NHIF inachangia kuua Huduma za Afya kwa kutolipa madeni ya Hospitali

Ndokeji

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
698
475
Shirika letu la Bima (NHIF) limechangia kuua Huduma za Afya katika kulipa Madai ya Hospitali zetu kwa kuchelewesha kulipa kwa wakati, ambapo hospitali zote nchini zimekuwa zikilamika kuchelewesha malipo hayo ili ziweze kununua dawa,vifaa tiba na kulipa uendeshaji wa hospitali

NHIF imekuwa na tabia ya kukopesha hospitali kwa mda wa miezi mitano(5) kitu kinachopelekea hizi hospitali kuwambia wagonjwa kujinunulia vifaa na dawa ili waweze kutibiwa hali hii imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi, na kwa kiwango cha wananch wanaotumia Bima ni zaidi ya 70 %. Na Taifa linakoelekea watu wengi watajiunga na Bima, Hili shirika lispokuwa na Mipango mikakati linaenda kuua Sekta ya afya

Ushauri
- Kuwepo na sheria ya kulipa claim za tasisi na Hospitali kulipwa mapema not more than 2 month
-Uongozi uliopo ufumuliwe ni kero
  • Makato ya ovyo yaangawe upya
  • kuwepo na specialist Mabingwa wenye kukagua ujazaji wa formu za NHIF siyo MD
- Kuwepo na Mfumo wa moja kutoka hospitali mpaka kwenya kitengo
 
Mbali na kuchelewesha malipo, pia wamekuwa na tabia ya kutolipa kabisa hayo madeni iwapo Form haikujazwa vizuri. Wawe na utaratibu wa kuchunguza au kuwapigia simu hao wafanyakazi kujua kama ni kweli wamepata hayo matibabu kisha walipe hayo madeni.

Mgonjwa kashapata matibabu halafu Bima wanagoma kulipa kwa sababu nyepesi tu hiyo hali inafanya wale wanaolipia Cash wathaminiwe kuliko wateja wao wa Bima.
 
Tutashauri bodi iondoshwe wakishindwa kurekebisha hiyo hali,kwa mazoea waliyoyapata kipindi cha hivi karibuni.
Bodi hii ni ovyo kabisa sijapata kuona, imekuwa haina msaada zaidi ya kujilipa wenyewe
Nenda katembelee hospitali mpaka unatamani hivi huu mfuko unasaidiaje hizi hospitali, Mteja anapata huduma wao wanakuja kukagua form na kutofauta makosa madogo madogo na kukata yaani ni bora waunde bodi mpya yenye mkakati wa kusaidia hii tasisi wateja wao na hosipitali zinazotoa huduama
Wewe mpaka inafika NHIF inadaiwa bil 10 haijalipa na taasisi moja sijui wanawaza nini juu uendeshaji wa taasissi hiyo
 
Mbali na kuchelewesha malipo, pia wamekuwa na tabia ya kutolipa kabisa hayo madeni iwapo Form haikujazwa vizuri.

Mgonjwa kashapata matibabu halafu Bima wanagoma kulipa kwa sababu nyepesi tu hiyo hali inafanya wale wanaolipia Cash wathaminiwe kuliko wateja wao wa Bima.
Sababu zenyewe hazijulikani
 
Shujaa aliharibu kila kitu nchi hii,sina cha kumsifia.
Na huu ndio ukweli. Kama aliyoiua NFRA ndivyo hivyo alivyotaka kuua NHIF.

Ruzuku waliyokuwa wanapewa NHIF ilikatishwa, mfuko ukayumba.

Yaani matumizi ya wachangiaji yalikuwa makubwa kuliko pesa zinazokusanywa na NHIF kutoka kwa wachangiaji.

Kilichofuata ndio hicho. Na ili kuunusuru mfuko kina Anna Makinda wakaamua kuunda vifurushi vipya ambavyo mpaka leo kila mchangiaji analalamika!

Magonjwa mengi wameyaondoa, kima cha chini cha uchangiaji wamepandisha yaani ni zig zag.

Magu alikuwa shetani kabisa.
 
Shirika letu la Bima (NHIF) limechangia kuua Huduma za Afya katika kulipa Madai ya Hospitali zetu kwa kuchelewesha kulipa kwa wakati, ambapo hospitali zote nchini zimekuwa zikilamika kuchelewesha malipo hayo ili ziweze kununua dawa,vifaa tiba na kulipa uendeshaji wa hospitali

NHIF imekuwa na tabia ya kukopesha hospitali kwa mda wa miezi mitano(5) kitu kinachopelekea hizi hospitali kuwambia wagonjwa kujinunulia vifaa na dawa ili waweze kutibiwa hali hii imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi, na kwa kiwango cha wananch wanaotumia Bima ni zaidi ya 70 %. Na Taifa linakoelekea watu wengi watajiunga na Bima, Hili shirika lispokuwa na Mipango mikakati linaenda kuua Sekta ya afya

Ushauri
- Kuwepo na sheria ya kulipa claim za tasisi na Hospitali kulipwa mapema not more than 2 month
-Uongozi uliopo ufumuliwe ni kero
  • Makato ya ovyo yaangawe upya
  • kuwepo na specialist Mabingwa wenye kukagua ujazaji wa formu za NHIF siyo MD
- Kuwepo na Mfumo wa moja kutoka hospitali mpaka kwenya kitengo
Watalipa na nini wakati pesa yote mmepeleka kujengea miradi mnayoita ya kimkakati?
 
Back
Top Bottom