Nguzo ya umeme ni mali ya Tanesco au Mteja anayeunganishiwa umeme? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguzo ya umeme ni mali ya Tanesco au Mteja anayeunganishiwa umeme?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by PrN-kazi, Nov 9, 2011.

 1. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tanesco wakitaka kumuunganishia mteja umeme, wanamtaka alipie nguzo kwanza kwa misingi ya kuinunua: na akisha ilipia inakuwa si mali yake tena bali ni mali ya Tanesco, dhana hii iko-je!!

  Swali limeulizwa Bungeni na Mh Regia (CHADEMA) na Mh. Ngereja(Waziri) kajibu kwamba Tanesco ndiyo wanaosimamia miundo mbinu kwenye nishati ya umeme hivyo hawanabudi kutoa nguzo pia swali limebaki: kwanini mteja anunue nguzo alafu isiwe mali yake?
   
 2. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Huo unaitwa Urasimu kazini,kwani hata hospitalini kunatakiwa dawa ziwepo ila unaambiwa hakuna ila hapo nje kuwa pharmacy zipo kanunue.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Na nyaya ni mali ya nani? Maana hili nalo ni swali lingine pia
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ni wizi mtupu
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Hiki kisa cha Abunuwasi. Hao ndio wabunge wetu, sasa mbunge anataka nguzo iwe ya mnunuzi ili siku akihama ahame nayo? Mnanchekesha.
   
 6. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  duh!!!! hili nalo ni neno.
   
 7. B

  Buza Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nafikiri sahihi ingekuwa angalau ukishanunua hiyo hela irudishiwe kwa kupewa units za umeme ili hiyo nguzo iwe halali kuwa ya tanesco.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Hii kitu surely it does not make any sense!! Sisi tulihamia mahali ambapo kulikuwa ni eneo jipya wakati huo tukanunua nguzo. Baada ya muda watu waliofuata wao walipewa umeme kupitia nguzo tlizozilipia sisi bila kuturefund part of our cost. Kwa ujumla hii ni dhuruma kwa mwananchi. Tanesco ao walitakiwa waunganishe umeme na kucharge gharama zao. Mwenye uwezo aunganishe asiye nao awashe kibatari kuliko kutwika mzigo kwa mtu mmoja na wengine kuponea huo. Idara ya maji wao wanautaratibu mzuri kidogo ingawa nao bado siyo fare kwa vile si kazi ya mteja. Ukinunua bomba la maji na mtu akaja kuunga kwenye bomba lako inabidi akufidie kidogo gharama zako.
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hii ndio tatizo la monopoly kwenye biashara. Lakini siku zao zinahesabika....wataanza kuona mteja ndiye mfalme na hizo nguzo watakuwa wanatoa bure pengine! Nani miaka ya 90 au kabla yake angeweza kudhania kama TTCL itakuwa ilivyo sasa(pamoja na kufisadiwa)? Tungekuwa na TTCL pekee bado mpaka leo hii simu ingekuwa ni suala la watu wachache wa mijini na wenye nazo!
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  unachekesha wewe unaeunga mkono hata wizi wa mchana kweupe
  nina mashaka na fikra zako
  Tanesco wanatakiwa kusambaza miundo mbinu hadi kwa mtejai ili wamuuzie umeme. hizo sera ni kwa kila nchi ndio maana kazi yaoni kuzalisha,kusambaza na kuuza lkn kwa vile kuna urasimu wizi na ulaghai kwa wateja unaambiwa ununue nguzo kwa zaidi ya milioni moja. Kwa akili hata ya kitoto nguzo inathamani hiyo? kwa vile makampuni mengine yameruhusiwa kuzalisha na kusambaza utaona ushindani mkubwa. YAANI UKISHAKUWA MAGAMBA HATA UKIAMBIWA UTAUZIWA SUKARI KG 1 KWA SH 10,000 UTAKUBALI TU KWA VILE MNA AKILI ZA KUCHEKESHA
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Wewe bibi FaizaFoxy ndo unachekesha sana,kwani wewe unavyoenda kununua cm la kichina kariakoo ili upate mawasliano kwenye mnara hiyo cm inakuwa mali ya tiGO/Voda/airtel/zantel/sasatel/bol? Acha ushabiki usiokua na kichwa wala mguu hapa tunajadili maswala ya taifa na sio pumba zako hizo.
   
 12. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  huo ni wizi..kwa nini ununue.wakati si mali yako?
   
 13. b

  bagain JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  mbunge aliuliza swali muhimu sana na waziri amejibu kulingana na utaratibu ulivyo kwenye makaratasi, lakini si katika kile kinachofanywa na tanesco kivitendo.

  Tanesco wanapaswa kurefund hiyo gharama ya nguzo, kama si kwa pesa taslimu basi mteja apewe units za thamani ya nguzo.
   
 14. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani kuna watu wapo duniani kupinga kila jambo linalokuja mbele yao, na mimi mara nyinga huwa sina muda wa kupoteza kupingana nao.
  Wabunge, rais na hata madiwani (vyama vyote) wana kawimbo wanakaimba eti ooh nimewaletea umeme, au nitawaletea umeme mkinichagua, swali linakuwa je atagharamikia miundombinu ya huo umeme? Kwani ni wangapi waliovuta umeme kwa gharama za rais, mbunge au diwani?
  Kwani mtu akienda pale TANESCO kuomba kuvuta umeme wanamwomba barua ya mbunge, diwani au barua kutoka ikulu?

  Kiukweli swala la kuchangia gharama ya huduma fulani silikatai moja kwa moja, ila basi kama mtu akijitolea kuvuta umeme pawepo na makubaliano(mkataba) fulani wa namna ya ku refund japo kidogo kidogo. Imagine mtu anaishi 10km kutoka ulipo umeme, na mtu huyu kweli anaweza kulipa gharama ya kuvuta umeme mpaka pale, tunamfikiriaje mtu huyu kwa zile milioni zake kadhaa anazotumi(achilia mbali kiasi alichohonga mpaka kukamilika mchakato mzima)?

  Ikumbukwe kuwa watanzania wanaotumia umeme ni chini ya 30%, lakini hii 70% iliyobaki sio kwamba wote wanashindwa kulipia tsh 5000/= kwa mwezi kwa ajili ya umeme. Watu wanashindwa kulupa kwa mkupuo mamilioni ya hela kuvuta umeme katika maeneo yao. Ukiongea na watu wa maeneo mbalimbali utasikia wanavyohitaji umeme.Binafsi nimeshuhudia maeneo kadhaa mikoa mbalimbali, wananchi wanajitolea kuchangishana hela kwa ajili ya kuvuta umeme, wakawatafuta mafundi wakafanya wiring ktk nyumba zao, lkn hadi sasa (zaidi ya miaka 5) umeme huo kwao ni ndoto.

  Je, tunapokuwa tunabisha hapa kijinga, tuanajua wawekezaji wanalipia kiasi gani ili umeme upelekwe kwenye maeneo yao? Je, wawekezaji, let's say migodini, wanaanza kulipa kodi baada ya muda gani? Mimi siamini kuwa TANESCO(serikali) wanashindwa kujenga miundombinu ya umeme kuwafikia wateja. Kama zaidi ya tsh 3bil. zinaweza kutumika kutafutia ubunge kwenye jimbo moja tu, sidhani kama kiasi hicho kingetumika kusambaza umeme pale Igunga,wanaigunga wote waliojiandikisha wangepiga kura na wangeendelea kuichagua ccm miaka yote ya uhai wao.

  Mimi naamini wachangiaji wengine humu JF wanajua maisha ya pale Mbezi Beach pekee, na wanafikiri watanzania wote wanaishi maisha ya vile. Au wanaishi maeneo ambayo umeme upo full 24/7. Na wakisikia mbunge fulani akihoji uhalali wa jambo kubwa kama hili anaona ni hadithi za abunuasi. They can't be serious. Jaribuni angalau (hata kwa kutalii tu) kutoka hapo na muende mikoani, vijijini huko ili muwaone walipa kodi wenzenu wana maisha gani.

  This is serious issue. Serikali inaweza kuwasaidia wananchi na hilo hata Ngeleja anajua. Ni kitendo cha kuamua tu. Sio kulalamila tu umasikini kwamba watu wanaishi kwa chini ya dola moja. Hili ni jambo la kuweka pembeni tofauti zetu na kuisukuma serikali ili ihakikishe kwamba panakuwapo na magawanyo sawa wa rasilimali tulizonazo.

  Napenda kuishauri serikali kwamba umeme ni kigezo kikuu katika kuwakwamua wananchi kutoka tope hili la umasikini tulionao. Watu wanahitaji umeme, wanaweza kulipia bili kwa mwezi. Tatizo ni gharama kubwa ya miundominu yake, watu hawawezi na hawatweza kamwe bila support ya serikali.

  Watu wanahitaji umeme, sio barabara za angani. Hao watu wanaosababisha msonagamano huko, wamefuata umeme. Waleteeni umeme huku muone kama wataendelea kutoka mijasho huko.
   
 15. k

  kuungutana Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Wadau natatizika sana na namna Tanesco wanavyoweka umeme kwenye nyumba hasa pale inapohitajika kuweka nguzo za umeme iki kumfikia mteja wao.Tanesco huwa wanamuuzia nguzo hizo mteja na baada ya hapo zinakua mali ya Tanesco tena,na mteja analipia gharama za matumizi yake bila compensation yoyote.Hili mnalionaje wadau?

  Nawakilisha!
   
 16. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ingetakiwa tanesco ndio waweke miundombinu alafu wananch wafanyiwe servec line tu!
   
 17. i

  ivungwe New Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nimelipia wiki 3 sasa hata simu sijapigiwa!sijui nikalalamike?
   
Loading...