NHIF itangaze kama inatoa huduma ya mitungi ya gas (oxygen)

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,580
4,262
Kutokana na ongezeko la mahitaji ya gasi ya Oxygen yaliyojitokeza hivi karibuni umekuwa na mkanganyiko mkubwa wa huduma hasa hiyo gas ya oxygen inayotumika kwa wingi
Ukiangalia kwenye matangazo ya NHIF yanasema hiyo gasi inatolewa Bure. Ila kiuhalisia hiyo gasi inauzwa kwa hospitali za serikali na zile za Binafsi
Ninacho omba
Kuwe na maelekezo yatakayo bandikwa hospitali zote kubwa yanayo elekeza huduma zinazotolewa na Bima kwenye hii changamoto ya Uviko 19; kwa hili la gas,
1. NHIF iseme wazi kuwa italipia gasi ya Oxygen
2. Na kama wanalipia kiasi mfano chupa 5 kwa mgonjwa mmoja, pia waseme wazi wazi
3. Na kama hawalipii kabisa pia waseme wazi wazi
4, Ingependeza kama kungekuwa na bei Elekezi ya hii mitungi kwani hii ni huduma muhimu inayogusa watu wengi
Bila hivyo wanachi wanatozwa hela kwa kuwa hakuna muongozo ulio wazi, Lakini pia NHIF italipia hiyo hiyo mitungi ambayo mwananchi ameshalipia
 
Nina shemeji yangu yupo Ntyuka hospital ana kadi ya NHIF, oxygen ni mwendo wa kupasua mfuko tu. Hayo matengazo ni usanii mtupu.
 
Mtungi mmoja wa gesi ni 30,000, unaweza kukuta mgonjwa anahaitaji mitungi 3 - 5 kwa siku...na haipo kwenye bima, haya mambo yasikie tu kwa wengine...ila chanjo ni bure, kwa hiyo kupanga ni kuchagua !
 
Mtungi mmoja wa gesi ni 30,000, unaweza kukuta mgonjwa anahaitaji mitungi 3 - 5 kwa siku...na haipo kwenye bima, haya mambo yasikie tu kwa wengine...ila chanjo ni bure, kwa hiyo kupanga ni kuchagua !
Kule Arusha (Mt Meru Referral) wanachaji shs 50,000 kwa mtungi, yaani inatia huruma. Ndio sababu nimepekeza kuwe na bei elekezi
 
Back
Top Bottom