NHIF, kwanini vifurushi vipya vikatae kutibu figo, moyo na kansa?

Date20210317

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
3,862
2,000
Kama ni kwel, basi ni hatar sana.Ingawa Bima inasaidia sana .

Wajaribu kuweka utaratibu wa kuya take care na haya masuala kwa maslah ya Watanzania.
Nashauri badala ya kusema magonjwa hayo bima haita cover wafanye hivi, ukiugua hayo magonjwa, bima iwe na % yake ya kugharamia na mgonjwa atakiwe ku top up some % remaining.

Lakin kuacha the whole Lot kwa mgonjwa ambaye anakatwa pesa zake monthly, is not fair. Tufanye kushare hizo cost basi maana wafanyakazi wanakatwa pesa zao nyingi.
 
Wanu

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
352
250
Ni wajibu wa serikali kuhakiksha Mwananchi wake anapona hata kama hana bima, unaposema wakitoa zaidi ya wanachopokea wana collapse sasa serikali inamchango gani hapo??
FRESHMAN,
Bima ya afya siyo msaada kama unavyofikiri. Wakitoa zaidi ya wanazokusanya basi itafikia muda ita-colapse na hakutakuwa na fedha za matibabu. Pengine ungetowa ushauri kama hayo magonjwa hayapo kwenye list basi wayaweke ila gharama zake ziwe kubwa.
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,291
2,000
Wanaharakati wapo wapi? haya ndio mambo ya kupigia kelele lakini mara nyingi hawa wanaojiita wanaharakati wana ajenda zao za kisiasa kwa kivuli cha harakati. TETEA MNYONGE KWA MAMBO YA MSINGI.
Nakuunga mkono mdau.
Wana harakati wa Tanzania wapo active kwenye mambo ya kisiasa zaidi, ndio maana serikali inawawekea mashariti na sheria ngumu ikiamini wanasukuma na kutekeleza agenda za wafadhili wao.

Ukiangalia vifurushi vya bima ya afya ya NHIF vimekaa kibiashara zaidi na sio kutoa huduma.
Zipo kama taasisi au kampuni binafsi ya kibiashara iliyo lenga faida.

Afya, elimu, miundombinu ni wajibu wa serikali sababu inakusanya kodi. Inatakiwa wananchi wachangie afya kwa mfumo wa bima mpango wa taifa wa mfuko wa bima ya afya.

Vifurushi muhimu vihudumie na magonjwa hayo makubwa yanayo hitaji gharama kubwa. Kama michango ya wananchama haitoshi, basi kiasi kilicho pungua ijazie serikali. Mfuko uwe ni wa kutoa huduma sio wa kibishara 100%. Kama serikali inaweza kuyabeba mashirika mengine ya umma basi hata huu mfuko ubebwe zaidi kwa vile tunazungumzia maisha ya raia wake.

Hayo malaria na magonjwa mengine madogo tunaweza wenyewe kujihudumia.
Mleta mada kataja figo, moyo na saratani lakini ukweli kuna huduma nyingi sana za vipimo na madawa zimeondolewa, imekuwa kero kubwa mno kiasimfuko unaanza kuonekana ni wa kinyonyaji tu, ipo siku watu wataenda mahakamani kuomba watumishi wa umma na wanachuo wasilazimishwe kujiunga.

Kero ya mwisho ni bima ya wanafunnzi(wanachuo) wa elimu ya juu. Kuna baadhi ya vyuo kuna uhuni mkubwa unafanyika.
Mwanafunzi analipia bima lakini hapati kadi hadi mwaka unaisha au anapata kadi baada ya miezi zaidi ya 6 tangu alipie bima.
Unakuta mwaka mwingine mpya wa masomo umeingia analazimishwa alipie tena vinginevyo hafanyiwi usajili hadi alipie bima ya afya wakati ya mwaka uliopita haijatimia mwaka tangu apewe kadi yake.

Nauliza kuna uhusiano gani kati ya mambo yake ya taaluma na hiyo bima ya afya hadi anyimwe haki yake ya msingi?
Chuo cha Ustawi wa Jamii kilichopo DSM ndio kinaongoza kwa hili tatizo. Inafikia hatua mtoto akienda kuwaambia mzazi wangu amekuwa mkali anataka majibu kabla hajaenda ngazi zingine utaona wanampa kadi haraka sana.

Inawezekana uongozi wa chuo au wa wanafunzi unao husika na mambo ya bima ya afya chuoni hapo wanatakatisha fedha hapa kwa kuziweka bank ktk fixed account kisha wanachukua faida(riba) au wanajikopesha au wanakopesha sehemu zikirudishwa ndipo wanaenda kumlipia mwanafunzi. Hizi ni hisia tu hivyo ni wajibu wa mamlaka husika kufuatilia tuhuma hizi na wahusika wajisafishe.
Inawezekana kuna uzembe tu na sio utakatishaji fedha.
 
seyayi

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
681
1,000
Mfuko umeyumba hilo liko wazi tena sasa hivi wamekuwa wahuni mno,dawa zinatolewa kwa masharti mno,dawa wagonjwa wanapewa nusunusu,nyingine ukanunue mwenyewe ni wazi kujoin kwa watu wasio watumishi kumewaelemea,lakini pia mifuko hii ndimo central govt inapochota chapaa kufanya mambo yake.#TWAFA#
 
Siempre Hechos

JF-Expert Member
Dec 9, 2016
1,063
2,000
Fahari ya mwanadamu ni kuwa na afya njema na ndio maana serikali imeona ni jambo jema sana kuweka vifurushi vya watu kuweza kujilipia kwa wale ambao sio waajiliwa. Lakini sambamba na hilo mi nafikiri serikali ( kwenye hospitali za serikali) ingeanzisha mfumo (online ) wa kuweka gharama za vipimo vyote, gharama za dawa zote( maana ziko registered) na gharama za consultation kwa madaktari ili wananchi wajue anapokwenda hospitali hasa kwa wale wasiokuwa na bima ya afya waweze kujiandaa kwa kiasi gani. Nimelisema hili kwani kuna rafiki yangu alimpeleka mdogo wake hospitali ya serikali ( mdogo wake hana bima) bili yake aliyopewa hakuamini kama ingekuwa kubwa kwa kiasi kile kulingana na huduma aliyopewa, mpaka akajiuliza hivi kujilipia matibabu tena hospitali ya serikali ni ghali kiasi hiki?

Hivyo basi, mi nafikiri hili likifanyika basi watu (wasiokuwa na bima ya afya) watapata wasaa wa kufanya makadirio ya gharama za matibabu pindi wanapokwenda hospitali sio unafika kule unajikuta pesa uliyonayo haitoshi sijui hapo watakufanyaje na huduma umeshapata!
 
double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,363
2,000
Mifumo ya Afya mibovu inatengeza shida nyingi.
Kuna nchi zilizofaulu kwa nini tusiige huko.
 
Kiwarhoapandenga

JF-Expert Member
Aug 10, 2019
2,080
2,000
habari wadau,

NHIF ni shirika la uma.. na linatoa huduma kwa Watanzania. Nimeshangaa kuona vifurushi vyao vyote vipya, vinakataa kutibu magonjwa makubwa figo, kansa na moyo

Inasemekana zamani walikuwa wanatibu ila hadi upite mwaka mmoja toka umejiunga. Ila vya sasa havitibu kabisa hata ukipita mwaka. Hii ni hatari maana ikitokea mtu ukaja pata ugonjwa mkubwa wa moyo, kansa au figo mbeleni. NHIF haikusaidiii chochote.

Mtu unalipia bima ya afya na ni unakatwa kodi ila unakufa huku unajiona. maana bima inakataa hayo magonjwa. Kwa hili NHIF wajiangalie. maana magonjwa makubwa kama figo, moyo, kansa ndio yana gharama kubwa na yanahitaji msaada wa bima ya afya na serikali

KABLA HUJAJIUNGA NA BIMA YA AFYA NI VIZURI UKASOMA MAELEZO YAO VIZURI.. NIMEAMBATANISHA COPY NILIYOSOMA.. NA NIKAONA FIGO, KANSA, MOYO NA MENGINEYO HAWATIBU

=====
Hoja za wadau
Aiseee labda enzi za mwaalimu kulikuwa kuna fungu la weupe walikuwa wanaongezea hapo kwa sasa halipo kazi ndio inaanzia hapo ile michango ya kicheni pati ,harusi naiona hiyooo inahamia kwenye kutibiana MUNGU saidia masikini
 
Ze Heby

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,641
2,000
Umeiweka vizuri sana

Bima ni kushare risk, maana gharama za matibabu nu kubwa..Watu wanakata bima ya laki tano kwa mwaka anatumia matibabu ya milioni tatu hajui ile nyingine inatoka wapi. Tunachangiana aisee
Watu wengi hawajui jinsi mifuko ya Bima ya Afya inavyofanya kazi, hasa mfumo wa Bima ya Afya ya Taifa.

Kwanza tujue Bima ya Afya ya Taifa imeanzishwa kwa sheria, na awali ilianza kwa kukata mishahara ya watumishi wa serikali bila kujali kama huumwi au waumwa. Na ukweli hii michango ya Watumishi ndio hasa inayoifanya mifuko hii isife. Hii kwa sababu ndani ya ‘pool’ ya hawa wachangiaji, watu wengi hawaumwi. Lakini kwa sasa kwa wale watanzania wanaokwenda kujiunga kwenye mifuko hii kwa hiari wengi huwa ni wagonjwa na hivyo mara wakijiunga huanza kutumia pesa ambazo zimeshachangwa na wananchi wengine (ambao wengi ni wafanyakazi) kama mchwa.

Mimi sio mtumishi wa Bima ya Afya yeyote ile. Mimi ni daktari ambaye ninahudumia wagonjwa wote wenye Bima ya Afya na wasio na Bima ya Afya. Kati ya watu ambao huwa napata changamoto kuwahudumia ni wale wasiokuwa na Bima ya Afya. Kila kitu ninachotaka nifanye, kama kuomba vipimo au kuandika dawa, inanipasa nimpe wastani wa gharama anazopaswa kulipia, kwa sababu ya uwezo wake. Huwa naanza kufanya kazi kama daktari lakini pia ‘mhasibu’ ili mgonjwa asilemewe. Kuna baadhi ya vipimo na dawa za muhimu itanipasa niziondoe ili mgonjwa aweze kumudu matibabu. Kwa ufupi matibabu bora kwake hupungua kulingana na uwezo wake.

Watanzania wengi hatujui bima ya Afya ni nini. Nataka nitumie lugha nyepesi labda ninaweza kueleweka kwa baadhi ya watu.

Mtu yeyote kati yetu anaweza akawa ni tegemeo kubwa kwa ukoo au familia fulani kubwa, labda tumfananishe na Chifu. Anategemewa kuunganisha familia kwa pesa, ushauri, na kuwaunganisha katika matukio mbalimbali. Mtu huyu kila kuwapo na shida ukoo humfuata ili ahusike kulitatua. Huyu ni sauti ya ukoo.

Labda nitoe mfano. Tufikirie kila baada ya siku kadhaa huyu mtu anaambiwa ndugu yake fulani anaumwa, hivyo anapaswa apelekwe hospitali. Yamkini hadi sasa ameshatumia gharama nyingi za kutibu wanafamilia wengine huko nyuma na au ameshachangisha wanafamilia fulani wenye uwezo kiasi ili kusaidia matibabu lakini sasa nao wamechoka kwa kuwa yamkini hawana pesa tena au na wao wana majukumu mengine ya muhimu hivyo hawawezi kuchangia matibabu ya ndugu wengine wakati hizo pesa zinahitajika kwenye mambo mengine ya msingi.

Kwa hekima za Chifu anaamua kulipa gharama au kuchangisha kwa mara ya mwisho, lakini anaitisha mkutano wa ukoo. Chifu anawaambia ndugu kwa sababu kumekuwa na changamoto ya gharama za matibabu, basi wao kama familia watengeneze mfuko wa familia wa matibabu. Pesa za mfuko huu zitatumika kulipia matibabu kwa mchangoaji yeyote pale atakapoumwa. Kama mtu hatokubali kuchangia basi hatanufaika na michango ya mfuko huo. Mfuko huo utaanzishwa na pesa za wanafamilia na utaendeshwa na pesa hizohizo. Hakuna pesa ya nje inaingizwa kama mtaji.

Wanafamilia wanakubaliana kwamba basi kila mtu anayefanya kazi atachangia katika mfuko huu asilimia fulani ya mshahara wake wa mwezi, iwe una au huna watoto, mke, mume, au wazazi ni lazima uchangie. Inatolewa mwongozo kwamba kila mtu mchango wake unaweza kuwaingiza ndani ya mfuko wategemezi wake watano; na ili mfuko uweze kuwa endelevu na hao wategemezi wawe ni Baba au Mama au Watoto au Mke au Mume. Tukumbuke tegemezi ni yule ambaye kwa namna moja au nyingine anaweza akawa hawezi kuchangia kwenye mfuko na kwa watoto ni wale ambao hawajafikia umri wa miaka 18.

Hawa wana ndugu wanaweza kukubaliana kwa wale wasiokuwa na ajira rasmi kuwatengenezea vifurushi tofauti tofauti ili nao wanufaike na huduma hii.

Kitu kimoja kikubwa katika mfuko huu wa wanafamilia ni kuufanya mfuko huu uwe endelevu. Mfuko huu utakuwa endelevu hasa ikiwa watu wachache sana wataugua. Mtu akiugua basi ataweza tumia pesa toka katika mfuko wao, na mara nyingi wale wanaoumwa hutumia pesa zaidi ya zile walizowahi changia katika mfuko. Hii inamaanisha kama ana magonjwa sugu kama Kisukari au shinikizo la damu n.k. atakuwa akitumia pesa zaidi ya anachochangia na hivyo anatumia pesa ya mtu mwingine ambaye haumwi. Wote mkiumwa ndani ya mfuko huu, mtaua mfuko; kwani matibabu huwa ni gharama zaidi ya kile tunachochangia.

Ninaweza sema kwa sehemu ndivyo baadhi ya mifuko ya bima kama NHIF inavyofanya kazi.

Serikalini, watumishi wanakatwa nadhani ni asilimia 3 (yaani 3%) ya jumla ya mshahara ili kuchangia kwenye mfuko. Mfano kama mtu anapata laki 7 kwa mwezi ina maana atakatwa 21,000/= kila mwezi. Inawezekana huyu mtu ana mke au mume au mtoto au mzazi ambaye ni tegemezi ambaye ananufaika na makato yake ya kila mwezi. Hebu fikiria huyu ndugu ana baba na mama wenye shinikizo la damu na kisukari. Kila mmoja kila mwezi anatumia dawa za zaidi ya lakini na nusu, sawa na zaidi ya laki tatu kwa wazazi wawili. Hapo hujazungumzia vipimo mbalimbali anavyofanyiwa kila baada ya muda fulani. Gharama za matibabu za baba na mama ambao ni tegemezi kwa mwaka zinazidi 3,600,000/=. Lakini michango yake kwa mwaka ni 252,000/= pekee. Je, pesa ya ziada inatok wapi? Inatoka kwa wachangiaji wengine wasiougua.

Nimeona vifurushi vipya vya NHIF kwa wasio watumishi. Mfano katika kifurushi cha Najali Afya Premium kwa mtu binafsi unachangia 192,000/= kwa mwaka. Kuna vipimo kadhaa vinaweza vikafanywa kwa kifurushi hiki (na gharama zake halisi ambazo NHIF huzilipa hospitali kwenye mabano, nimeorodhesha vichache): X-Ray (15,000/=), ECHO (40,000/=), EEG (sifahamu bei yake), Ultrasound nyingine zaidi ya ile ya moyo (15,000/= na zaidi), kuna vipimo vya maabara takribani 162 (gharama zake ni zaidi ya 600,000/=). Kuna baadhi ya vipimo kama CT scan (150,000 na zaidi), MRI (zaidi ya 250,000/=) havimo katika hiki kifurushi.

Ukiangalia manufaa atakayopata mtu akiugua kwa kifurushi cha Najali Afya Premium yanazidi maradufu michango yake. Sasa je, akiumwa pesa za ziada hutoka wapi? Hutoka kwa wachangiaji wengine. Unaweza jiuliza kwanini baadhi ya vipimo vimeondolewa? Nadhani mantiki ni ileile, kwamba kifurushi hiki kimefanywa kiwe cha gharama ndogo kwa sababu kina mfaa mtu mwenye hatari ndogo ya kuugua, kama mtu anahisi ana hatari kubwa ya kuugua basi anapaswa achague kifurushi cha juu. Kifurushi hiki kinafanana na bima ndogo ya gari, ila kama unataka kuwa na bima nzuri basi utakata comprehensive insurance ingawa nayo ina masharti yake pia.

Kitu kinachopaswa kiondoke katika vichwa vyetu Watanzani wengi ni kwamba tusikate Bima tukiwa na nia ya kutumia pesa tulizokatia bima. Bima iwe kama mlinzi wa nyumba. Kwa wale wenye uwezo huweka mlinzi majumbani au kwenye shughuli zao za biashara. Sijawahi ona mtu aliyemweka mlinzi nyumbani analaani kutoibiwa. Sijawahi ona mtu anamfukuza mlinzi kwa sababu toka amweke mlinzi hajawahi ibiwa. Kama una mlinzi unafurahi huibiwi, lakini wakitokea wezi basi watakutana na mlinzi bila kujali matokeo ya kuvamiwa.

Mantiki za kufaidi kwa kila mchango tunaotoa si sawa. Wengine wanachukia kutoa michango ya misiba kwa wenzao kila siku. Wanataka ati na wao wafiwe. Sawa utafiwa na mtu wa karibu na hata huo mchango hautakufariji.

Nashauri watanzania (wasiokatwa kisheria) tuchague vifurushi kulingana na mahitaji yetu. Lakini pia tiache tabia ya kujiunga na mifuko ua bima ya afya pale tu tunapokuwa na ndugu wagonjwa. Ikiwa kila mtanzania angejiunga na mfuko wa bima ya afya gharama zingekuwa chini kwa sababu tungekuwa tuna share risk chache katika pool.
 
kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
3,953

Mkuu umetoa elimu nzuri hongera sana
Lakin hata kwa wagonjwa wenye bina NHIF na iCHF bado mnakutana na changamoto ya kiprofesional hasa pale unapotaka kutumia utaalamu wako kumtibu unakumbana na bei elekezi ya dawa na vipimo. Maana usipofuata mwisho wa siku claims zenu zitafyekwa na NHIF
 
Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
6,915

Moja ya majukumu ya serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya njema. Hivyo pamoja na kuhimiza michango ya bima ya afya pia serikali ina wajibu wa kuchangia pale wananchi wanaposhindwa.

Ni ukweli usiofichika kuwa magonjwa haya ambayo serikali inakwepa kusaidia hayaambikizi ndiyo sababu inaona kila mtu afe kivyake. Kama magonjwa haya yangekuwa yanaambukiza kama kufua kikuu serikali ingesaidia kimatibabu kwa kuhofia kupoteza nguvu kazi kubwa. Mbona kwa magonjwa haya haya serikali inawagharimia viongozi, kwa nini ishindwe kwa wananchi?
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,952

nhif hawana nia ya kumsaidia m Tanzania.. wana nia ya kupata faida kama wafanyabiashara binafsi
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,952
2,000
Moja ya majukumu ya serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya njema. Hivyo pamoja na kuhimiza michango ya bima ya afya pia serikali ina wajibu wa kuchangia pale wananchi wanaposhindwa.

Ni ukweli usiofichika kuwa magonjwa haya ambayo serikali inakwepa kusaidia hayaambikizi ndiyo sababu inaona kila mtu afe kivyake. Kama magonjwa haya yangekuwa yanaambukiza kama kufua kikuu serikali ingesaidia kimatibabu kwa kuhofia kupoteza nguvu kazi kubwa. Mbona kwa magonjwa haya haya serikali inawagharimia viongozi, kwa nini ishindwe kwa wananchi?

huu ni ukweli, serikali ni wajibu wake kuhakikisha wananchi wake wana afya.. sio mtu akiumwa figo, kansa au moyo unamkataaa.. huku hela zake za bima unazichukua
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom