafanya mambo ambayo yanarudisha nyuma nia njema ya serikali na NHIF kwa ujumla.

Mi nadani hili wahusika wa NHIF wamelipata na watafuatilia kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri huko NZEGA.

POLE SANA
 
MGURUGENZI WA NHIF MULIKA WATUMISHI WA NHIF HOSPITALI YA WILAYA YA NZEGA.

- Kwanza muda mwingi hawapo kazini.Mfano, JUMAMOSI,JUMAPILI,na nyakati zs USIKU!!! Je WAGONJWA WA BINA NYAKATI HIZO HUWA HAWAUMWI?? NDIVYO MLIVYOAGANA NAO KWAMBA NYAKATI HIZO WAGONJWA WANAOTUMIA BIMA HAWAPASWI KUUMWA NA IKITOKEA WAMEUMWA NYAKATI HIZO WANAPASWA WAJIGHARAMIE MATIBABU ILIHALI WANABI A KISA MJAZAJI WA FORMU HAYUPO KAZINI?????????

-Kadi la Mgonjwa Lile gumu ,Unaambiwa kanunue dafutari dogo hapo getini kwao!!! Huo huenda ni mradi wa mtu.!!

- Dawa nyingi Unaambiwa hazipo kanunue😠Ni wajibu wenu kuhakikisha Dawa zote zipo kwa wagonjwa wa Bima.Vinginevyo mtupage na hela za kununulia HIZO Dawa maduka ya Phamarcy.

MKURUGENZI HAKIKISHA WATUMISHI WAPO MUDA WOTE HASA NYAKATI ZA USIKU NA WIKENDI.HILI NI KEROOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Pole sana ndugu yangu.
HILI NI LA MKURUGENZI WA WILAYA YA NZEGA ......ILA

KWA KUWA NHIF INAFANYA KAZI SAMBAMBA NA SERIKALI NADHANI MKURUGENZI MKUU HILI AMESHALIPOKEA.

NA tunamwomba ahakikishe anawasiliana na Mkurugenzi wilaya ya Nzega ili watumishi wa Hospitali ya Nzega wanaosababisha malalamiko wanashughulikiwa kulingana na taratibu za utumishi wa umma. Kwa sababu kwanza wanatkiwa kujua kwamba Hospitali za serikali zina vyanzo vifuatavyo vya mapato.
1. Mapato yatokanayo na kutibu wanachama wa NHIF. (hiki ndo chanzo kikubwa)
2. Mapato yatokanayo na kutibu wananchi kwa cash (yaani wasio na Bima)
3. Na mapato yatokanayo misaada mbali mbali ya serikali

Sasa kitendo cha kufunga dirisha la Bima ni kuikosesha hospitali mapato kutoka Bima.

POLE SANA
 
Mkuu ulivyoelezea unaonesha unayajua haya mambo vizuri. Ila kumbuka wanaolalamika hapo juu ndi watumiaji halisia wa mwisho wa huduma.

Inaweza kua ulichokisema kiko kwenye makaratasi tu kama maua. Nenda front sasa....utumbo.
Nilichokieleza hapo kipo kwenye soko na kinapatikana bila shida yoyote baada ya wizara kwa kushirikiana na NHIF kufanya maboresho katika kitita chake cha dawa......Nayazungumza haya maana waandishi waliitwa wakati kuzungumzia huduma za dawa za NHIF .

Hivyo hili ni jambo linajulikana na wala siyo la siri .

Muhimu ukipata shida kwenye kituo cha matibabu wapigie kwa numba zao za huduma kwa wateja 0800110063 na mambo yatakwenda vizuri.
 
Mzalendo mwenzangu....kwa nini uwaze Agakhan ambayo ni Zonal level Usiwaze Muhimbili ambayo ni National level?

Leo hii ukienda huko unakowaza wakikushindwa utahamishiwa Muhimbili ambako ukiwa na NHIF Kifurushi unafika bila tatizo lolote.

MI NADHANI TUACHE KUWA MADALALI......
Mkuu umeongea bonge la point. Na nakuambia aisee si umeona hapa watu wanalalamika NHIF sijui dawa hizi haziwi covered nenda kanunue sijui hiki, yaani haya ni malalamiko ya watu wengi sana.
Serekali kuna changamoto wanazifumbia macho aisee. Na wanajua kabisa sema ni ile kwamba iko kisiasa zaidi mtu akipanda jukwaani ikitajwa bima ya afya ya taifa vigelegele hakuna wakuuliza changamoto ni zipi. Yaani dizaini ile ya tumejenga mahospitali 999,999 watu weweeeeeeee. Makofi. Kumbe ukija ground zero huku hospital zipo madawa hamna, xray mbovu......

