NHC, mama Tibaijuka wapongezwe kwa hili wanalofanya?

MBURE JASHA

JF-Expert Member
May 7, 2011
200
46
nimekuwa mfuatiliaji wa habari katika TV station mbalimbali hapa nchini. Kuna habari muhimu inakosa coverage katika magazeti nimeona leo metoka kwenye gazeti la NIPASHE . Ni kuhusu hili sakata la ofisi za serikali kufukuzwa kwenye nyumba na NHC. Juzi walikuwa Wizara ya KCU na Vijana na Michezo leo sijui watakuwa Lithui Upanga au vipi!
Swali: Je tuwapongeze hawa watu wanaoendesha operesheni hii kwa maana mama Tibaijuka na NHC!
Je Nguvu hii pia ipo kwa wahindi waliojazana kwenye majumba mbalimbali ya NHC Tz nzima?
Je utendaji huu unapaswa kuigwa na wizara nyingine?
 
smz

JF-Expert Member
Dec 18, 2010
249
32
Ni aibu kwa serikali kudaiwa mamia ya mamilioni kama limbikizo la kodi ya pango.

Kama serikali ambayo ndiyo inayotakiwa kuya inua mashirika ya umma inadiwa kiasi hiki maana yake nini?? Jana tuliona kupitia ITV wizara ya "Dr" Nchimbi inatolewa nje kwa aibu namna hiyo, hii inatupa picha gani.

Hii isije ikawa nguvu ya soda, naomba NHC wapite kwa kila wanayemdai pango na wafanye kama walivyofanya jana pale wizara ya Nchimbi. Waendo kote pale DSM na mikoani kote.

Naamini NHC ina mipesa ya kumwaga imekaliwa na serikali na wapangaji wengine sugu wasiolipa kodi. Mama Tiba usirudi nyuma sana sana naomba Saidi Mwema akupe ulinzi wa uhakika wakati wa kutekeleza zoezi hili usije ukadhuliwa wewe na vijana wako.

Naomba kuwasilisha, na ninaunga mkono hoja asilimia 100 kwa mia. Tena nimesahau nilitakiwa kuunga mkono kwanza kabla ya kujielekeza kwenye hoja yenyewe. Hii inanikumbusha wah. wabunge wa CCM pale mjengoni. Hivi wanarudi mwezi gani vile??
 
Bigaraone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
723
351
Hakuna sababu yae kuwapongeza maana ndio wajibu wao. Wameajiriwa kufanya kazi hiyo. What they are in t doing should bue an ingredient in their core values. Halafu nidugu zangu Watanzania tujihadhari sana na pongezi kwa tuukio moja na la siku moja. Tuache siasa kwenye mambo muhimu na tujifunze na makosa. Nitatoa mifano michache ambayo inaonyesha ni jinsi gani tuna ugonjwa wa kusahau.

1.Hotuba ya JK ya kwanza kama rais aliyoitoa bungeni. Nijuavyo haikuwa yake iliandaliwa na Maprofesa wa UD na yeye akaisoma kwa mbwembwe kama yake.Mazuri ndani ya hotuba ile hayakuwahi na hayatahi yatekelezwe.

2. Kashifa ya wizi wa benki kuu maarufu kama EPA. Huu iliwekwa hadharani na Mheshimiwa, ndugu, mzalendo wa karne Dr.Slaa. Hii ni baada ya kukataliwa na aliyekuwa spika wa bunge Samweli Sita- mnafiki mwingine anahitaji thread yake. Rais JK naye alimbeza Dr. Slaa lakini penye ukweli uongo ujitenga. Wafadhili walipotishia kutunyima misaada Kikwete alizinduka usingizini kuajiri auditingi Ernest & Young kufanya ukaguzi nao wakaja na report inayotuhumu BOT na wakwapuaji. Rais na serikali yake wakaivalia njuga, akatoa ombi wezi warudishe pesa. Kilichofatia na ambacho tunaendelea kukiona na aibu na fedheha maana hakuna sentu iliwarudishwa. LAKINI kikubwa ni kwamba watu wazima walishangilia kila alichokuwa akisema JK na serikali yake kabla na baada ya kujifanya kuwa naye anakerwa na wizi wa BOT kumbe jana alisema ni uzushi . Lakini hata baadhi ya viongozi wa upinzani nao walitokea kumpongeza.

3. Kushitakiwa kwa Mramba, Yona na Mgonja-watu wazima wamepongeza. Aliyaamuru washtakiwe ni yule yule alikwenda kumpigia debe mrembe kwenye arakati za kuwania ubunge. Thank God, Mramba aliambulia patupu. Wachagga wana akili maana waliuliza wewe unasema huna kashifa, vema. Aliyekushtaki ndiye anakuja kutusanii anakufananisha na msumeno wa zamani. Sasa nenda akupe ubunge mwenyewe.

Ndugu zangi litania ni ndefu lakini itoshe kusema kuwa hakuna haja ya pongezi wala shukrani maana NHC na Waziri Tibaijuka wanachofanya ni wajibu wao na wanalipwa kwa sababu hiyo na ni tukio moja kati ya mengi ambayo tungetaraji na hivyo tujihadhari na pongezi maana zinalevya na watawala tukiwasifu wantuona mazezeta
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
nimekuwa mfuatiliaji wa habari katika TV station mbalimbali hapa nchini. Kuna habari muhimu inakosa coverage katika magazeti nimeona leo metoka kwenye gazeti la NIPASHE . Ni kuhusu hili sakata la ofisi za serikali kufukuzwa kwenye nyumba na NHC. Juzi walikuwa Wizara ya KCU na Vijana na Michezo leo sijui watakuwa Lithui Upanga au vipi!
Swali: Je tuwapongeze hawa watu wanaoendesha operesheni hii kwa maana mama Tibaijuka na NHC!
Je Nguvu hii pia ipo kwa wahindi waliojazana kwenye majumba mbalimbali ya NHC Tz nzima?
Je utendaji huu unapaswa kuigwa na wizara nyingine?

Kama wameweza kwa serikali, mhindi ni nani hata anusurike? Lakini si mpaka hao wahindi wawe wana arrears ndipo rungu liwaangukie?

Hawa wanastahili pongezi za uhakika.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,879
9,832
nimekuwa mfuatiliaji wa habari katika TV station mbalimbali hapa nchini. Kuna habari muhimu inakosa coverage katika magazeti nimeona leo metoka kwenye gazeti la NIPASHE . Ni kuhusu hili sakata la ofisi za serikali kufukuzwa kwenye nyumba na NHC. Juzi walikuwa Wizara ya KCU na Vijana na Michezo leo sijui watakuwa Lithui Upanga au vipi!
Swali: Je tuwapongeze hawa watu wanaoendesha operesheni hii kwa maana mama Tibaijuka na NHC!
Je Nguvu hii pia ipo kwa wahindi waliojazana kwenye majumba mbalimbali ya NHC Tz nzima?
Je utendaji huu unapaswa kuigwa na wizara nyingine?

Mkuu majibu ya maswali yako yote ni NDIYO. NHC wanafanya kazi inayoonekana kwa macho na kusikika kwa masikio!! Serikali ina dhihaka kubwa, wizara hazilipi pango wala bili za umeme, simu, nk. KAma unakumbuka walipokuja jamaa wale jamaa waliokodishwa kuiendesha (Sijui nini Soluation) walionekana wamekusanya pesa nyingi kumbe walikuwa wakikusanya madeni ya TANESCO toka serikalini na vyombo vyake. Watendaji wengi wa mashirika ya umma wamekuwa wakiziogopa wizara za serikali lakini sasa NHC wameamua na kusema si hadi tukawakodishe makaburu kuja kuziadabisha idara za serikali bali hata sisi tunaweza!! Big UP NHC hasa Mkurugenzi wake Mkuu Ndg. MCHECHU.
 
Mat.E

Member
Dec 28, 2010
66
13
Wakuu nakanyaga jukwaani kwa mara ya kwanza, nipokeeni.
Moja wapo ya majukumu ya waziri yeyote ni kusimamia sheria na taratibu zilizopo. Tibaijuka ni wajibu wake kufanya anavyofanya, ni kutekeleza majukumu yake. Kuwafukuza ni jambo moja, deni kulipwa ni jambo jingine. Tusubiri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom