NHC hatimaye imejikita kwenye biahsara kisawasawa

Dodoma Demand

Senior Member
Oct 6, 2021
130
74
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza mradi mkuwa wa ujenzi wa Fremu za Biashara 6,000 mkoani Dodoma ambazo zinatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2024.

Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dkt. Maulidi Banyani, kwenye ziara ya kukagua na kutembelea maeneo zinapojengwa Fremu hizo za biashara zilizopo Nara na Nkuhungu, amesema mradi huu unajengwa katika awamu tatu, awamu ya kwanza zinajengwa Fremu 2400 ambapo Fremu 1300 zitakuwa Nara na Nkuhungu Fremu 1100, awamu ya pili itahusisha Fremu 2000 na awamu ya tatu Fremu 1600.

Adha, Dkt. Banyani amesema Fremu 3000 zinajengwa kwa mtindo wa ghorofa wilayani Nkuhungu na zitapangishwa kwa wafanyabiashara, wananchi na taasisi mbalimbali huku 3000 zinazojengwa Nara ni kwa ajili ya kuuzwa kwa njia za makato na kushirikisha banki za kibiashara.

Akifafanua zaidi Dkt. Banyani amesema mradi huu unajengwa kwa msaada wa Serikali ambayo ililikopesha Shirika mkopo nafuu wa Sh. Bilioni 120 na Shirika likatoa Sh. Bilioni 14.3 na kufanya jumla ya gharama ya mradi huo kufikia Sh. Bilioni 164.3.

Amesema mradi wa nyumba za Nkuhungu umefikia zaidi ya asilimia 24 na mradi wa Nara wa Fremu 3000 umefikia asilimia 35, miradi hii inatarajiwa kufikia mwezi Novemba shirika litaanza mchakato wa mauzo.

Akizungumzia bei, amesema kuwa Fremu 3000 za Nara zitauzwa bei fedha taslimu ama kwa makubaliano na mabenki kwa gharama ya kati ya Sh Milioni 20 - 34 kutegemeana na ukubwa wa Fremu na eneo huku pia kukiwa na maeneo ya mapumziko. Lengo ikiwa ni kuanza kutumia ifikapo mwezi Julai mwakani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa NHC, Haikamen Mlekio amesema kuwa kampuni imejiongeza katika maeneo yote mawili Nara na Nkuhungu kwa kununua mashine 50 za kutengeneza matofali ambazo zimeajiri vijana 160 ambao wana uwezo wa kutengeneza matofali 70,000 kwa siku, kitendo hicho kimeimarisha ubora wa matofali wanayotumia na kupunguza gharama ununuzi kutoka kwa watu binafsi.

images.jpg

1687434_frempic.jpg
 
Wakitaka kuziuza kweli hizo nyumba waweke bei rafiki kwa hata wenye kipato cha wastani,wakiweka bei zao za ajabu zitadoda.

Wasitake faida kubwa sanaa,waweke kiasi ya kuwezesha shirika kujiendesha na hapo ndipo bei zitakapokuwa ni za kawaida
 
Hivi nyumba huwa wanauziwa akina nani? uuzaji wake umejaa rushwa rushwa
Rushwa ndio inayotakiwa duniani!? Maana mahitaji ni mengi kuliko Fremu zenyewe vile vile husaidia KWENYE KUJUA SURA ZINAZOTAKIWA KUMILIKI MALI!? MAANA NYWEWE ZA RASI ZILITUMIKA KUJENGEA GOROFA
 
Na Muda kidogo amfiriro inakua Kama ina mawaa,ingawa kwny utekekezaj wa kikanda udhuhuri hapo Ni uchumi tegemezu,karikiti na half hour ago.
 
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza mradi mkuwa wa ujenzi wa Fremu za Biashara 6,000 mkoani Dodoma ambazo zinatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2024.

Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dkt. Maulidi Banyani, kwenye ziara ya kukagua na kutembelea maeneo zinapojengwa Fremu hizo za biashara zilizopo Nara na Nkuhungu, amesema mradi huu unajengwa katika awamu tatu, awamu ya kwanza zinajengwa Fremu 2400 ambapo Fremu 1300 zitakuwa Nara na Nkuhungu Fremu 1100, awamu ya pili itahusisha Fremu 2000 na awamu ya tatu Fremu 1600.

Adha, Dkt. Banyani amesema Fremu 3000 zinajengwa kwa mtindo wa ghorofa wilayani Nkuhungu na zitapangishwa kwa wafanyabiashara, wananchi na taasisi mbalimbali huku 3000 zinazojengwa Nara ni kwa ajili ya kuuzwa kwa njia za makato na kushirikisha banki za kibiashara.

Akifafanua zaidi Dkt. Banyani amesema mradi huu unajengwa kwa msaada wa Serikali ambayo ililikopesha Shirika mkopo nafuu wa Sh. Bilioni 120 na Shirika likatoa Sh. Bilioni 14.3 na kufanya jumla ya gharama ya mradi huo kufikia Sh. Bilioni 164.3.

Amesema mradi wa nyumba za Nkuhungu umefikia zaidi ya asilimia 24 na mradi wa Nara wa Fremu 3000 umefikia asilimia 35, miradi hii inatarajiwa kufikia mwezi Novemba shirika litaanza mchakato wa mauzo.

Akizungumzia bei, amesema kuwa Fremu 3000 za Nara zitauzwa bei fedha taslimu ama kwa makubaliano na mabenki kwa gharama ya kati ya Sh Milioni 20 - 34 kutegemeana na ukubwa wa Fremu na eneo huku pia kukiwa na maeneo ya mapumziko. Lengo ikiwa ni kuanza kutumia ifikapo mwezi Julai mwakani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa NHC, Haikamen Mlekio amesema kuwa kampuni imejiongeza katika maeneo yote mawili Nara na Nkuhungu kwa kununua mashine 50 za kutengeneza matofali ambazo zimeajiri vijana 160 ambao wana uwezo wa kutengeneza matofali 70,000 kwa siku, kitendo hicho kimeimarisha ubora wa matofali wanayotumia na kupunguza gharama ununuzi kutoka kwa watu binafsi.

View attachment 1974852

View attachment 1974853
Wawauzie sasa wapangaji flats za Ubungo zile za zamani.

Kuna jamaa wamezaliwa pale na sasa wamekua na wazazi wamefariki bado tu serikali inachukua kodi!

Wamechangia vya kutosha sasa wauziwe.
 
Vita ya HELA NYEPESI VS HELA NGUMU
 
Back
Top Bottom