Back to the topic......mkuu mpk uumwe upelekwe muhimbili umeumwa kweli kweli. Nashkuru Mungu haijawahi tokea hivyo. Kama ingalikua hata magonjwa tu ya kawaida tunaruhusiwa kutimba muhimbili straight waaaaiiiii NHIF mbn mpango mzima. Napenda sana muhimbili pamoja na issues za hapa na pale kuliko hata Agakhan honestly.

Sasa km Mungu anajaalia mtu unaumwa tu kawaida bila kuhitaji referal ya Muhimbili NHIF inakua shida sasa km wadau walivyosema hapo juu. Yaani hata dawa zingine za kawaida tu eti haziko covered. Shida.
Mimi ni mzalendo sana aisee. Na hiyo Agakhan sio km nai promote hapana. Private ni private tu. Maana wife alijifungulia pale walikua wampige operation nikawashikia bango tusubiri uchungu uzidi meisho mtoto katoka kwa njia ya kawaida. Nao wako kipesa zaidi inabidi sometimes uwe nao makini. So hawako perfect wala.
 
Nilichokieleza hapo kipo kwenye soko na kinapatikana bila shida yoyote baada ya wizara kwa kushirikiana na NHIF kufanya maboresho katika kitita chake cha dawa......Nayazungumza haya maana waandishi waliitwa wakati kuzungumzia huduma za dawa za NHIF .

Hivyo hili ni jambo linajulikana na wala siyo la siri .

Muhimu ukipata shida kwenye kituo cha matibabu wapigie kwa numba zao za huduma kwa wateja 0800110063 na mambo yatakwenda vizuri.
Sasa haya ndio mambo sasa. Kumbe kuna mpk toll free number yakupiga. Nauhakika hii number watu hawaijui.
Na kusema kweli wakati mwingine hizi hospital private nahisi inategemea reception unakutana na nani na kaamkaje siku hiyo. Wengine wanajifanya wajuaji. Hiki hakiwi covered hiki sawa. Kumbe ukipiga number km hiyo ukaongea na mhusika wa NHIF anaweka mambo sawa maani yeye ndie mjuzi wa hiyo bima.
Anyhow wakati mwingine ni Elimu Elimu Elimu ambayo ni pamoja na kuwajuza watu kuna number so and so ukitatizika piga.
 
Mkuu umeongea bonge la point. Na nakuambia aisee si umeona hapa watu wanalalamika NHIF sijui dawa hizi haziwi covered nenda kanunue sijui hiki, yaani haya ni malalamiko ya watu wengi sana.
Serekali kuna changamoto wanazifumbia macho aisee. Na wanajua kabisa sema ni ile kwamba iko kisiasa zaidi mtu akipanda jukwaani ikitajwa bima ya afya ya taifa vigelegele hakuna wakuuliza changamoto ni zipi. Yaani dizaini ile ya tumejenga mahospitali 999,999 watu weweeeeeeee. Makofi. Kumbe ukija ground zero huku hospital zipo madawa hamna, xray mbovu......

Back to the topic......mkuu mpk uumwe upelekwe muhimbili umeumwa kweli kweli. Nashkuru Mungu haijawahi tokea hivyo. Kama ingalikua hata magonjwa tu ya kawaida tunaruhusiwa kutimba muhimbili straight waaaaiiiii NHIF mbn mpango mzima. Napenda sana muhimbili pamoja na issues za hapa na pale kuliko hata Agakhan honestly.

Sasa km Mungu anajaalia mtu unaumwa tu kawaida bila kuhitaji referal ya Muhimbili NHIF inakua shida sasa km wadau walivyosema hapo juu. Yaani hata dawa zingine za kawaida tu eti haziko covered. Shida.
Mimi ni mzalendo sana aisee. Na hiyo Agakhan sio km nai promote hapana. Private ni private tu. Maana wife alijifungulia pale walikua wampige operation nikawashikia bango tusubiri uchungu uzidi meisho mtoto katoka kwa njia ya kawaida. Nao wako kipesa zaidi inabidi sometimes uwe nao makini. So hawako perfect wala.

Asante sana....You are realy greatthinker.
Si unaona kama usingekuwa makini kwa sasa Wifi yetu angekuwa tayari na alama ya kidonda ambacho siyo sahihi.

Mi ninachojua serikali na NHIF inajitahidi sana kuhakikisha matibabu sahihi yanapatikana kwa wananchi wake bila kufanya biashara kwenye miili na maisha ya watu.....CHANGAMOTO NI TAARIFA SAHIHI KUWAFIKIA WANANCHI.

NA hili NHIF na serikali walichukue kama changamoto kuhakikisha taarifa za huduma za afya zinapatikana kwenye mikono ya wananchi kwa urahisi.
 
Ninamiaka 10+ sijaugua, zaidi ya mafua tu. Sina mpango wa hayo mabima. Siku nikiumwa nitatoa hela yangu mfukoni
 
Niliwahi kwenda kwa Mama Ngoma hospital kuchek malaria tuu nikakutwa no malaria.
Dr akanipandikia panadol basi nimeenda dirishani ananipa tembe za kuhesabu namuuliza kwani hakuna za blister ananijibu wewe unatumia kadi huwezi pata hizi........................... Aliyaoga maana sio kwa kumpa maneno yale.
 
Kwa upeo wangu mdogo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatoa huduma dawa zote za msingi kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla, hakuna ukweli wowote wa kuondolewa kwa baadhi ya dawa katika orodha, dawa aina ya intravenous iron sucrose(Iron sucrose Injection) ipo katika orodha ya dawa za NHIF na inapatikana katika hospitali na maduka ya dawa yaliyosajiliwa

zaidi mfuko hivi karibuni kwa kushirikiana na wizara ya afya umeongeza dawa nyingine zaidi 71 katika orodha yake ya dawa hii ni baada ya mapitio na maboresho ya orodha za dawa za msingi zilizoainishwa katika muongozo wa Tiba wa Taifa (Standard Treatment Guideline)
Ndugu wameongeza dawa zisizohitajika, wametoa dawa zinazohitajika, hasa za wazee na magonjwa korofi.. Watu tunaouguza tunaelewa maumivu!

Everyday is Saturday............................. :cool:
 
Kwa upeo wangu mdogo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatoa huduma dawa zote za msingi kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla, hakuna ukweli wowote wa kuondolewa kwa baadhi ya dawa katika orodha, dawa aina ya intravenous iron sucrose(Iron sucrose Injection) ipo katika orodha ya dawa za NHIF na inapatikana katika hospitali na maduka ya dawa yaliyosajiliwa

zaidi mfuko hivi karibuni kwa kushirikiana na wizara ya afya umeongeza dawa nyingine zaidi 71 katika orodha yake ya dawa hii ni baada ya mapitio na maboresho ya orodha za dawa za msingi zilizoainishwa katika muongozo wa Tiba wa Taifa (Standard Treatment Guideline)
Hivi unatumia bima ya NHIF kweli wewe? Umewahi kuugua ugonjwa unaokuhitaji kuchukua dawa kila mwezi hivi karibuni mkuu?
 
Ninamiaka 10+ sijaugua, zaidi ya mafua tu. Sina mpango wa hayo mabima. Siku nikiumwa nitatoa hela yangu mfukoni
Kama utataka labda ukate zile za binafsi zenye bei kubwa, ila hiyo ya "najali afya" wala hata usihangaike nayo, watakuhesabu tu miongoni mwa watu wenye kumiliki bima Tanzania lakini hutapata huduma nyingi sana za msingi ikiwemo madawa. Sisi spana mkononi ndio tunaumia sana kutuondolea madawa yetu ya maana 😔
 
Wengine tumekata bima za binafsi kukwepa gharama kubwa za dawa za kila mwezi lakini nilipopiga namba yao ya huduma kwa wateja wananiambia ninawalaumu bure, wa kuwalaumu ni wizara ya afya waliowapa muongozo wa kuondoa hizo dawa.
Na huo ndio ukweli wenyewe, mchawi ni wizara na Standard Treatment Guidelines zao. NHIF wamekazia tu maana wanaona ipo in their favour

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichokieleza hapo kipo kwenye soko na kinapatikana bila shida yoyote baada ya wizara kwa kushirikiana na NHIF kufanya maboresho katika kitita chake cha dawa......Nayazungumza haya maana waandishi waliitwa wakati kuzungumzia huduma za dawa za NHIF .

Hivyo hili ni jambo linajulikana na wala siyo la siri .

Muhimu ukipata shida kwenye kituo cha matibabu wapigie kwa numba zao za huduma kwa wateja 0800110063 na mambo yatakwenda vizuri.
Wewe jamaa utakua moja ya wagombea waliopita bila kupingwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom