NHIF kwa hili hamtutendei haki Toto afya card

Hili hata mimi limenitokea nilichelewa ku renew kadi ya mtoto wameniambia mpaka mienzi mitatu ndio itafanya kazi tena

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Wanachofanya si sawa badala ya kujikita kwenye huduma kusaidia watu wao wanalenga ki biashara
Mimi ninalipia watoto wawili nalipa laki moja hunipi huduma ati hadi siku 90 pesa wanachukua hii sio kabisa
 
... lengo ni kuhakikisha hakuna anayekimbilia kukata bima baada ya tatizo la ugonjwa kutokea; sio utaratibu wa bima yoyote huo. Risks ndizo zinakatiwa bima na sio issues. Ajali ya gari imeshatokea ndio unaenda kukata bima, sivyo bima ilivyo! Unatakiwa uikate kabla ya ajali yaani wakati huna uhakika kama ajali itatokea au haitatokea.

Ikiruhusiwa bima (NHIF au mfuko mwingne wowote) zikatwe baada ya ugonjwa kutokea mfuko utafilisika kwa sababu kila mtu ataenda kukata bima baada ya kujiridhisha kuwa ni mgonjwa. This means atakacholipa ndicho kitakachotumika kumtibu na pengine huenda kisitoshe unadhani sustainability ya mfuko itakuwaje?

Sustainability ya bima ya afya inataka wagonjwa wawe wachache sana kuliko wazima. Wanachama wazima wasiougua mara kwa mara ndio husaidia ku-top kwa wengine wagonjwa wa mara kwa mara na gharama nyingine za uendeshaji wa mfuko including mishahara, kodi, n.k.

Logic yake ndio hiyo!
Umeeleza vizuri Sana mkuu
 
Nilikata ya mwanangu 2018 Ilikuwa inachukua Siku 21 tu.
Mwaka huu Nikaenda kumkatia mwingine ndio nikakuta hayo mabadiliko lakini kwenye kuhuisha(renew) iliyoisha nlipata ndani ya siku 7.

Naelewa mantiki ya kuweza muda mrefu Kwa wateja wapya lakini miez mitatu ni mingi Sana, angalao miezi miwili inatosha
 
Back
Top Bottom