NHIF Kwa nini Bima yenu hailipii kipimo cha Dengue??

mliverpool

JF-Expert Member
Jan 6, 2015
1,507
2,832
Jana baada ya futari nilikuwa najisikia vibaya joto lilipanda ghafla na baridi Kali likawa linaniandama

Asubuhi leo nimeamkia hospitali fulani hivi huku maeneo ya Temeke Dr. kaniambia miongoni mwa vipimo atakavyonipima ni pamoja na Dengue

Sasa kimbembe Dr akasema bima haiwez kulipa hivyo niingie mfukoni, kipimo chenyewe gharama 40,000/-

Kuna haja gani ya kuwa na bima kama haiwez kulipa kipimo?? Mm niliamua kulipa japokuwa Kwa shingo upande Ila Vipi wazee wetu huko kijijini tulilowakatia bima??

Hii ni bima ya serikali lakn inaongoza Kwa ubabaishaji, halafu Kwa sisi watumishi wanatuambia kujiunga no lazima, si Bora iwe huru ishindane tuamue wenyewe pa kwenda??

Hivi waziri na wahusika wa afya wanalitambua hili?? Au Sisi wananchi tumekuwa wapole Sana kiasi kwamba wanatupeleka wawezavyo?? Tupaze sauti dhidi ya huu udhalimu,
 
Dengue ni ugonjwa wa mlipuko ambao haukuwepo kwenye kundi la magonjwa sumbufu katika maeneo ya wanufaika wa bima, vipimo vya dengue havipo katika orodha isipokuwa kama ugonjwa utaendelea kuwepo kwa muda mrefu, NHIF watalazimika kulipia gharama ya vipimo kwa wateja wao.

Nb: NHIF wanapaswa kuchukua hatua na kuweka vipimo vya dengue katika orodha yao ili kuwasaidia wateja na wanaonufaika na mfuko.
 
Jana baada ya futari nilikuwa najisikia vibaya joto lilipanda ghafla na baridi Kali likawa linaniandama,Asubuh leo nimeamkia hospitali fulani hivi huku maeneo ya Temeke Dr kaniambia miongoni mwa vipimo atakavyonipima ni pamoja na Dengue, sasa kimbembe Dr akasema bima haiwez kulipa hivyo niingie mfukoni,kipimo chenyewe gharama 40,000/- sasa inahaja gani ya kuwa na bima kama haiwez kulipa kipimo?? Mm niliamua kulipa japokuwa Kwa shingo upande Ila Vipi wazee wetu huko kijijini tulilowakatia bima??hii ni bima ya serikali lakn inaongoza Kwa ubabaishaji,halaf Kwa sisi watumishi wanatuambia kujiunga no lazima,si Bora iwe huru ishindane tuamue wenyewe PA kwenda?? Hivi waziri na wahusika WA wizara ya afya wanalitambua hili?? Au Sisi wananchi tumekuwa wapole Sana kiasi kwamba wanatupeleka wawezavyo?? Tupaze sauti dhidi ya huu udhalimu,

UFAFANUZI KUTOKA KWA WENYEWE
 

Attachments

  • TAARIFA KWA UMMA -DENGUE - 10 MEI 2019.pdf
    78.8 KB · Views: 35
Dengue ni ugonjwa wa mlipuko ambao haukuwepo kwenye kundi la magonjwa sumbufu katika maeneo ya wanufaika wa bima, vipimo vya dengue havipo katika orodha isipokuwa kama ugonjwa utaendelea kuwepo kwa muda mrefu, NHIF watalazimika kulipia gharama ya vipimo kwa wateja wao.

Nb: NHIF wanapaswa kuchukua hatua na kuweka vipimo vya dengue katika orodha yao ili kuwasaidia wateja na wanaonufaika na mfuko.
Na cha typhoid mbona hakipo mkuu
 
Back
Top Bottom