NHIF mnahatarisha maisha ya Wajawazito

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,123
7,709
Wakina mama Wajawazito ni kundi maalum ambalo linapaswa kuangaliwa vyema ndio maana serikali inatoa huduma bure kwa wamama wajawazito.

Lakini jambo la kushangaza NHIF hawajali kabisa inapotokea mama mjamzito kaandikiwa dawa muhimu ya kuongeza damu kwa mama mjamzito NHIF wanakataa na kusema hiyo dawa haipo katika bima, hakika hii ni hatari sana kwa mama zetu.

Muongozo uliowekwa na NHIF hauwajali wala kuwazingatia kundi la maalum la wamama wajawazito ambalo ni kutokana na hali zao ni rahisi kupoteza uhai wao.

NHIF kuweni ni utu kwa wajawazito tu, utaratibu au muongozo mlioutoa unawanyanyasa wajawazito badilisheni huo muongozo/utaratibu haraka ili wajawazito wapate huduma zinazo stahili bila kikwazo, haswa katika hospitali za binafsi kuna shida.

NHIF zingatieni wajawazito ondoeni vikwazo mtaangamiza maisha ya mama zetu.
 
Hawa watu wanakoelekea siko, hata huduma tu kwa sasa wanazingua, yaan ni kama luku kwa sasa hujalipa huduma hupati but mostly wao ndio wanaweza kuwa chanzo cha kutokamilisha malipo. Mfano wanakupa invoice iliyo na makosa.
 
Huwa najiuliza sipati jibu!

Hivi kweli hao ambao hupanga utaratibu ni watanzania kweli?! ni wanawake au wanaume? wanauchungu na kina mama kweli?

Wanaishi nchi hiii hiii au wanaishi nchi jirani?
 
NHIF ni matapeli sana hivi vifurushi vipya ni sawa na kulipia kumuona daktari zaidi ya hapo zingine unanunua mara hailipii kulaza mara kuna baadhi ya vipimo huwezi fanya bila kulipia ni kero tupu.
 
Dawa za kuongeza damu ferrous sulphate kwa wajawazito ni aina ya suppliment (virutubisho). Ikiwa mama mjamzito atapata mlo kamili kama vyakula vya dagaa, nyama, maini, mboga mboga n.k hatakuwa katika hatari ya kupungukiwa damu kipindi cha ujauzito au wakati wa kujifungua.

Jambo la kuzingatia ni mama mjamzito apate lishe bora, aende kiliniki inavyotakiwa, kule atapimwa uzito, wingi wake wa damu, uwepo wa minyoo na magonjwa kama malaria n.k.(ambayo kwa pamoja husababisha upungufu wa damu).

NHIF wanapaswa kubadilika na kuweka hivi virutubisho vya wajawazito vitolewe na vipewe umuhimu. Kutokana na mazingira, hali ya maisha, uelewa wa lishe bora bila kusahau umasikini. NHIF wasiangalie kutengeneza pesa na kupata faida kubwa tu, ila pia wajali afya na maisha ya wanachama wao na wachangiaji, pia kuna umuhimu wa huu mfuko kufanya mabadiliko mara kwa mara kutokana na mahitaji ya wateja na wanachama wake.
 
wanachama haswa watumishi wa umma ambao ni wachangiaji wazuri wa NHIF lkn bado utakuta wanadhalalika!!! NHIF toeni huduma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF fanya kazi kwa maslahi ya watanzania wanyonge,
fuatilia kero za wanachama wachangiaji usisubiri mpaka waziri wa afya au waziri mkuu
 
Hizo dawa zinatakiwa wapatiwe Bure hawa wajawazito kama sehemu ya kuhamasisha watu wazaliane kwa wingi,Kama NHIF hawazitoi kutakuwa na tatizo mahali.
 
NHIF nao wamebanwa hawana pesa, pesa yote ya makato na malipo kwa watoa huduma ipo chini ya mhasibu mkuu wa Taifa. Kuna vipimo vipo kwenye Bima, lakini kuna baadhi ya hosp wanasita kukuhudumia sababu ya mlolongo wa kudai malipo yao.
 
Hujui Unachokiongeaa mzee...!! Hizi suppliment ni za muhimu sana sababu mama wajawazito wengi hawana uwezo wa kulaa vyakula vyenye iron au folic kwa wingi kama inavyotakiwa na pia hata wakila hawawezi kupata Enough amount ya kusupport ukuaji wa mtoto vilivyo so hii ndo unapata watoto wenye Vichwa vikubwa na wengine wenye defect kibao.

Wanachofanya NHIF ni utapeliii mkubwa wametoa mpaka Dawa za pressure nyingine nyingi tuu sasa wasipodhibitiwaa watawaibiaa sana watanzania aisee.. Serikali isiwachekee NHIF wanaletaa ufalaa sanaa
 
Ni sahihi dawa zinazo wahusu wajawazito zinapaswa ziwe covered kwenye Bima (NHIF)maaana hapo tunaokoa vifo vya mama Na mtoto hakuna sababu ya kukwepa, isitoshe ni kipindi cha mpito tu kwa nn wasipewe upendeleo wa kupewe dawa za msingi?
Kwa nn mnaziondoa dawa ZA msingi kwa wajawazito? Mnataka wafe? Hili halikubaliki kabisa,
Nasimama Na mama zetu wajawazito waIngatiwe ipasavyo ktk Bima zao isitokee mama mjamzito apoteze maisha kisa eti dawa aliyotakiwa kupewa haipo ktk bima!! Watanzania nani katuloga?!
 
Ile bima ya watoto ya 50400/= ni kiini macho.
1. Kuipata ni baada ya siku 90 tokea uikate.
2. Huduma nyingi hakuna.

Najuta kuikata.
... ili usisubiri mtoto yuko mahututi na gharama za matibabu ya tatizo ni kubwa ndio ukimbilie kukata bima. Taratibu za bima (yoyote) haziko hivyo; insurance means to protect you from the unforeseen than the already seen! Huwezi kuwa gari limeshapata ajali ndio ukakate bima; kata likiwa zima bila hata wazo kwamba kuna siku litapata ajali.
 
Hujui Unachokiongeaa mzee...!! Hizi suppliment ni za muhimu sana sababu mama wajawazito wengi hawana uwezo wa kulaa vyakula vyenye iron au folic kwa wingi kama inavyotakiwa na pia hata wakila hawawezi kupata Enough amount ya kusupport ukuaji wa mtoto vilivyo so hii ndo unapata watoto wenye Vichwa vikubwa na wengine wenye defect kibao.

Wanachofanya NHIF ni utapeliii mkubwa wametoa mpaka Dawa za pressure nyingine nyingi tuu sasa wasipodhibitiwaa watawaibiaa sana watanzania aisee.. Serikali isiwachekee NHIF wanaletaa ufalaa sanaa
... sure! Tunahitaji taifa lenye watoto wenye afya bora kuliko mazezeta! Bila kujenga msingi imara (wajawazito wenye afya, watoto wenye afya) kuzifikia Korea, Singapore, sijui Taiwan ni ndoto maana bongo na afya za watoto wetu zitakuwa chini ya kiwango. We need great mathematicians, scientists, lawyers, etc.
 
Wakina mama Wajawazito ni kundi maalum ambalo linapaswa kuangaliwa vyema ndio maana serikali inatoa huduma bure kwa wamama wajawazito.

Lakini jambo la kushangaza NHIF hawajali kabisa inapotokea mama mjamzito kaandikiwa dawa muhimu ya kuongeza damu kwa mama mjamzito NHIF wanakataa na kusema hiyo dawa haipo katika bima, hakika hii ni hatari sana kwa mama zetu.

Muongozo uliowekwa na NHIF hauwajali wala kuwazingatia kundi la maalum la wamama wajawazito ambalo ni kutokana na hali zao ni rahisi kupoteza uhai wao.

NHIF kuweni ni utu kwa wajawazito tu, utaratibu au muongozo mlioutoa unawanyanyasa wajawazito badilisheni huo muongozo/utaratibu haraka ili wajawazito wapate huduma zinazo stahili bila kikwazo, haswa katika hospitali za binafsi kuna shida.

NHIF zingatieni wajawazito ondoeni vikwazo mtaangamiza maisha ya mama zetu.
Mfuko wa taifa wa bima ya Afya unawajali wanachama wake na wananchi kwa ujumla wakiwemo wajawazito na watoto katika kuzingatia hilo mfuko unatoa huduma za dawa zote zinazotumika hospitali katika kuongeza damu dawa hizo ni kama vidonge vya kuongeza damu (ferrous sulphate + folic acid) dawa ya maji ya kuongeza damu (ferrous fumarate syrup) pia mfuko unatoa dawa za sindano za kuongeza damu (intravenous iron sucrose) pamoja na homoni ya kuongeza damu Erythropoietin

Huduma hizi zote zinapatikana kuanzia ngazi ya zahanati Nchi nzima mpaka hospitali za Taifa hii ni kama huduma hizi zilivyoelekezwa na sera za Wizara katika kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto

NHIF Huduma bora za matibabu ni haki yako na ni dhamana yetu.
 
Hujui Unachokiongeaa mzee...!! Hizi suppliment ni za muhimu sana sababu mama wajawazito wengi hawana uwezo wa kulaa vyakula vyenye iron au folic kwa wingi kama inavyotakiwa na pia hata wakila hawawezi kupata Enough amount ya kusupport ukuaji wa mtoto vilivyo so hii ndo unapata watoto wenye Vichwa vikubwa na wengine wenye defect kibao.

Wanachofanya NHIF ni utapeliii mkubwa wametoa mpaka Dawa za pressure nyingine nyingi tuu sasa wasipodhibitiwaa watawaibiaa sana watanzania aisee.. Serikali isiwachekee NHIF wanaletaa ufalaa sanaa
Ulieleza kama vile NHIF na serikali havifahamiani!
 
Dawa za kuongeza damu ferrous sulphate kwa wajawazito ni aina ya suppliment (virutubisho). Ikiwa mama mjamzito atapata mlo kamili kama vyakula vya dagaa, nyama, maini, mboga mboga n.k hatakuwa katika hatari ya kupungukiwa damu kipindi cha ujauzito au wakati wa kujifungua.

Jambo la kuzingatia ni mama mjamzito apate lishe bora, aende kiliniki inavyotakiwa, kule atapimwa uzito, wingi wake wa damu, uwepo wa minyoo na magonjwa kama malaria n.k.(ambayo kwa pamoja husababisha upungufu wa damu).

NHIF wanapaswa kubadilika na kuweka hivi virutubisho vya wajawazito vitolewe na vipewe umuhimu. Kutokana na mazingira, hali ya maisha, uelewa wa lishe bora bila kusahau umasikini. NHIF wasiangalie kutengeneza pesa na kupata faida kubwa tu, ila pia wajali afya na maisha ya wanachama wao na wachangiaji, pia kuna umuhimu wa huu mfuko kufanya mabadiliko mara kwa mara kutokana na mahitaji ya wateja na wanachama wake.
Unaweza kupata balansid dayati vyema kbs lakini ukapatwa upungufu na malaria plus..mimba isikie tu
 
Back
Top Bottom