Nguzo za umeme

lidoda

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
641
574
NGUZO ZA UMEME
Naombeni mnielimishe. Mbona ktk nchi za wenzetu mfano Japan na hata nchi kama za dunia ya tatu kama Sudan wanatumia nguzo za umeme za zege badala ya miti kama Tanzania? Nikitathimini tu gharama ya hizi nguzo, hata shilingi milioni mojakwa nguzo, hazi wezi kughalimu, na nizionavyo mimi ni za kudumu zaidi kuliko za kwetu Tanzania. Wenzangu sijui mna maoni gani juu ya hilo. Na kama nguzo za zege ni nafuu na za kudumu kwa nini tuendelee kutumia hizo nguzo za miti? Na kuna wakati TANESCO wali ishiwa na wakasema wameagiza kutoka Afrika ya kusini
 
Ata Tanzania nguzo za cement zipo,mfano ktk miradi yote ya wachina before 1990s.apa Dar urafika Textile zipo na bado zinapiga kaz.Tatizo la ufisadi apa Tanzania ndo sababu,mfano sasa hivi ata hizo nguzo zinatoka Sauz,za apa makambako wanasema azina ubora kwa sasa.bei ni mara 2 ya hizi za apa!.so watanzania wanaaangalia ULAJI na sio maslai ya Utaifa
 
Au qama vipi watumie hata za chuma kisichoshika kutu kama zile za askofu kakobe.
 
Mkuuu umeleta hoja nzuri sana na hii ni changamoto kwa tenesco na serikali,maoni yangu nguzo za cement ni bora kuliko hizi za miti,inabidi watu waimplement hii na maendelea yatakuja kwa kasi kuliko hizi ambao wanasema lazima zitoke kwao,Hii idea ni nzuri sana wanajamvi kwanini chadema/wanaharakati/wasomi walivalie nyuga ili liwe implemented hayo mambo ya miti ni wizi,pili si za kudumu
 
hoja nzuri sana hawa watu wanatuibia sana, wanatakiwa wakuletee umeme hadi kwako nguzo si
haki ya mteja kulipia kwani unachonunua kwao ni umeme na sio miundombinu cha kushangaza unalipia tena service line
wezi wakubwa zipo hele zinatengwa kwaajili ya huduma hizo mfano goba kule wamesambaza umeme
wa mradi kwa watu wengi garama inakuwa ya ww kuvuta tu.fanya kautafiti kadogo tu hakuna mfanyakazi wa tanesco maskini
labda awe mtakatifu.kwa vile ushindani wa kampuni zingine umeruhusiwa kutakuwa na mabadiliko makubwa ktk
usambazaji na uboreshaji wa miundo mbinu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom