NHIF kwanini tusijiunge bima kama tunavyokata za magari?

Mitsubish

Member
Apr 26, 2018
85
125
Kuna urasimu mkubwa pindi mtu (individual) unapotaka kujiunga na huduma za mfuko wa bima ya afya.

Wao siku zote husisitiza watu wajiunge kwa bei nafuu yaani chini ya laki moja, lakini ukisema ufuatilie serious ukifika ofisi zao Kurasini utarudi mbio baada ya kutajiwa gharama kubwa hata milioni mbili.

Wao watakushauri muende kama kikundi
hivi watu wa NHIF mkiamua tujiunge na mfuko wenu na tukalipia hiyo elfu 80 ya mwaka kama tunavyolipia bima za magari kutakua na tatizo gani?

Tunaomba mturahisishie ili wengi tujiunge na nyie mpate wateja na faida kubwa kulikoni hali ilivyo sasa ambapo wengi wanashindwa kutokana na gharama kubwa.

Hongereni kwa kufanikisha afya Toto card sasa rahisisheni na kwetu watu wazima.

Nawakilisha.
 
Who Cares?

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
3,517
2,000
Mleta mada you are genious mannnnnn.....tatizo hawako market oriented. Walivyokuwa wapuuzi utaskia NHIF INAUZA HISA ILI KUKUZA MTAJI ...hisa moja tsh 120....unachoka kabisa. Wala hata isiwe tsh elf 80...wafanye hata laki 2...kwa mwaka.kila myu akate bima yake kuliko hayo ma milioni.
 
shin gun wook

JF-Expert Member
Sep 26, 2017
984
1,000
nafikiri watajirekebisha kwa ili maana mwanzo ata individual ilikua hawakati bima kutokana na kuaepo kwenye ugumu wakujua income yako ,ilikua kwa wafanyakazi kwa kua ni regular income,wao kila mwenzi kukata chai kutokana na kipato chako
 
kubwa_Lao

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
934
1,000
Mie nililifikiria hilo, nikawapongeza pia kwenye toto card.....
Yaani wanamuokoa mtoto halafu wanamuacha mzazi afe kwa mgonjwa mtoto abaki yatima, maana kama hujamuokoa na mzazi hata hiyo toto card sijui itapatikana wapi
 
kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,332
2,000
nafikiri watajirekebisha kwa ili maana mwanzo ata individual ilikua hawakati bima kutokana na kuaepo kwenye ugumu wakujua income yako ,ilikua kwa wafanyakazi kwa kua ni regular income,wao kila mwenzi kukata chai kutokana na kipato chako
Wafanyakazi wengi wanakatwa kuanzia kati ya laki mbili hadi milioni 2 kwa mwaka kwa mtu mmoja.
Wafanyakazi hao hao wanalipa kodi kati ya laki nane hadi milioni milioni tano kwa mwaka tena hawa naongelea wa serikali.
Ni kwa nini wafanya biashara mnataka mbebwe na mfanyakazi ambaye mwisho wa mwezi tu utasikia anaulizia mshahara kama umetoka,na ninyi mnakuwa wa kwanza kumzodoa?Ni lazima kila mtu atimize wajibu wake vizuri na si kutegemea kuwanyonya wafanyakazi
 
KIOO

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
6,136

Wee kweli kibaravumba.
 
GSS

Member
Mar 13, 2018
22
45
Ukisema bima ikatwe kama Magari basi itabidi sheria zirekebishwe kwa sababu sisi wafanyakazi tunabeba mzigo mkubwa sana,sisi tunakatwa kila mwezi,lakini sheria zikibadilishwa hilo linawezekana sana
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
54,615
2,000
Wazo zuri sana...

Matatibu ni gharama sana, hususan pale unapohitajika kutoa pesa nyingi kwa wakati mmoja...

Ila ukiwa na Bima ya afya unafuu mkubwa unakuwepo...

Cc: mahondaw
 
tru rasta

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
302
500
Ukisema bima ikatwe kama Magari basi itabidi sheria zirekebishwe kwa sababu sisi wafanyakazi tunabeba mzigo mkubwa sana,sisi tunakatwa kila mwezi,lakini sheria zikibadilishwa hilo linawezekana sana

Wewe kama mfanyakazi unakatwa kiasi gani na nhif mpaka ulalamike?kwenu hii huduma si ni mchekea kabisa,acha kufuru
 
Tissaphernes

JF-Expert Member
Mar 27, 2018
2,429
2,000
Wafanyakazi walioajiriwa hukatwa 3pc na mwajiri hukatwa 3pc

Kuna bima ya vikundi vilivyosajiliwa ambapo kila mwanachama hulipia 76-79000 kwa mwaka .
Bima binafsi ni 1500400 kwa mwanachama 1 mwenye wategemezi 5 (mke/watoto wa kuwazaa 4/ wakwe)

Ukitaka jua 1.504 ni ndogo kwa watu sita acha uugue kwa mwezi ndio utajua umuhimu wa bima
 
GSS

Member
Mar 13, 2018
22
45
Wewe kama mfanyakazi unakatwa kiasi gani na nhif mpaka ulalamike?kwenu hii huduma si ni mchekea kabisa,acha kufuru
Kiasi ninachokatwa ni kikubwa sana kwa mwezi na ukipiga hesabu kwa mwaka ndio nagundua mzigo ni mkubwa sana
 
onduru ogy

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
1,133
2,000
Nimegundua wananchi hasa hawa wanaodai ni wafanyakazi hapa jf na mtoa huduma ya Bima hasa hiyo ya NHIF wote hawajui maana ya bima.

Bima ya afya mtu anaweza kukata hata ya miezi mitatu, miezi sita, mwaka nk kutegemea na anavyotaka
Mtoa mada achana na waliolala hao NHIF tafuta zako kampuni ya bima inayojitambua wanaofanya biashara utakata bima unayotaka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom